Anthony Joshua afanikiwa kumtwanga Wladimir Klitschko katika pambano la uzito wa juu

Anthony Joshua afanikiwa kumtwanga Wladimir Klitschko katika pambano la uzito wa juu

Mimi kwa mtazamo wangu naona bado dogo hajapata mpinzani wa kweli.....ninaamini kabisa kama Wladimir Klistchiko angekuwa kwenye prime yake.....AJ angepoteza pambano kwa KO.....

Naweza kusema kuwa uzee umechangia kwa kiasi kikubwa sana kupigwa kwa WK.....

Hakuwa kwenye speed tuliyoizoea kwenye ringi.....

Naweza kusema kuwa kapigwa upper cut ya kizembe sana maana ni kama alikuwa anaisubiria.....

Kwa mchezo wa leo kama Aj angecheza dhidi ya bondia mwenye kasi.....nadhani round ya 5 tungekuwa tunazungumza mengine....

AJ anatakiwa ajiimrishe kiulinzi zaidi...bado mapema sana
 
tupa kule ule mpambano ulioitwa wa karne kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquio ambalo lilitikisa dunia kwa wakati ule tukishuhudia Mayweather akichomoza kwa ushindi wa points yani ushindi wa mezani.

wiki ijayo ule utamu wa boxer unarudi tena duniani na hili ndio pambano la karne, wiki ijayo dunia itakuwa kijiji wakati wanaume wawili wakishuka dimbani kati ya Wladimir Klitschko na Anthony Joshua

mimi karata yangu natupa kwa Wladimir Klitschko ngumi 1 kilo 100 wewe je???

let's get ready to the rumbleeeeeeeeeeeeeeeeeee
ebwana wacha dogo joshua anatisha kinoma
 
Kwanza hizi ngumi siziamini kabisa nasikia huwa kuna makubaliano mmoja apigwe raundi fulani, hilo lipo hasa lenye hela kama hizo.
 
Sijaona pambano la maana hapa, wala sijaona boxer hapa.

Mtu ana miaka 41 bado unamsubirisha hadi raudi ya 11, tena akiwa anaongoza kwa point?

Antany hakuna kitu, basi tu zali imemdondokea ila hauna kitu, hata kwa waingereza kina Player boy, Haye au Fury sidhani kama atatoka.

Baada ya Lenox Lewis sijaona tena boxer mwingine miaka ya hivi karibuni.

Boxers wangu wa muda wote ni Smoking Joe Frazier, Tysn, Lewis na kidogo Money ingawa aliniudhi sana kupaki basi mechi yake na mfilipino.
 
AJ ameshinda lakini naona hajafurahia ushindi wake kama vile inavyo takiwa.

ila mm namshauri klitschko huu ndio muda wake sahihi wa kustaafu ngumi
saazi aangalie maisha mengine aachane maisha ya kuwaza kila siku kuingia ulingoni.
 
Ni kweli mkuu, yaani ile round ya 5 hata ningeingia Mimi ningemaliza mchezo, maana AJ pumzi ilikata hata kutembea ilikuwa tatizo, na mikono ilikuwa haichomoki kabisa. Kwa uzee wake akambwelambwela weeee hadi Dogo aka-recover.

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Joshua ameshinda lakini ukweli utabaki ukweli sio bondia mzuri anakata punzi mapema ni mzito na mvivu.....kinachombeba ni vitu viwili cha kwanza ni ujasiri akiamua kushambulia anashambulia kweli na hampi mpinzani wake nafasi ya kujipanga na kingine ni dogo ana ngumi nzito sana....................anahitaji kufanyia kazi sana mapungufu yake round ya tano alichoka mno yaani alishakata tamaa sijui kwa nini klitsko na uzoefu wake wote alishindwa kumaliza pambano pale
 
I
Jamani lazima tukumbuke ile ni heavyweight.
Si mchezo wa kitoto.

Mie nampongeza sana AJ kwa skills zake. Kama utafuatilia vizuri, AJ ana ngumi nzito sana na anazipeleka nyingi kwa haraka sana kiasi kwamba hata ukiweka guard haisaidii.

Alichokifanya AJ baada ya kwenda chini, alijivuta hadi kengere. Baada ya hapo alikua mpole akivuta pumzi wakati klitschko alikua anatafuta the best punch amalize mchezo. Dogo akawa anamuharibia target.

Baada ya kupata pumzi dogo akajitoa muhanga maana angesubiri hadi round ya mwisho points zingembeba klitschko, kwahiyo klitschko akijua ile knock down bado mmempoza dogo hawezi tena makeke, dogo akamstukiza. Kilichomaliza pambano na hadi mnamuona klitschko alilainika ni ile uppercut ya mwanzo ambayo mtu mzima alielewa kabisa. Pia dkk zilikua bado nyingi kufikia kengere hivyo hakupata muda wa kukaa sawa na dogo akajitoa muhanga zaidi kwa kuendelea kumnyeshea za kutosha hadi anaondoka mara ya pili, na ya tatu kukosa refa kuingia kati basi angedondoka vibaya zaidi ya kuchanwachanwa kabisa.

Bado nampongeza AJ....kajitahidi sana sana na anastahili ushindi ule.
It was a thrilling fight I ever witnessed, Hii gemu imenirudisha nyuma nkaikumbuka Rumble in the Jungle pale Kinshasa kwa Mzee Mobutu seseseko
 
Hapo ndo
Joshua ameshinda lakini ukweli utabaki ukweli sio bondia mzuri anakata punzi mapema ni mzito na mvivu.....kinachombeba ni vitu viwili cha kwanza ni ujasiri akiamua kushambulia anashambulia kweli na hampi mpinzani wake nafasi ya kujipanga na kingine ni dogo ana ngumi nzito sana....................anahitaji kufanyia kazi sana mapungufu yake round ya tano alichoka mno yaani alishakata tamaa sijui kwa nini klitsko na uzoefu wake wote alishindwa kumaliza pambano pale
Pananiuma sana kiongozi, yaani nshaanza kushangalia kabisa, watu wote kimyaaa, sijui Wladmir alishindwa nini kumaliza gemu hapo hapo
 
Hi
Haunishindi mie. Nilikua natetemeka mbaya....round ya 11 nataka kusimama nishangilie nikajikuta kumbe nilipanda juu ya kabati, hata sijui nilifikaje Ikabidi niitishe stuli na kiti ili niweze kushuka. Waifu ananishangaa nilipanda kutafuta nini na nilipandaje maana nilikua peke yangu naangalia na si kwamba watu walijaa wakaniziba nisione screen.

Haya mambo tuyaache tu kama yalivyo.
Mzuka huo kiongozi, mi nkuwa napiga kelele tu ndani yaani kama napigwa mimi
 
Awali ya yote napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa watanzania wote mlioanza kulifuatilia pambano hili siku 3 zilizopita ama masaa machache kabla ya mpambano kuanza, hivyo kikubwa mlicho kiona kwenu ni kushabikia rangi ya mwili tu.

Niwashukuru pia kwa mayowe makali mliyopiga kutoka kila pande ya jiji la Dar na kuashiria kuwa bado mnamchukia Mzungu ati kisa tu aliwatawala.

Wengi wenu sio wapenzi wa mchezo wa Ndondi kwa sasa na miaka ya hivi karibuni. Wengi wenu hamumjui Wladimir Klitschko na wala hamumjui Antony Joshua...ila tu kwa kuwa mmekuta ndio jambo lililo na kick Duniani basi na nyie mkatumbukia na kushabikia kuliko hata wale mlio wakuta.

Nirudi kwenye pongezi kuu na za pekee ambazo zinakwenda kwa mwana Masumbwi Wladimir Klitschko ambae ndie bondia wa uzito wa juu kipenzi cha wengi Duniani kwa sasa. Bondia huyu mwenye rekodi ya kumiliki mkanda wa Uzito wa juu wa Dunia kwa miaka 9 mfululizo ni bondia bora kabisa ambae ameweza kuusimamisha uzito wa juu wa mchezo huu uwe na heshima. Pongezi hizi kwake ni kitendo chake cha kuomba haraka pambano la marudiano kati yake na bondia mchanga asie na jina wala mashabiki katika kila kona ya Dunia Antony Joshua.

Wladimir Klitschko Usiku wa kuamkia hii leo amepoteza pambano lake dhidi ya bondia huyo aliekuwa anapambana kwenye ardhi ya kwao, huku akishangiliwa na maelfu ya raia wenzie, lakini cha kuchosha zaidi ushindi huo amekwenda kuupata kwenye liuwanja la Mpira, mbaya zaidi ushindi huo wa bahati ameupata huku Wladimir Klitschko akiwa anaongoza kwa pointi nyingi tu.

Kwa kuonesha wazi kuwa yeye ni bora zaidi, bondia Wladimir Klitschko alimtwanga gumi moja takatifu na kufanikisha kumlambisha dogo ardhi ya nchi yake...kwa wanaojuwa masumbwi na kumjuwa Wladimir Klitschko basi ni wazi kabisa tunafahamu kuwa pambano liliishia pale. Ujasiri wa dogo kukomaa na pambano ni kutokana tu na makelele ya raia wenzake ambao waliuvaa uzalendo kabla hata mabondia hawa hawajapimwa uzito.

Katika mapambano machache aliopambana, Bondia huyu Antony Joshua alikuwa akiringa kuwa hajawahi kupigwa jeb mpaka kuanguka chini, lakini rekodi hio kwa sasa hana tena, na amebaki nayo kaka yake Wladimir Klitschko ambae katika kupigana kwake masumbwi kote mpaka alipo stahafu hakuwahi kuangushwa, huyu anajulikana kwa majina Vitali Klitschko ambae alikuwa bingwa wa Dunia wa Uzito wa Juu kwa mikanda yote, kabla ya kuja muachia mdogo wake Wladimir Klitschko.

Kwa watu wanaoujuwa mchezo huu wa masumbwi, sambamba na kumjuwa Wladimir Klitschko tunajuwa nini kitaenda mpata dogo Antony Joshua katika mechi ya marudiano. Mbaya zaidi kwa dogo huyu ni kwamba kama akijidanganya na kukubali kwenda kurudiana na Nguli huyu katika Ardhi ya Marekani ama iwe Madison Square Garden, ama iwe Trump Tower basi ni lazima apokee kipigo ambacho waingereza wenzie hawatakuja kukisahau. Kwenye ardhi ya marekani kuna watu wanaojuwa Ndondi na sio wapiga makelele ambao wengi wao walikuwa walevi na cha msingi kwao ni utaifa.

Namuonea huruma Joshua kama atakubali kusaini kupambana na Wladimir Klitschko katika ukumbi wa MGM Grand uliopo Las Vegas Nevada nchini Marekani, kwani umauti waweza mkuta humohumo.

Katika ukumbi huu wa kihistoria, dogo huyu Joshua atashangiliwa TU atakapo fanya shambulizi la maana mwilini mwa Wladimir Klitschko, kitu ambacho sioni kama kina nafasi siku hio. Dogo anatakiwa ajiulize kwanini bondia Muingereza mwenzie Tyson Furry alikuwa yupo tayari hata kufungwa jela ili tu asirudiane na Klitschko. Furry alijitetea na kukataa katakata kurudiana na bondia huyu na kusema kuwa yeye binafsi anatumia Madawa ya kulevya hivyo hawezi kupigana tena na Wladimir Klitschko .

Katika Ukumbi wa MGM ukumbi ambao Wladimir Klitschko hupendelea zaidi na zaidi kuvaa bukta yake nyekundu na Gloves nyekundu hakuna alietoka akiwa salama, kuna ambao walishindwa kuongea baada ya pambano, kuna walio ng'oka meno, kuna walio vunjwa taya, lakini hakuna ambae alitoka bila kuchanwa usoni na kutolewa damu...

Gang Chomba
 
Joshua amelamba ardhi, Huyu babu klischoko sio wa mchezo mchezo

Naona mods hawaelewi maana ya thread yako uliyoiita ya fans wa AJ

Wamekuja kuunga humu, sasa ikija fight ingine yake AJ naona wanataka uanzishe tena ya fans.... inasikitisha at times maamuzi yao.

Ila tunawazoea bila kuingia humu na kuwafikiria wengi wao, unaweza rudi nyuma ukakosa na furaha.
 
Joshua ameshinda lakini ukweli utabaki ukweli sio bondia mzuri anakata punzi mapema ni mzito na mvivu.....kinachombeba ni vitu viwili cha kwanza ni ujasiri akiamua kushambulia anashambulia kweli na hampi mpinzani wake nafasi ya kujipanga na kingine ni dogo ana ngumi nzito sana....................anahitaji kufanyia kazi sana mapungufu yake round ya tano alichoka mno yaani alishakata tamaa sijui kwa nini klitsko na uzoefu wake wote alishindwa kumaliza pambano pale
lakini kumbuka alikuwa anapigana na bingwa wa dunia.
 
Joshua ameshinda lakini ukweli utabaki ukweli sio bondia mzuri anakata punzi mapema ni mzito na mvivu.....kinachombeba ni vitu viwili cha kwanza ni ujasiri akiamua kushambulia anashambulia kweli na hampi mpinzani wake nafasi ya kujipanga na kingine ni dogo ana ngumi nzito sana....................anahitaji kufanyia kazi sana mapungufu yake round ya tano alichoka mno yaani alishakata tamaa sijui kwa nini klitsko na uzoefu wake wote alishindwa kumaliza pambano pale
Hakuchoka mkuu bali alipigwa ngumi ya kidevu network ikakata. Alikua anaombea kengele ilie tu.
 
Naona mods hawaelewi maana ya thread yako uliyoiita ya fans wa AJ

Wamekuja kuunga humu, sasa ikija fight ingine yake AJ naona wanataka uanzishe tena ya fans.... inasikitisha at times maamuzi yao.

Ila tunawazoea bila kuingia humu na kuwafikiria wengi wao, unaweza rudi nyuma ukakosa na furaha.
Wangeurekebisha tu wanavyotaka wao ila ubaki uzi maalum wa A. Joshua ingekuwa poa...... Tungetupia na rekodi zake zote za nyuma uzi ungenoga.!
 
Wangeurekebisha tu wanavyotaka wao ila ubaki uzi maalum wa A. Joshua ingekuwa poa...... Tungetupia na rekodi zake zote za nyuma uzi ungenoga.!

Ndio kitu huwa sielewi why mtu anakuwa anachukua hatua bila kuelewa.
 
Back
Top Bottom