Katika Mahojiano na vyombo vya habari kupitia Mtandao wa Darmpya, Mbunge Peter Msigwa amefunguka na kuwatuhumu wabunge wenzake wa CHADEMA, Antony Komu wa Jimbo la Moshi Vijijini na Saed Kubenea wa Jimbo la Ubungo.
Msigwa amesema, "Hakuna shaka kuwa watu hawa Kubenea na Komu wamekuwa wenzetu kimwili tu, lakini kiroho wapo kwingine. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hawa wabunge wawili, mara ya kwanza sauti zao zilinaswa wakipanga kumuua na kumpoteza Mhe mbowe na Meya Boniface wa Ubungo"
"Ni mimi niliyekwenda nyumbani kwa mwenyekiti Mbowe usiku usiku nikiwa na biblia yangu ikiwa ni siku moja kabla ya kamati Kuu ya CHADEMA kuketi, lengo langu likiwa ni kumtaka mwenyekiti wetu, Mhe. Mbowe arudishe upanga wake kwenye ala, atoe msamaha kwa wabunge hao"
"Pamoja na wakati mgumu tulionao katika kukabiliana uonevu na ukandamizaji unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, wenzetu hawa wamekuwa "busy" kutushambulia sisi wenzao tulio mstari wa mbele dhidi ya CCM na vyombo vyake vya dola"
"Tena hili limenifanya nitafakari na kukumbuka kwanini wabunge hawa wawili hawakuwahi kufika hata Segerea wakati Mwenyekiti Mbowe alipofungwa miezi karibuni minne. Hawakuwahi pia kufika hata Kisutu kujua mwenendo wa kesi yetu, kuonesha upendo, umoja na mshikamano’’
Mbunge Msigwa anamaliza kwa kusema, "Licha ya mbunge kama Kubenea kuishi Dar es salaam, hajawahi hata mara moja kukanyaga Kisutu kwenye kesi ya viongozi wenzie wa CHADEMA. Bila shaka amekuwa akituombea dua mbaya ili wenzie tufungwe ndipo afurahi"
NOTA BENE: Historia inaonyesha kila ukikaribia Uchaguzi Mkuu wa ndani ya CHADEMA lazima kuna viongozi wa juu hupata misukosuko na kufukuzwa ndani ya CHADEMA. Kikombe cha misukosuko kwa sasa watakinywa kina Kubenea na Komu!
Kubenea alifanya juu chini ili Zitto Kabwe afukuzwe ndani ya CHADEMA wakati wa Uchaguzi ndani ya CHADEMA 2014, kwa sasa naye ni zamu yake kufukuzwa ndani ya CHADEMA.
Karma at its finest!
Tusishangae kumuona Kubenea kesho anaomba kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo, chama ambacho Kiongozi wake Mkuu alimfanyia fitna ili afukuzwe CHADEMA!