Antinatalism vs Childfree: Mambo ya uelewa kati ya haya mawili

Antinatalism vs Childfree: Mambo ya uelewa kati ya haya mawili

MullaB

Member
Joined
Aug 22, 2023
Posts
24
Reaction score
12
Natumaini mko wazima wanna forum. Mada ya leo itahusu antinatalism na childfree. Nitaanza kwa kuweka hizi hoja mbili wazi kuwa kuna watu ni childfree (by choice) na pia ni antinatalist ila si kila antinatalist ni childfree. Nitaanza kuzungumzia watu childfree

Watu wanaochagua kuwa childfree kwa sababu wanaozijua wenyewe huchagua kutokuwa na watoto katika maisha yao, awe ni wa kuzaa au wa kufika. Sababu zinakuwa ni nyingi, na kila alietaka kuwa childfree Ana sababu zake binafsi. Wenzetu nje wanajua tolerance kwa hio mambo ya kuwa childfree hawashtuki sana. Ila kiafrica, kitamaduni haswa kwa wanawake imezoeleka kuwa hata kama asipopata mume basi lazma apate mtoto. Wanaoingia kwenye ndoa pia, watu huwa wanategemea.

Wawe na watoto. Na kama mnavyojua kwenye ndoa mtoto asipopatikana, analaumiwa mama. Anyway, watu childfree wanaamua kutokuwa na watoto. Watu walio childfree wawili, mke na mume pia wanaweza kuchukua maamuzi hayo. Pia imezoeleka kuwa watu childfree ni tasa, lakini sio. Alie tasa pia anaweza kutaka watoto lakini wa kufika (adopted) Sasa naongelea antinatalism.
Trigger Warning ahead

Antinatalism au anti-nataliism ni msimamo wa kifalsafa ambao hutoa thamani hasi kwa kuzaa/kuzaliwa. Kwa hivyo, wanaopinga kuzaa wenye hio falsafa wanasema kwamba wanadamu wanapaswa kujiepusha na kuzaa kwa sababu za kimaadili (ethics). Najua wengi mtashtuka kuhusu hii falsafa lakini ni falsafa inayoaminika na watu wengi sana. Falsafa hio huwa ina endana(intersect) na veganism. Antinatalists wanadai kuwa hakuna mtu duniani anaeomba kuzaliwa na hujikuta kuwa wamezaliwa bila kupenda.

Kama mnakumbuka story moja ya jamaa anejiita Raphael Samuel wa India alitaka kuoeleka wazazi court kwa tuhuma za kumleta duniani bila ruhusa (consent) yake. Tukio hili alilifanya kusudi watu wajue hio falsafa. Falsafa hii huweza kumleta hofu kwa kuwa watu wengi hasa Africa, tunaamini kwenye Abrahamic religion za Uislam na Ukristo. Katika Ukristo, biblia inasema zaeni muongezeke kwa hio hii falsafa haiwezi kueleweka hata siku moja.

Wakristo wengi wataona hilo jambo kama dhambi mbele za Mungu na kuipinga na kutotaka kusikia hio falsafa. Antinatalism imenukuliwa na professor mmoja nchi South Africa alie andika kitabu kiitwacho "Never to have been". Kuna mahojiano mengi kuhusu hii falsafa ila nimejaribu kueleza kwa ufupi. Antinatalists lengo Lao ni kujaribu kuounguza nafsi zitakazokuja kuteseka bila sababu yoyote. Karibuni kwa maswali na maoni yenu
 
Mimi nimechagua childfree lifestyle, sijawahi penda watoto ever na sidhani kama nitajutia.
I love spending money on myself na freedom…. machokuvimba wananisema hatari ila najua ni wivu tu lol
 
Mimi nimechagua childfree lifestyle, sijawahi penda watoto ever na sidhani kama nitajutia.
I love spending money on myself na freedom…. machokuvimba wananisema hatari ila najua ni wivu tu lol
Hey gorgeous! Inaonekana many Young Millenials na Gen Z tuna kuwa na mpanuko wa mawazo. Tupo kwenye information age. Sikuwahi kujua kuna childfree bongo. So glad to see the representation. Mimi ni antinatalism sympathiser. Nimepitia vitu vigumu in my life so I understand the philosophy. Congratulations girlie
 
Facts! Generation zetu ziendelee kujitahidi ili tusipangiane life, nawajua childfree watatu in their 40’s ila wanaficha wakiulizwa na society. I respect the antinatalism choice ( life is tough enough, why bring other folks to suffer)…kudos to you!
Ila wewe as a man its easy kuishi hii lifestyle bongo, kimbembe ni women smh
 
I'm just like you. Women get the sharp end of the stick yaani
Facts! Generation zetu ziendelee kujitahidi ili tusipangiane life, nawajua childfree watatu in their 40’s ila wanaficha wakiulizwa na society. I respect the antinatalism choice ( life is tough enough, why bring other folks to suffer)…kudos to you!
Ila wewe as a man its easy kuishi hii lifestyle bongo, kimbembe ni women smh
 
Back
Top Bottom