Antony Joshua beats Eric Molina to retain IBF world heavyweight title

Antony Joshua beats Eric Molina to retain IBF world heavyweight title

Observer

JF HQ
Joined
Oct 18, 2006
Posts
189
Reaction score
299
Muda sio mrefu pambano la kugombea mkanda wa dunia uzito wa Heavyweight kati ya Muingereza Antony Joshua ambaye ni bingwa mtetezi dhidi ya Mmarekani Eric Molina litaanza.

Tujumuikeni hapa kufuatilia pambano hilo linalofanyika katika Jiji la Manchester Uingereza

4229.jpg

Rekodi zao

Joshua
kapigana mapambano 17 kashinda 17 knockouts 17 sare 0 kapigwa 0

Molina kapigana mapambano 28 kashinda 25 knockouts 19 sare 0 kapigwa 3

Update 1:
Mabondia sasa wanaingia uwanjani anaanza Molina kuingia uwanjani sasa

Update 2: Bingwa Joshua anaingia ukumbini akisindikizwa na mwimbo wa hate me now by Nas & Puff

=======================
Antony Joshua amefanikiwa kutetea ubingwa wake baada ya refa kumaliza pambano katika round ya 3 kumuokoa Molina asiendelee kupata kipigo kutoka kwa Joshua

Round 3:Joshua anamdondosha mpinzani wake, anahesabiwa anainuka pambano linaendelea Joshua anaendelea kumshambulia Molina ohhh pambano limeisha

Round 2: Pambano bado halika msisimiko inaonekana kila bondia anamsikilizia mwenzake. Round ya 2 imekwisha

Round 1: Imeanza kwa mabondia wote kuonekana kama wanasomana , round ya 1 imekwisha
 
Oh wow....kumbe mpo mnaofuatilia hii kitu...?

Safi sana.

Nilidhani niko peke yangu tu humu.
 
AJ...but anything can happen.

Vipi Dilian Whyte vs Derek Chisora?

Whyte vs Chisora wapo round ya 9 sasa

Pambano zuri sana ... hawa jamaa wamekamiana sana

Ila Chisora anaweza kuwa anaongoza kwa points

LOL AJ kiukweli ni mziki mwingine ila ngoja tuangalie

USA Baby lol
 
Whyte vs Chisora wapo round ya 9 sasa

Pambano zuri sana ... hawa jamaa wamekamiana sana

Ila Chisora anaweza kuwa anaongoza kwa points

LOL AJ kiukweli ni mziki mwingine ila ngoja tuangalie

USA Baby lol

Pande za huku hawaonyeshi bana huo mtanange wa Whyte na Chisora.

Kuhusu AJ, kusema ukweli bado hajawa tested kabisa yaani.

Lakini kadri siku zinavyoenda ndo atazidi kukabiliana na upinzani ulio bora zaidi.

Wale wapinzani wake wawili walopita ni kama vile walilipwa kwenda kusimama tu mbele yake.

Hawakupigana kabisa. Yule Charles Martin hakumpiga AJ hata ngumi moja. Aibu kabisa.
 
Wana weza kumuharibia joshua kwa kutaka apigane na heavy hitters haraka haraka mno

Inatakiwa waende naye kidogo kidogo, wakifanya hivyo anaweza kuja ku dominate uzito huo

LOL Charles Martin walivyokuwa wanamsifia nilijua AJ atapata shida ila duh ikawa vice versa
 
Whyte kashinda kwa points

Vipi, wamepongezana mwishoni au bifu limeendelea?

Ila Dilian huwa ananichekesha sana aisee.

Huwa namfuatilia kupitia IFL TV kwenye YouTube.

Halafu nahisi Chisora ana matatio ya akili.
 
Huyo Charles Martin hata alivoshinda huo ubingwa wake ilikuwa kdizaini tu.

Hakustahili kabisa kuwa bingwa.

Alienda pale kuchukua paycheck tu.
 
Vipi, wamepongezana mwishoni au bifu limeendelea?

Ila Dilian huwa ananichekesha sana aisee.

Huwa namfuatilia kupitia IFL TV kwenye YouTube.

Halafu nahisi Chisora ana matatio ya akili.

Yeah wamekumbatiana baada ya pambano ila kama Chisora hakuwa kwenye mood

Chisora nahisi atakuja kuwa hayuko sawa kama Frank Bruno
 
Huyu Molina vipi huyu....

Hahahaaa naye dizaini kaja kuchukua paycheck tu.

Utashindaje ndondi kama hurushi ngumi?
 
Hahahaaa....huyu jamaa hakuja kabisa kupigana aisee.

Hovyo kabisa yaani.
 
Jamani jamani chuma wanachopigana nacho sio cha mchezo mchezo , mmesahau wale jamaa waliokuwa wanapigana na Tyson, si kama hawa wakina Molina tuu.

Sijui wanakuwa wanaogopa ila ukiwa unamuogopa mpinzani wako halafu akakuwahi na ngumi kama aliyokula Molina ile iliyomuangusha lazima ufikirie mara 2 kama utataka kuendelea
 
Hapana bana...huwezi uka ignore quality of opponents.

Hata Tyson alipopigana na quality opponents alipata challenge.

Hivi uliona Tyson vs Holyfield?

Mtu unaingia ulingoni halafu hurushi ngumi unadhani utashindaje?

Afadhali mpambano ujao dhidi ya Klitschko.

Hopefully huo utakuwa mpambano kweli.
 
Back
Top Bottom