Antony Joshua Vs. Joseph Parker 31/03/2018 [Special Thread]

Kumbukeni hawa wote ni ma undefeated.so damu lazima imwagike, halafu antony joshua ndo mwenye pressure sababu dunia nzima imembetia yeye kushinda halafu yeye ndo yupo nyumbani. But nilivomuangalia Parker previous fights zake nadiriki kusema this fight won't be easy lazima kinuke
 
Umeongea bonge la poit mkuu huyu dogo watu wengi wanamchukulia kawaida tu lakini ana hatari yake
Kweli mkuu huyu Joseph Parker pia ni mvumilivu sana anaweza hata akaenda round mpaka hata ya kumi lazini speed ya makonde yake haipungui lakin Antony Joshua yeye amezoea kumaliza pambano mapema zaidi round za awali sasa akishakutana na mbishi asiyepigika haraka lazima impe shida. Sasa wewe fikiria wakati may be wamefika round ya nane wakati Aj amechoka mwenzie JP ni km anaanza. Labda pia Aj amalize pambano haraka kwa sababu huyu Aj ngumi anazorusha ngumi za mfululizo na ni nzito sasa kuweza kumuhimili ni ngumu vinginevyo anaweza akakuua. Kwa hiyo round tatu mpaka nne za mwanzo ukiweza kuhimili combination za Aj basi wewe ni mwanaume coz upigaji wake unafanana kidogo na Mike Tyson. Ukimuhimili hizo round unaweza kumpiga labda tu uzembee km alivyofanya Vladimir Klichko.

Pambano lingine Kali zaidi tunalisubiria la Dangerous Deontay Wielder na Aj. Kwa ule usugu Wa Wilder sipati picha.
 
Dillian whyte alipigwa round 7,klitchiko round ya 11,carlos takam round ya 10
 
Dillian whyte alipigwa round 7,klitchiko round ya 11,carlos takam round ya 10
Kikubwa ninachomaanisha ni kwamba Aj hana stamina za kuhimili round nyingi ukimfananisha na JP, refer pambano lake na Klitshko au lile la Carlos Takam. So hapa ni bora akamaliza pambano mapema coz the way round zinavyosonga anazid kuishiwa stamina ukimlinganisha na mpinzani wake, anyway pambano tutaliona SAA ngap?
 
Hili pambano ni moja ya mapambano makubwa kushudiwa duniani.
AJ anaweza shinda endapo atatawala kuanzia round ya 2 mpaka ya 10 baada ya chochote kinaweza tokea kwani mara nyingi upoteza stamina... Jamaa ana masumbwi makali sana compared to JP na mara nyingi anacheza kwa akiri sana huyu jamaa..
JP anawezashinda kama ataweza simama mpak round ya 10 kwani mpinzan wake anaweza kua kapoteza stamina.
Wilder ( BronzeBomber) ni bondia mjanja sana kama TBE uwa anategemea sana makosa ya mpinzani wake ili kushinda rejea pambano lake na KingKong(Luis Ortiz).. ni bondia mwenye mdhaifu kwenye kujirinda na katika mapambano alipigana ni moja tu ambalo kapiga na mtu ndan ya top 10 dunia ambae ni kingkong wengne dagaa tu huyu ili kuprove anatakiwa atleast ashinde kwa wafuatao joshu, parker, bigbabymiller na whyte

Kwa sasa AJ bado ni the best
 
Tujuzane na kachanel gani maana wengine tuna tumia makarai ya kitanzania
 
True & well said mkuu
 
Mimi ni team AJ kama nlivokuwa team Tyson miaka ya 90's.
Naona fight kuwa ngumu coz nmechek fight nying za parker ni mtu hatari.!!
AJ akipigwa pasaka yangu itaharibika aisee.
Kwa wadau wa masumbwi unaeza stream www.mamahd.com fight zimeanza za awali 9:30 it seem ndo fight yenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…