1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Mtaharibu sana juhudi za watanzania wengi za Kupigania Demokrasia.anakoelekea ndo huko huko tunakokutaka, kama hutaki unga juhudi, na mtakufa nakihoro uchaguzi umekaribia na mbowe hata kwa kumchukulia fomu lazima awe mwenyekiti
Kama munampigania Dikteta asiye na nguvu yoyote zaidi ya hivyo vinafasi vichache anavuofanya uteuzi ndani ya Chama itakuaje Hicho chama kikishika Dola?
Mnaonaje CCM nao wakiandamana kuda kuwa Mwenyekiti wao aendelee miaka 40 mana yeye ni kiboko ya wapinzani!?
Jengeni mifumo sio kujenga mtu.
Manaabisha sana kwa kweli !!
Yani tangu mbowe alipobadili katiba ili awe kiongozi wa kudumu ndani ya Chama niliidharau sana Chadema na niliona anguko lake.
Mbowe alibadili Chama na hakujaua kuwa kuna wakati mgumu ungekuja mbele yake alifurahia chama na kutanua wakati wa JK ndio maana akalewa madaraka na kutamani kufia Kwenye Chama. Alikua akiwatisha na kuwadhalilisha kingono wanawake kwa sababu ya nafasi za ubunge lakini sasa awamu hii ni ya kusafisha dhulma pande zote.
Waliozoea dhulma waacheni watoke waje watu safi. Kinachotokea kwa Mbowe ni dhulma na madhambi aliyofanya wakati wa A 4 .
Itendeeni haki Demokrasia Kwenye nchi hii . Acheni ubinafsi muokoe Vizazi vijavyo , Chadema ni zaidi ya Mbowe. Kuna watu huko Mbeya,Iringa , Mpanda , Musoma , Kigoma Kagera ,Mwanza n.k walivuta mamilioni ya wanachama na mashabiki wa Chadema kwa kupitia kwenye mapito magumu ambapo wakati huo Mbowe alikua anakula bata tu huko Kwenye makasino Dubai. Kumuabudu Mbowe ni laana kubwa kwa chama na Taifa la Tanzania! Hizo formu chukueni mumpelekee Lisu awe mwenyekiti huko huko aliko. Mana kuna wenyeviti waliwahi kuishi uhamishoni na hata kuishi gerezani lakini nia thabiti ya mioyo yao ndiyo iliyokuwa inatumiwa na Mwenyezi Mungu kujenga spirit ya mabadiliko na kuwavuta watu kwa mamilioni.
Mbowe kuna roho ya kitapeli iliyoko ndani yake ,hivyo Mungu kamwe hawezi kuleta ukombozi kupitia matapeli na waongo. Kama mnabisha mtaona kitakachotokea siku Mbowe akitumia watu wake aliowapandikiza muda mrefu ili wamuone kama Mungu mtu asiyestahili kupingwa ndani ya chama na asiyeshindwa. Hakika wataondoka robo tatu ya viongozi wenzake hasa wale wa mikoa mingine na wilaya nyingine mbali na Hai.