The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
KANISA KATOLIKI SI POPULISM.
Hata tukitoa nafasi ya kudhani kuwa WaandamaWAnaji walikuwa na nia njema, njia waliyotumia haiwezi kabisa kuzaa matokeo yoyote halali ndani ya mfumo wa Kanisa Katoliki.
Iwapo lengo lilikuwa kumuondoa Father & Padre Charles Kitima katika wadhifa wake kama Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), basi kikanisa na kisheria hilo haliwezekani hata kwa nadharia, na pengine hata kwa ndoto tu...!
Padre Kitima hawajibiki kwa Ubalozi wa Vatican, wala kwa waumini binafsi, bali kwa Mkutano wa Maaskofu wa Tanzania, chini ya taratibu rasmi za Kanisa....
Kwa lugha ya Canon Law waumini wa kawaida hawana locus standi ya kumwondoa kiongozi wa ngazi hiyo kwa hatua ya hadhara, wala maandamano hayaundi forum halali ya kikanisa.
Iwapo lengo lilikuwa kumtia shinikizo la kimaadili au kisaikolojia, basi pia Kanisa Katoliki si taasisi inayofanya maamuzi kwa misingi ya presha ya hadhara...
Uamuzi wa Kanisa hutokana na ushahidi, taratibu na busara ya kichungaji...
Na iwapo, kwa mtazamo mpana zaidi, tukio hili lilikuwa na ajenda ya kisiasa iliyojificha nyuma ya lugha ya dini, basi hapo ndipo hatari yake inapoongezeka maradufu.
KANISA SI POPULISM INSTITUTION
Hapa ndipo mantiki ya kikanisa ilipo.
Kanisa Katoliki ni taasisi ya hierarchical authority, si taasisi ya populist democracy.
Hili ni jambo la msingi linalopaswa kueleweka kabla ya kutoa hukumu yoyote...
Kwa mujibu wa Code of Canon Law (CIC, 1983), viongozi wa Kanisa huwekwa na kuondolewa kwa taratibu mahsusi, chini ya mamlaka ya Maaskofu na, kwa kiwango cha juu, Vatican kupitia Dicastery husika...
Dicaster ni idara au wizara rasmi ya Kanisa Katoliki, hasa uongozi wa Vatican, inayoshughulikia eneo maalumu la kazi za Kanisa. Hilo linatokana na neno la Kigiriki "dikasterion" ikimaanisha chombo cha utawala au mahakama ya kanisa...
Hakuna hata kifungu kimoja, nasema hata kimoja miongoni mwa vifungu vyote 1,752 vya Canon Law kinachotambua maandamano ya barabarani kama chombo cha kinidhamu cha Kanisa...
ZINGATIA:
Malalamiko, hata yakiwa mazito kiasi gani, huandikwa kwa heshima, huwasilishwa kwa Askofu husika, hujadiliwa ndani ya Mabaraza, na pale inapobidi, huwasilishwa Vatican kwa njia rasmi....
CC: THE BIG SHOW