Antivirus MixTape: Sugu awachana Clouds FM

Antivirus MixTape: Sugu awachana Clouds FM

Itakuwa ile singo yake ya kuwapiga nyundo hao Clouds.
Na hivi katangaza kuhamia CHADEMA hawa CCM wanaweza zaa na yeye sasa hivi.


Nitaenda kuwashtaki kwa mganga wangu.... it seems is a serious case eeh, tutafikishana pabaya namna hii. Ndo maana sometimes rafiki yangu mmoja alikuwa ana-doubt kuandika hapa aikihoji usalama wa taarifa zake.
God Save Us
 
hey......cjui nini kimetokea mpaka amekamatwa....tupeni full data ili tujue kilichomsibu huyu nguli wa hihop tz
 
Nimepokea kwa mshangao na masikitiko makubwa hizi habari na kama ni za kweli basii huyu ndg yetu tushampoteza nakumbuka Lamwai ilivyokuwa, Mrema Lyatonga etc
 
Kinywa kilimponza kichwa wowo wowo! kujiunga Chadema mpaka uwe na matatizo wowow wowo,siku zote ulikuwa wapi wowo wowo,hiyo ndo song langu jipya ,vesi zake zimeenda shule
 
Nafikiri ndiyo maana walijiunga kwanza na CHADEMA wakifahamu kuwa kuna Wanasheria huko kwa ndani.

Kama watakuwa wamemkamata peke yake wakati Mix tape iko mtaani, itawajengea sura mbaya sana na wenzake itabidi waongeze mapigo ili kama ikibidi wakamatwe wote. Watawakamata hadi watachoka na kibaya zaidi, wanaweza kuwa ndiyo wanawapa umaarufu kwani kila mtu atataka sasa kufahamu kilitokea nini. Ngoja nizitafute hizi nyimbo. Nafikiri watoto wa Kihuni wataomba sasa hivi kibali kuandamana. Kama wasipoangalia, ndiyo wataelewa kwa mara ya kwanza nini maana ya wananchi kusema "we have nothing to loose."
 
Kuna taarifa kuwa Mr II Sugu yule aliye wachana live kituo cha radio amekamatwa. Mwenye taarifa kamili aweke hapa ni je ni sakata la kuwachana live wale jamaa au?

Source: Michuzi blog
 
jamani leteni taarifa kamili wengine tuko mbali na bongo, kafanyaje tena?
 
Nina huakika atakuwa alikuwa amejiandaa na hili baada hile nyimbo yake ya kuishambulia clouds.na kama msomaji wa JF atakuwa liona comments zetu na yangu ilisema vizuri kwamba wanaenda kumtia ndani huyu kutokana na nchi yetu mambo yanavyo kwenda.

kama alijiandaa kuwa mpambanaje wa kutetea haki za wanyonge basi haya ndio matokeo yake kwa nchi yetu.tusubiri wataamua kumfanya nini na kama haki itatendeka kwani yeye mambo aliyo rap yote yana ukweli.
 
Tusubiri kwanza tupate uhakika.

Kama ni kweli basi CHADEMA waitishe mchango wa pesa za WAKILI wakali sana wa kumtetea.

Kama tutawaachia hawa jamaa wasote peke yao, basi itakuwa tumelaaniwa.

Hawa jamaa wanaweza kuwaangusha MAFISADI wa Tanzania.

Kama siyo CHADEMA basi umoja wao utangaze michango ya hiyo pesa.

Itabidi kama kilichotokea JF ilipokamatwa, basi na sasa turudishe ule MOTO.
 
Kama ni kweli mimi nasema hilo ni bao la kisigino la Mr. Sugu, hakuna mtetezi wa haki wa kweli ambaye hajaonja machungu. PAMOJA NAWE SUGU mpaka kieleweke, kama huna nguvu za dola au bunduki kwa nini usitumie silaha uliyopewa na MUNGU ambayo ni mdomo?
 
Tusubiri kwanza tupate uhakika.

Kama ni kweli basi CHADEMA waitishe mchango wa pesa za WAKILI wakali sana wa kumtetea.

Kama tutawaachia hawa jamaa wasote peke yao, basi itakuwa tumelaaniwa.

Hawa jamaa wanaweza kuwaangusha MAFISADI wa Tanzania.

Kama siyo CHADEMA basi umoja wao utangaze michango ya hiyo pesa.

Itabidi kama kilichotokea JF ilipokamatwa, basi na sasa turudishe ule MOTO.

Kweli ngoja uhakika upatikana kwanza
 
Back
Top Bottom