Anthony Mavunde aiomba Wizara ya Nishati kutoa matangazo ya fursa katika ujenzi wa Bomba la Mafuta-Hoima

Anthony Mavunde aiomba Wizara ya Nishati kutoa matangazo ya fursa katika ujenzi wa Bomba la Mafuta-Hoima

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde amempongeza Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa za kuharakisha utiaji saini wa Mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Hoima - Tanga. Maana Mradi huo utatoa ajira zaidi ya elfu kumi na tano (15,000) kwa Watanzania.

Hivyo basi Mhe. Mavunde ameitaka Wizara ya Nishati kutoa Matangazo ya kuonyesha fursa zipatikanazo katika mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Hoima - Tanga ili watanzania waweze kujiandaa Katika kukamata fursa hizo

Pia, Mhe. Mavunde ameiomba wizara ya Nishati kuangalia namna watakavyo toa fursa kwa wajasiliamari wadogo wadogo Kama mamalishe (Wanawake) na vijana ambapo mradi huo unapita waweze kupata fursa za kufanya biashara zao.

#KAZIINAENDELEA

Screenshot_20210603-090214.png
 
Wanachofanya na alichofanya ni tofauti kabisa
 
Ikisoma kwenye vyombo vya habari vya nje ya nchi inaelekea bomba hilo linapigwa vita kali kuanzia vikundi vya mazingira hadi Banks zinazotakiwa kutoa mkopo wa kujenga bonmba hilo. Sasa sijui uhalisia umesimama wapi. Naona mikataba inatiwa sign. Ila nina imani Serikali ya Mama Rais wetu wapo makini na hivi vyote wanaviona. Let us give then support they will finally create jobs for our people.
 
Watu tuli-apply toka mwaka juzi - nafasi zimejaa!! zilizobakia labda ya kufyeka miti na nyasi linamopita bomba. (vibarua)
 
Back
Top Bottom