Antony Komu na Said Kubenea waivua nguo CHADEMA

Antony Komu na Said Kubenea waivua nguo CHADEMA

Siasa za uongo, au za kutumiwa na kike chama cha kununua watu hazitakusaidia kitu. Mbinu za kuua hivi vyama zikafanikiwa wanafuata ni watu
Wabunge wanamageuzi wa siku nyingi nchini wamegoma kuhama CHADEMA sasa wameamua kushughulika na Mbowe na vijana wake. Nasikia harufu ya Damu ndani ya CHADEMA

Sikiliza sauti ya Mbunge Komu na Kubenea wakijadili.

Wapenda mabadiliko wote wanapaswa kuwaunga mkono wabunge hawa. Wasiojielewa wataaminishwa kuwa hawa ni mamluki

 
Hivi kwanini wanaotaka mbowe ajiuzulu ni CCM? Kama CDM inaharibika chini ya Mbowe si ndio nzuri kwenu CCM?
Tatizo hamuelewi wana ccm, sisi tunataka upinzani uwepo lakini ubaki upunzani tu. Sio.kushika nchi.
Hii sababu ua kitaka mbowe atole.
 
Tatizo hamuelewi wana ccm, sisi tunataka upinzani uwepo lakini ubaki upunzani tu. Sio.kushika nchi.
Hii sababu ua kitaka mbowe atole.
Mngekuwa mnataka upinzani uwepo mngeruhusu mikutano ya kisiasa,mngeruhusu maandamano,mngefuta kesi kwa viongozi wa chadema etc
 
kinachoendelea ndani ya chadema kinasikitisha sana. Mbowe alitakiwa awe ameshajiuzulu siku nyingi ili upinzani upone.
Ndivyo LUMUMBA wanavyosema?, mko bize kumuondoa MBOWE. Katafuteni wasiojulikana kwanza kisha ndo mje CDM.
 
kinachoendelea ndani ya chadema kinasikitisha sana. Mbowe alitakiwa awe ameshajiuzulu siku nyingi ili upinzani upone.
Tumia akili kufikiri, kwanini nyinyi masisiemu msiuponye upinzani kwenye vile vyama vyenu visivyokuwa na wabunge wala diwani ili siku moja na vyenyewe vipate wabunge na madiwani?Ama kweli Mbowe anawanyima usingizi mabinti na wavulana kwaajili ya uchanga wa akili.Lakini pia anawanyima usingizi wanaume na wanawake wenye kale kagonjwa kaitwako kichaa.
 
Katika Mahojiano na vyombo vya habari kupitia Mtandao wa Darmpya, Mbunge Peter Msigwa amefunguka na kuwatuhumu wabunge wenzake wa CHADEMA, Antony Komu wa Jimbo la Moshi Vijijini na Saed Kubenea wa Jimbo la Ubungo.

Msigwa amesema, "Hakuna shaka kuwa watu hawa Kubenea na Komu wamekuwa wenzetu kimwili tu, lakini kiroho wapo kwingine. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hawa wabunge wawili, mara ya kwanza sauti zao zilinaswa wakipanga kumuua na kumpoteza Mhe mbowe na Meya Boniface wa Ubungo"

"Ni mimi niliyekwenda nyumbani kwa mwenyekiti Mbowe usiku usiku nikiwa na biblia yangu ikiwa ni siku moja kabla ya kamati Kuu ya CHADEMA kuketi, lengo langu likiwa ni kumtaka mwenyekiti wetu, Mhe. Mbowe arudishe upanga wake kwenye ala, atoe msamaha kwa wabunge hao"

"Pamoja na wakati mgumu tulionao katika kukabiliana uonevu na ukandamizaji unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, wenzetu hawa wamekuwa "busy" kutushambulia sisi wenzao tulio mstari wa mbele dhidi ya CCM na vyombo vyake vya dola"

"Tena hili limenifanya nitafakari na kukumbuka kwanini wabunge hawa wawili hawakuwahi kufika hata Segerea wakati Mwenyekiti Mbowe alipofungwa miezi karibuni minne. Hawakuwahi pia kufika hata Kisutu kujua mwenendo wa kesi yetu, kuonesha upendo, umoja na mshikamano’’

Mbunge Msigwa anamaliza kwa kusema, "Licha ya mbunge kama Kubenea kuishi Dar es salaam, hajawahi hata mara moja kukanyaga Kisutu kwenye kesi ya viongozi wenzie wa CHADEMA. Bila shaka amekuwa akituombea dua mbaya ili wenzie tufungwe ndipo afurahi"

NOTA BENE: Historia inaonyesha kila ukikaribia Uchaguzi Mkuu wa ndani ya CHADEMA lazima kuna viongozi wa juu hupata misukosuko na kufukuzwa ndani ya CHADEMA. Kikombe cha misukosuko kwa sasa watakinywa kina Kubenea na Komu!

Kubenea alifanya juu chini ili Zitto Kabwe afukuzwe ndani ya CHADEMA wakati wa Uchaguzi ndani ya CHADEMA 2014, kwa sasa naye ni zamu yake kufukuzwa ndani ya CHADEMA.

Karma at its finest!

Tusishangae kumuona Kubenea kesho anaomba kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo, chama ambacho Kiongozi wake Mkuu alimfanyia fitna ili afukuzwe CHADEMA!
 
Mkuu MsemajiUkweli , ni wazi kuwa umeiweka habari kishabiki na hujaielewa. Unajaribu kuitumia habari iliyopita kujenga propaganda zako nyepesi na kuchanganya na mchakato wa uchaguzi ndani ya CHADEMA. Kwa hilo hujafanikiwa. Msigwa alikuwa anazungumzia Kikao kilichokwishafanyika huko nyuma. Na hata huo msamaha ulishatolewa. Ona soni na propaganda zako nyepesi dhidi ya vyama vya watu!
 
Mkuu MsemajiUkweli , ni wazi kuwa umeiweka habari kishabiki na hujaielewa. Unajaribu kuitumia habari iliyopita kujenga propaganda zako nyepesi na kuchanganya na mchakato wa uchaguzi ndani ya CHADEMA. Kwa hilo hujafanikiwa. Msigwa alikuwa anazungumzia Kikao kilichokwishafanyika huko nyuma. Na hata huo msamaha ulishatolewa. Ona soni na propaganda zako nyepesi dhidi ya vyama vya watu!
Wapambane wao ndani ya CHADEMA halafu unituhumu kuwa ninaleta propaganda!

Please, don't shoot the messanger!

Unaniambia sijafanikiwa, kwani nilikuambia ninataka kufanikiwa?

Angalia pia hii video ya audio ya pili iliyovuja!
VIDEO:
 
Back
Top Bottom