Antony Komu na Said Kubenea waivua nguo CHADEMA

Antony Komu na Said Kubenea waivua nguo CHADEMA

Ni propaganda tupu. Upuuzi wa kuunga unga ili kuwachafua watu.

WanaCCM hawapati usingizi kila wakisikia jina la CHADEMA au Mbowe likitajawa.

Kuwakumbusha tu, upuuzi kama huo ulishawahi kutengenezwa ikimuhusu.
-Lwakatare na ugaidi wa kutaka kumuua Zitto.
-Mbowe na Wema Sepetu wakitongozana.

Vipi ziliishia wapi?
 
Matukio yote ya kiharamia nchi hii hufanywa na chadema, ndo maana wanalaaniwa na kupata kilema cha maisha na bado maisha yatazidi kuwaadhibu hadi mje kutubu na kuwaomba radhi Watanzania, mazafanta!
Aliyekwama kumteka Zakaria ni nani?Aliyetaka kumdhuru Lissu ni nani?
Jiwe ananuka damu ndio maana hata misiba ya kitaifa hahudhurii
 
Ni kwa nini Komu hajaunga mkono juhudi mpaka sasa
 
Matukio yote ya kiharamia nchi hii hufanywa na chadema, ndo maana wanalaaniwa na kupata kilema cha maisha na bado maisha yatazidi kuwaadhibu hadi mje kutubu na kuwaomba radhi Watanzania, mazafanta!
Unahisi serikali inapenda kuchafuliwa?! Hata mtoto mdogo angejiuliza kama Ni kweli Chadema ndio hufanya matukio ya Kiharamia kwanini hawakamatwi? Je, serikali inawagwaya?!
 
Hapana ! Ni mbaya sana kwa nchi na upinzani....sijui kwa nini mh. Mbowe anajifanya kutoona athari ya kung'ang'ania madaraka....
CCM ndo inayong’ang’ania madaraka. Chadema wana madaraka gani?upinzani una madaraka gani kama una ubongo wa kufikiri?
 
Ni propaganda tupu. Upuuzi wa kuunga unga ili kuwachafua watu.

WanaCCM hawapati usingizi kila wakisikia jina la CHADEMA au Mbowe likitajawa.

Kuwakumbusha tu, upuuzi kama huo ulishawahi kutengenezwa ikimuhusu.
-Lwakatare na ugaidi wa kutaka kumuua Zitto.
-Mbowe na Wema Sepetu wakitongozana.

Vipi ziliishia wapi?
Hivi Chadema kinafikiri Jimbo la Ubungo bila kumweka Mtu wa aina ya Kunenea watalichukua ?
Hata kwa tume inayoundwa na Chadema wenyewe hawachukui hilo jumbo siku wakimfukuza Kubenea.

Propaganda na majungu yanadumishwa na Mbowe mana akili ya mjinga ni majungu.
Chadema kina bahati mbaya sana ,Chama kikubwa kinaongozwa na akili ndogo ya Darasa la saba aliyefeli form six.
Akili ndogo inataka iburuze akili kubwa ni lazima atumie ubabe sio hoja.

Nadhani hata Dr. Mashinji ameshamchoka huyo darasa la Saba Mbowe.
Mashinji anajipotezea Muda na riziki zake kwa kukaa na Chama cha familia badala wakati yule ni mtu wa kuongoza wizara. Mashinji anafaa kuwa katibu wa Wizara ya Afya lakini anapoteza muda wake na wajinga wasiojua mfumo wa Demokrasia ulivyo.
Hilo li Mbowe likajifunze demokrasia ndani ya vyama huko Marekani halafu aje aangalie na ushuzi anaoufanya ndani ya Chadema
 
Sauti hizi 'zinatajwa' kuwa ni za Anthony Komu na Saed Kubenea, kwa mujibu wa sauti hizi wanapanga kumdhuru Meya Boniphace Jacob ambaye ni mtu wa karibu wa Mbowe, kwa mujibu wa hizi sauti ni kwamba lengo la kutaka kufanya hivyo ni kumdhoofisha mwenyekiti wa sasa wa Chadema yaani Mbowe.

Baada ya kusikiliza hayo mazungumzo, weka mambo yafuatayo akilini kabla ya kukoment

i) Uchaguzi wa viongozi ktk nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo uenyekiti unakaribia kufanyika ndani ya Chadema, na Anthony Komu ni miongoni mwa wanatarajiwa kugombea uenyekiti kumng'oa Mbowe, kwahiyo hizi sauti zinaweza kuwa kweli wanapanga kumdhuru meya Jacob au Mbowe ametumia mbinu zake kuhakikisha kuwa Anthony Komu anachafuka kama alivyowahi kufanya kwa Marehemu Chacha Wangwe, Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, Samsoni Mwigamba nk

ii) Kama ni kweli Anthony Komu na Saed Kubenea wanapanga kumdhuru Meya Boniface Jacob, ni ushahidi wa wazi kuwa ndani ya Chadema kuna migogoro mikubwa sana ambayo hawaitafutii ufumbuzi na huenda ndiyo maana viongozi wake wanahama chama hovyo hovyo kwasababu hakuna kinachowaunganisha ndani ya chama.

iii) Hoja ya mwisho ni kwamba, je ni matukio mangapi ambayo viongozi wa Chadema wamekuwa wakihujumiana na kuumizana au kuuana ambayo hafuyajui??

iv) Kama ni kweli wana nia ya kumdhuru meya Jacob, wangefanikiwa kumdhuru unadhani wafuasi na viongozi wa Chadema wangesema nani anaudhuru upinzani?? Wangejitaja au wangesukuma hilo furushi kwa serikali ya Magufuli??

#Note Mwisho niseme sijawahi kuona upinzani wa kijinga kama huu unaofanywa na Chadema ktk nchi hii. Kabla sijamaliza, naomba kukujulisha kuwa ile post ya Malisa ya kulaumiana kuwa wanahujumiana ndani kwa ndani ameamuliwa kuifuta haraka iwezekanavyo, na ameifuta
Sijawahi kuona post ya kijinga.kama hii humu JF.wewe ndo wakwanza kuandika uharo kama huu.kuhujumiana kupo tu hiyo ni human nature kama YESU alisalitiwa sembuse watu wa kawaida?.Katika chama wanachoongoza kuhujumiana ni Ccm.kumbuka mpaka upinzani upite ujue ndani ya ccm watu wamehujumiana.cc mbeya mjini,Iringa,Arusha,n.k .Wasaliti wanafukuzwa.Serikali hii ya awamu ya 5 imeua wengi sana.kwa hiyo usishangae.Ila wewe usiige serikali yako kuua watu ni dhambi
 
Sauti hizi 'zinatajwa' kuwa ni za Anthony Komu na Saed Kubenea, kwa mujibu wa sauti hizi wanapanga kumdhuru Meya Boniphace Jacob ambaye ni mtu wa karibu wa Mbowe, kwa mujibu wa hizi sauti ni kwamba lengo la kutaka kufanya hivyo ni kumdhoofisha mwenyekiti wa sasa wa Chadema yaani Mbowe.

Baada ya kusikiliza hayo mazungumzo, weka mambo yafuatayo akilini kabla ya kukoment

i) Uchaguzi wa viongozi ktk nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo uenyekiti unakaribia kufanyika ndani ya Chadema, na Anthony Komu ni miongoni mwa wanatarajiwa kugombea uenyekiti kumng'oa Mbowe, kwahiyo hizi sauti zinaweza kuwa kweli wanapanga kumdhuru meya Jacob au Mbowe ametumia mbinu zake kuhakikisha kuwa Anthony Komu anachafuka kama alivyowahi kufanya kwa Marehemu Chacha Wangwe, Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo, Samsoni Mwigamba nk

ii) Kama ni kweli Anthony Komu na Saed Kubenea wanapanga kumdhuru Meya Boniface Jacob, ni ushahidi wa wazi kuwa ndani ya Chadema kuna migogoro mikubwa sana ambayo hawaitafutii ufumbuzi na huenda ndiyo maana viongozi wake wanahama chama hovyo hovyo kwasababu hakuna kinachowaunganisha ndani ya chama.

iii) Hoja ya mwisho ni kwamba, je ni matukio mangapi ambayo viongozi wa Chadema wamekuwa wakihujumiana na kuumizana au kuuana ambayo hafuyajui??

iv) Kama ni kweli wana nia ya kumdhuru meya Jacob, wangefanikiwa kumdhuru unadhani wafuasi na viongozi wa Chadema wangesema nani anaudhuru upinzani?? Wangejitaja au wangesukuma hilo furushi kwa serikali ya Magufuli??

#Note Mwisho niseme sijawahi kuona upinzani wa kijinga kama huu unaofanywa na Chadema ktk nchi hii. Kabla sijamaliza, naomba kukujulisha kuwa ile post ya Malisa ya kulaumiana kuwa wanahujumiana ndani kwa ndani ameamuliwa kuifuta haraka iwezekanavyo, na ameifuta
WAMEFUKUZWA
 
Mtaharibu sana juhudi za watanzania wengi za Kupigania Demokrasia.
Kama munampigania Dikteta asiye na nguvu yoyote zaidi ya hivyo vinafasi vichache anavuofanya uteuzi ndani ya Chama itakuaje Hicho chama kikishika Dola?

Mnaonaje CCM nao wakiandamana kuda kuwa Mwenyekiti wao aendelee miaka 40 mana yeye ni kiboko ya wapinzani!?

Jengeni mifumo sio kujenga mtu.
Manaabisha sana kwa kweli !!
Yani tangu mbowe alipobadili katiba ili awe kiongozi wa kudumu ndani ya Chama niliidharau sana Chadema na niliona anguko lake.
Mbowe alibadili Chama na hakujaua kuwa kuna wakati mgumu ungekuja mbele yake alifurahia chama na kutanua wakati wa JK ndio maana akalewa madaraka na kutamani kufia Kwenye Chama. Alikua akiwatisha na kuwadhalilisha kingono wanawake kwa sababu ya nafasi za ubunge lakini sasa awamu hii ni ya kusafisha dhulma pande zote.
Waliozoea dhulma waacheni watoke waje watu safi. Kinachotokea kwa Mbowe ni dhulma na madhambi aliyofanya wakati wa A 4 .

Itendeeni haki Demokrasia Kwenye nchi hii . Acheni ubinafsi muokoe Vizazi vijavyo , Chadema ni zaidi ya Mbowe. Kuna watu huko Mbeya,Iringa , Mpanda , Musoma , Kigoma Kagera ,Mwanza n.k walivuta mamilioni ya wanachama na mashabiki wa Chadema kwa kupitia kwenye mapito magumu ambapo wakati huo Mbowe alikua anakula bata tu huko Kwenye makasino Dubai. Kumuabudu Mbowe ni laana kubwa kwa chama na Taifa la Tanzania! Hizo formu chukueni mumpelekee Lisu awe mwenyekiti huko huko aliko. Mana kuna wenyeviti waliwahi kuishi uhamishoni na hata kuishi gerezani lakini nia thabiti ya mioyo yao ndiyo iliyokuwa inatumiwa na Mwenyezi Mungu kujenga spirit ya mabadiliko na kuwavuta watu kwa mamilioni.
Mbowe kuna roho ya kitapeli iliyoko ndani yake ,hivyo Mungu kamwe hawezi kuleta ukombozi kupitia matapeli na waongo. Kama mnabisha mtaona kitakachotokea siku Mbowe akitumia watu wake aliowapandikiza muda mrefu ili wamuone kama Mungu mtu asiyestahili kupingwa ndani ya chama na asiyeshindwa. Hakika wataondoka robo tatu ya viongozi wenzake hasa wale wa mikoa mingine na wilaya nyingine mbali na Hai.
vijana gani hao wanaoharibiwa labuda lumumba fc, ila vijana wa chama wa wako na mwenyekiti. pili, hao viongozi uliowataja kuwa ni kheri nguvu kubwa ilekezwe kwao ili wawe wenyekiti kuliko mbowe ni sawa kwani ni viongozi na wapigania chama wazuri ila muda wao bado chama bado kinatakiwa kuwa mikononi mwa jemedali mwenyewe kulingana na khari ilivyo kwa sasa. tatu,swala la kula bata mwanaume yeyote anakula bata ila tunatofautiana kipato na maeneo ya kulia bata kulingana na kipato. nne, kubadilshwa kwa kipengele so swala la mbowe ila ni wanachama wenyewe baada ya kuona vijana walioko bado hawafuzu kama sasa wanachama wanavyotaka aendelee. tano, ngono ipo tu ni kheri ya huyo aliyezalilisha ila kuna mtu amezalisha ila hamuongei. hitmisho, roho ya mtu ni roho hakuna roho isiyokuwa nautapeli ndani yake, kuondoka kwa 1/3 ya viongozi kwenda kuunga huhudi ni jambo njema na ni faida kwa usajili mpya ndani ya chama.
 
Chadema kuweni makini, Huu mpango aliuanza Musiba, Jacob anawaumiza kichwa, Jacob kuwa makini, Msizipuuze hizo sauti,
 
kinachoendelea ndani ya chadema kinasikitisha sana. Mbowe alitakiwa awe ameshajiuzulu siku nyingi ili upinzani upone.
Kwani hawana vikao vya maamuzi? Na kama vipo, nipe mrejesho waliamua nini. Vinginevyo hoja yako ni ya kuchonga ili kufitini haki za msingi za viongozi wa hicho chama!
 
CCM ndo inayong’ang’ania madaraka. Chadema wana madaraka gani?upinzani una madaraka gani kama una ubongo wa kufikiri?
Kwani ndani ya CHADEMA mwenye maamuzi ya mwisho ni nani ? Honestly speaking? Madaraka si tu kuongoza nchi, hata kuongoza chama tena kikubwa kama CHADEMA.
 
HAMA-HAMA ISIWAFEDHEHESHE, TUJADILI HILI LA KUBENEA NA KOMU; sio JINAI pekee huu ni UASI dhidi ya taasisi; Kupanga njama za kumdhuru Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob. Tena wanakwenda mbali na kupanga namna ya kumshughulikia mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa kuomba hata TAKUKURU wamfikie!

Hayo ni maneno kati ya mbunge wa Ubungo Saed Kubenea na mbunge wa Moshi Vijijini Anthony KOMU wakijadili namna sahihi ya kumaliza nguvu za Freeman Mbowe kwa kuteka na kujeruhi au kuwaua kabisa watu wa karibu yake, akitajwa meya wa manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob kwa sababu ni sehemu ya hao watu wa karibu!

Nilipoanza kupoteza imani yangu na Saed Kubenea! January 2, 2017 binafsi ndio ilikuwa mwisho wa kusoma magazeti yanayotokana na Kampuni yoyote ya Saed Kubenea. Nilipoteza imani yangu kwake baada ya kusaidia kupotea na kutokomea kwa Ben Saanane. Kubenea ametupotezea Saanane wetu kwa sababu ya chuki zake vs BEN.

Alileta kupitia gazeti la Mwanahalisi taarifa za UDAKU, umbea na uzandiki, habari za uchochoroni, bils kuwa na ushahidi wa kimantiki. Yote ilitokana na chuki yake kwa Saanane. Kubenea akasema kwenye habari hiyo kwamba waliokota karatasi iliyorushwa mlangoni katika ofisi yao (chanzo cha habari) na kuamua kutumia karatasi hiyo kuandika habari yenye kuonesha BEN kaonekana kijiweni.

Huyu Kubenea alikuwa na mtafaruku na BEN, hadi kufikia kumfungia Saanane kutotumia mtandao wa Mwanahalisi online, akaondoa akaunti ya BEN katika Server ya mtandao huo. Hapo Mwanahalisi wametumia siku saba kuandaa wasomaji (ukizingatia ndio wakati tunapiga kelele za Ben Saanane) ndio baadae wakaamua kuleta hiyo habari kwa data za kuokota mlangoni. "Ben aonekana akirandaranda mtaani"

Kwanini tusiamini kwamba anahusika kwa namna yoyote kutekwa kwa BEN? kama hana uhusiano, basi alishiriki kuendelea kumpoteza BEN baada ya hiyo habari yake kuchapishwa. Kwa sababu, wakati tukiwa katika taharuki ya wapi alipo BEN, Kubenea akajitokeza na gazeti lake na kuandika ambayo aliandika, upepo wa CCM ukahamia "Kubenea amesema Saanane yupo"

Njama za Kubenea na KOMU dhidi ya Mbowe na Meya Boniface Jacob! Hii yote ni sababu mbili kubwa, ndio msingi wa kuanza kujenga hizi mbinu za mauaji, kuteka na mashtaka! 1. Ubunge Jimbo la Ubungo 2020; 2. Uenyekiti wa CHADEMA 2019; HIZI ndio sababu za msingi za kwanini Kubenea ni butter sana kwa Freeman na yoyote anaemtetea!

KUBENEA nafahamu, anaamini Bonny ni 'threat' Ubungo come 2020, Anaamini Ubungo kwake ni ngumu, hivyo Bonny kwake ni tatizo (ndani ya chama). And yoyote ambaye ni rafiki wa Bonny kwake ni adui mkubwa. Si-Shangai hizi 'allegations' za kupotezwa. NA; Kuhusu uenyekiti wa CHADEMA, Kubenea ni kati ya watu wasiompenda na kuhitaji uwepo wa Mbowe. Ni mtu ambaye anahitaji yeye au mwingine kurios kwenye sideline yake kuwa mwenyekiti wa CHADEMA.

Ukisikiliza maongezi ya Kubenea katika clip hiyo ni wazi kuna msukumo mkubwa na nguvu kutoka lernte dola. Ni mtu ambaye anataka kupambana na Freeman kwa gharama yoyote. Ukisikiliza vyema, Kubenea anamsilkiliza KOMU wakati akipewa mkakati wa kumuangamiza Mbowe, ni kumharibia watu wake wa karibu wenye kuaminika. Anaetajwa hapo ni Boniface Jacob.

Wanakwenda mbele na kusema "Magufuli ni dhaifu kwa sababu ameshindwa kumshughulikia Mbowe kwa akili" wanatoa ushauri Mbowe ashughulikiwe na TAKUKURU, kupitia vitabu vya CAG. katika Sauti hizo za Kubenea na KOMU wanasema Mbowe ni rahisi kupambana nae kama tu utaweza kumfikia, unamfikia kwa kuangamiza watu wake wa karibu. Wakamatwe, wafungwe, au wauwawe, anatajwa Meya Bonny hapo.

Kwanini Kubenea anamchukia Mbowe?

Uamuzi wa Baraza Kuu wa kuwaondoa wabunge na madiwani kutoka makao makuu, wasipewe ukurugenzi, wakafanye kazi kwenye majimbo na kata (Lissu na Mbowe excluded) hapo ndio mtufuano ulianza. Kati ya ambao waliondolewa katika ukurugenzi wa makao makuu ni KOMU, Lwakatare na Waitara. Hapa Kubenea akaamua kuungana na kundi hili kulalamika, wakisema Mbowe kawaondoa makao makuu kimkakati.

Maslahi ya Kubenea ni yapi ndani ya CHADEMA?

KUBENEA nu mbunge wa Ubungo. Lakini pia ni Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers. Yeye (Kubenea) na KOMU wote ni wakurugenzi wa kampuni hiyo. Ni watu ambao wameoa sehemu moja (nyumba moja) Kwa mtazamo huo, ni wazi watu hawa wanayo maslahi ya pamoja ambayo yanawakutanisha. Wakihitaji kuwa na nguvu ndani ya CHADEMA na ushawishi makao makuu kwa maslahi ya kisiasa au binafsi au mengine ambayo yapo nje ya uwezo wangu.

Wakati huo wa marekebisho ya muundo wa utawala makao makuu, ndio wakati Esther Daffi (mzazi mwenzake na Kubenea) alipoondolewa makao makuu, nyuma yake (2015) amekosa uteuzi wa viti maalum. Nafasi akachukua Jesca Kishoa. Shughuli ikaanzia hapa. Kubenea na wengine ambao ni waathirika wa mabadiliko ya muundo wa utawala makao makuu wakatengeneza kikundi cha kumuondoa Mbowe madarakani. Kikundi hiki kinajulikana. Na dhamira yao inaongonzwa na Kubenea akisema "Mbowe amechoka, aondoke waje watu wengine"

Hapa sasa ndio mwanzo kuanza kuzaliwa makundi mengi ya vijana kwenye mitandao kijamii. Makundi yenye kumuunga mkono Kubenea. Moja kati ya kundi hilo ni "FRIENDS OF BAVICHA ORIGINAL" kundi ambalo nimekula 'kifungo cha maisha' kutorejeshwa humo. Kubenea amekuwa akitumia makundi hayo kusambaza propaganda na porojo kwamba anaonewa, anachafuliwa na kuonesha mchango wake hauna thamani. Amekuwa kiumbe wa kutafuta huruma kwa wanachama. Kidogo afanikiwe kabla ya kushtukiwa.

Kubenea na makundi yake hayo kwenye mtandao wa kijamii wa whatsApp wanamshambulia Mbowe na yoyote ambaye atathubutu Kumtetea Freeman kwa namna yoyote, hata kwa kutumia 'emoji' ni watu wa kali, hawakawii kukuita "mlamba NYAYO" ukiwakamata koromeo Kwenye hoja zako. Hata wakati ule Kubenea kavujishasha barua yake ya kujieleza kwenye kwa KM ni watu hawa walisema "Kubenea anachafuliwa"

Kubenea na Tuhuma za kuhama CHADEMA kwenda CCM..

Hizi sio tuhuma za leo, ni tuhuma zimetembea kwa muda mrefu. Ingawa ameendelea kuzikanusha. Amewajibika mara kadhaa kukanusha kuhamia CCM lakini bado anatajwa ni kati ya wabunge ambao wanakaribia "kujiuza". Hata shughuli za chama kushiriki ni kwa nadra sana. Aghalabu kumkuta anatenda kwa niaba ya CHADEMA.

KUBENEA amewahi kupewa barua ya kujieleza kutoka kwa katibu mkuu wa CHADEMA ambayo ilikuwa na tuhuma kadhaa zikiwepo kukiuka maamuzi ya kamati kuu na kuyapinga hadharani. Alituhumiwa pia kuzuia zoezi la CHADEMA ni msingi jimboni kwake. Anatajwa kuwa sehemu ya watu waliokwisha na kuchelewesha zoezi hilo sana.

Amekuwa mtu wa kupinga maamuzi yote ya kamati kuu na uongozi, alipinga maamuzi ya katibu mkuu vs Lilian Wassira pia maamuzi ua BAVICHA vs Kibona Dickson. Alilimwa barua kutoka kwa katibu mkuu kutokana na hilo. Ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani. Hakuhudhuria kabisa katika uzinduzi wa será mbadala za CHADEMA. Hii ilileta maswali, akasema "sio yeye pekee ambaye hakuwepo ukumbini"

Ushauri wangu katika hili;

Kimsingi nimekumbuka nyakati zile za Zitto na wenzake walipoanza kufuatiliwa kwa mpango wao wa mapinduzi ndani ya chama 2013, intelejensia ya CHADEMA ilikuwa Makini nyakati zile (sio sasa) waasi waligundulika mapema, wakashughulikiwa. Sasa hadi mwenyekiti anapangiwa kufanyiwa UASI, CHADEMA hawajachukua hatua kabla ba baada ya mpango mkakati kuvuja?

Sitegemei kusikia CHADEMA kama taasisi wakisema "tumezipata audio hizo na tunazifanyia kazi" utakuwa ni uzembe wa hali ya juu. Nyakati za mashaka nje ya chama, bado tunaendelea kuishi kwa 'kukumbatiana' na waasi ndani ya chama? CHADEMA imekutwa na kitu gani?

Hizi tuhuma ni jinai, ni UASI, licha ya kupelekwa polisi, muhimu zifanyiwe kazi ndani ya chama, hata wenye kuhusika na masuala ya 'intelejensia' wanapaswa kuwajibika, huu ni uzembe wa hali ya juu, taswira ya taasisi ni mwenyekiti, anaguswa vipi na 'wahuni' nanyi mpo?

Nyakati hizi sio za kumbembeleza yoyote ambaye anataka kufanya mapinduzi, UASI ndani ya chama, hawa hawana tofauti na wenye kuhamia CCM, kuwavua uanachama sio ujinga ni adabu, kuanza upya sio ujinga, wafukuzeni wote ikibidi, tuliingia mkenge mkubwa 2015, ni hatari.

Ushahidi unajitosheleza!

Namba ya mbunge wa Moshi vijijini, Anthony KOMU (CDM) katika kundi la whatsApp la "kanda ya kaskazini" ndio ambayo ilipakia ujumbe huo wa sauti, bila wengine kufahamu malengo ya kufanya hivyo.

Chini yake katika muktadha huo Kuna mjumbe mmoja (Joshua Bin Sira) alimuuliza KOMU kama ni yeye ameamua kupakia au kuvujisha ujumbe huo wa sauti, majibu ya KOMU yalikuwa ni yenye kutia shaka.

Ni namba halisi ambayo anatumia KOMU. Ni sauti halisi ya Kubenea na KOMU katika mazungumzo yao. Sababu za kurekodi ujumbe huo ndio hazifahamiki, ni bahati mbaya au ni kwa makusudi, hiyo ni kazi kitengo cha intelejensia ndani ya chama.

#MMM
You must not be serious mkuu,

Unamaanisha kuwa Kubenea ndio kampoteza Ben??

Tutasikia mengi sana mwaka huu.
 
Back
Top Bottom