Antony Mtaka aambiwe kwamba sera ya elimu ni ya kitaifa na siyo mkoa kwa mkoa

Badala ya kupambana kuanzisha mabweni au hostel kwa kila shule, yuko busy na hizo camps.

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Kosa la mtaka ni nn sasa? Maana sera ya elimu kitaifa ni kufaulu mitihani. Mtaka amekuja na mbinu ya kufaulu hio mitihan. Ww unakataa, kwa nn sasa?
Anaepinga wazo la RC Mtaka aidha hakwenda shule ama yu miongoni mwa wanaofaidika na ujinga wa wengi hapa nchini.
 
No comment here
 
Umeandika mengi sana lakini uelewa wako juu ya jambo hili ni mdogo sana.
 
We Ndalichako kwani na watoto wako wanasoma kayumba?
 
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kimuundo ipo Chini ya Serikali Kuu sio TAMISEMI

Tuanze hapa, ntaomba unijibu simply..

Kwa nini waalimu wanahamishwa na ofisi ya mkuu wa mkoa au mamlaka yao ya nidhamu ipo hapa?

"Unaposema Kimuundo ipo Serikali kuu na Sio TAMISEMI,"

pia unasema "Na Wizara ya TAMISEMI kimuundo ipo Serikali Kuu ingawa amepewa Jukumu la kusimamia Serikali za Mitaa".

Mbona Logically kauli hizi zinafanana?
Sasa napokwambia RC Office ipo TAMISEMI ambayo kimuundo ipo Serikali kuu lakini inasimamia S/Mitaa kuna tofauti na Kauli yako. Au niambie wewe Ofisi ya RC ipo chini ya wizara gani?

Au kwa nini mamlaka ya nidhamu kwa waalimu kimkoa yapo Ofisi ya mkuu wa mkoa na si huko TAMISEMI unaposema hakuhusiani na RC office
 
Tanzania kuna Sera ya Elimu?
Nani kaiona?
Inasemaje?
Tuwekeeni hiyo SERA YA ELIMU hapa kwenye Jamvi ili tujue kati ya Waziri na RC ni nani anaikiuka.

ni ndefu mkuu,
LAKINI KIUFUPI SERA IMEWEKWA NA WIZARA , LAKINI USIMAMIZI AU UGATUZI WA MADARAKA ULIHAMISHWA TOKA W. ELIMU. NDO MAANA TUKAMKATAA NALICHAKO KUINGILIA URATIBU:

NANUKUU:
Ukisoma Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ukurasa wa 5 kuhusu Utekelezaji wa Ibara ya 146(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) inayohusu ugatuaji. Katiba inatamka katika Sura ya Nane (kuhusu madaraka kwa umma), kwamba, madhumuni ya kuwapo Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi na hivyo kuwezesha Serikali za Mitaa kuwajibika kutekeleza kazi zake katika eneo husika.

Sheria za Serikali za Mitaa zinatoa majukumu kwa Halmashauri kuhusu elimu katika Kifungu cha 55 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Miji) ya 1982. Ni kwa mantiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Matangazo ya Serikali Na. 494 na 494A ya mwaka 2010 aligatua na kuiweka katika usimamiaji wa iliyokuwa OWM-TAMISEMI na sasa OR-TAMISEMI elimu ya awali, msingi na sekondari na kuacha iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushughulikia Sera katika masuala yote ya elimu na mafunzo.
........

MAJUKUMU YA TAMISEMI:
TAMISEMI inatekeleza majukumu yafuatayo:
i)Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Ugatuaji Madaraka (D byD), Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikaliza Mitaa, Maendeleo Mijini na Vijijini;
ii)Kuziwezesha Tawala za Mikoa kutekeleza majukumu yake ya kisheria;
iii)Kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yake ya kisheria;
iv)Kuratibu shughuli za utoaji wa huduma mijini kama vile usafiri na usafirishaji, upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira;
v)Kusimamia shughuli za Tume ya Utumishi wa Walimu;
vi)Kusimamia shughuli za Elimu ya Msingi na Sekondari;
vii)Kujenga uwezo wa watumishi wa OR –TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi; na
viii)Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programuna Miradi iliyopo chini ya OR-TAMISEMI.

Mheshimiwa Spika,majukumu yanayotekelezwa na Mikoa ni kama ifuatavyo:
i)Kuhakikisha kunakuwepo amani, usalama na utulivu katika Mikoa na Wilaya;
ii)Kusimamia na kuratibu shughuli zote za maendeleo katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
iii)Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa ili zitekeleze majukumu yake kwa ufanisi;
iv)Kufuatilia utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali zinazotekelezwa na Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maeneo yake;
v)Kuratibu usimamizi na uendeshaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
vi)Kusimamia uendeshaji wa Afya ya Msingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa; na
vii)Kuhakikisha kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi utawala.

.......

KUHUSU MTAALA WA ELIMU:
Tukija hapo kwenye Uratibum Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu sote tunafahamu kuwa kuwa kwa kiasi kikubwa Sera ya Elimu ni sera ya Taifa na Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia ndo yenye kuratIbu sera hii . Pia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndo inayoandaa mtaala wa Elimu kitaifa. Tunapaswa kukumbuka jambo moja kuwa ukisoma muhtasari wa Taasisi ya Elimu Tanzania. (2015). Mtaala wa Elimu ya Msingi Darasa la I–VII. Dar es Salaam: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia tunaona kuwa mtaala umetoa muongozo wa Idadi ya masomo pamoja na ya hiari .

Lakini pia umetoa muda ambao mwanafunzi anapaswa kufundishwa darasani. Pia huu Mtaala umeruhusu kuwa na shughuli za ziada mbazo zinaweza kupangwa hata na shule husika au mamlaka ya utekelezaji. Mfano wa shughuli hizo ni kama Michezo, Masomo kwa ajili ya kujijengea uwezo, sanaa, klabu za masomo, n.k . Haya masuala Mtaala haujayaweka bayana wala muda wake haujalaimishiwa kufuatwa bali kuna makadirio ya "At least" na hayana kuanzia muda gani mpaka muda gani. Hapa imetolewa idadi ya masaa kwa siku.

Kiuhalisia Muongozo ni Blueprint au Platform ya kufanyia jambo na huwa haijaweka masharti rasmi katika kutekeleza jambo bali umeweka vipengele muhimu tu vya kufuatwa. Hapa ndo kwenye shida, pale ninapokua muongozo na unaeleweka halafu umshauratibu then mimi nakuja na kukupangia namna ya uratibu ni lazima tutaona tatizo la ugatuaji madaraka.

Nanukuu ukurasa wa 49
"11.3 Shughuli za ziada katika MtaalaShughuli za ziada katika Mtaala zitafanyika kwa lengo la kuimarisha maarifa na stadi ambazo mwanafunzi amejifunza ndani ya darasa. Hii itamwezesha mwanafunzi kuchangamana na wanafunzi wengine pamoja na mazingira ya nje ya darasa. Muktadha huu huimarisha ujenzi wa maana kwa yale anayojifunza. Shughuli hizo zitajumuisha klabu za masomo na maeneo mengine ya kujifunza. Vilevile zitakuwepo shughuli za michezo, uzalishaji mali, utamaduni, malezi na unasihi. Shughuli hizi zitawezesha wanafunzi kujifunza kwa kina. Ufuatao ni ufafanuzi wa shughuli za ziada katika Mtaala:

a) Klabu za masomo
Klabu hizi zinahusisha masomo mbalimbali na klabu za masuala mtambuka. Hizi ni kama klabu ya mazingira, VVU na UKIMWI, jinsia na haki za mtoto. Nyingine ni kama klabu ya stadi za maisha, kupinga/kudhibiti rushwa, afya, uelimishaji rika, biashara na usalama barabarani.

b) Michezo na sanaa
Wanafunzi watahimizwa kucheza michezo mbalimbali ili kuibua vipaji na vipawa ambavyo vitapaswa kuendelezwa. Michezo itafanyika kwa wanafunzi wote kufuatana na ratiba itakayopangwa na shule husika. Michezo hiyo ni pamoja na: uigizaji, uimbaji na riadha. Mingine ni kama mpira wa miguu, pete, mikono, kikapu, wavu, meza, mchezo wa bao. Umahiri katika shughuli za michezo umegawanywa kimadarasa kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 20. - (Wale wa UMISETA na UMITASHUMTA, Mashairi, Ngonjera, Maigizo,n.k tunayajua haya na mpaka leo hii bado timu za shule zinafanya. Kuna wakati mnaweka kambi kabisa kwa ajili ya mashindano ya Volleyball tu)


AJABU NI PALE MTU ANAPOTAKA KUTENGANISHA KATI YA TAMISEMI MKOA NA OFISI YA MKUU WA MKOA.
 
Kwa maana hii ndiyo maana mfumo wetu unalaumiwa kwakua ni decentralization (political) centralization (budgets)...Ugatushaji haujakamilika kama ilivyokusudiwa katika ule mradi wa uboreshaji

Na hapa ndo tatizo lilipoanzia,
 
Mkuu wa mkoa yupo sahihi kwa upande wake sababu kaangalia mazingira ya eneo husika pamoja na uwezo na hali za wananchi wa eneo lake.

Waziri yeye anafata mtaala wa elimu ambao n mbovu kwa nchi yetu na Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye sera mbovu za elimu refer to;BRN, COBET, SEDP etc.

Kikubwa Mtaka pale alichojaribu ni kueleza hisia binafsi kuhusu kuongeza ufaulu kwa wananchi wake na hakukosea kabisa inawezekn yupo sahihi kwa mazingira yanayomzunguka.
 
Kwenda zako kule!
 
Anaepinga wazo la RC Mtaka aidha hakwenda shule ama yu miongoni mwa wanaofaidika na ujinga wa wengi hapa nchini.
wazo lake ni lipi? wewe umelielewa vingine zaidi ya makambi ya elimu kwa miezi miwili ijayo?
 
Badala ya kupambana kuanzisha mabweni au hostel kwa kila shule, yuko busy na hizo camps.

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
Hatujiulizi kwa nini wakoloni walijenga boarding schools kwa watoto wa kiafrika. Mazingira yetu nyumbabani ni magumu kiasi kwamba bila boarding, mchana kijana anakuwa mwanafunzi, jioni anarudi nyumbani na kuwa mwanakijiji sawa na waliokosa shule.

Mtaka analeta bhla! bhla! za kushindisha wananafunzi halafu ngumbalu wa JF wanashangilia eti Ndalichako kaambiwa. Yaani furaha ya waliobanwa na maisha naiona ni kila wanaposikia kiongozi katukanwa, kazomewa au hata kafariki. Shiiiida!
 
Boss, wengine tunafundisha Dodoma kwa miaka mingi. Mkuu wa mkoa hawezi kuja leo baada ya mwezi mmoja anajua matatizo yetu kuliko sisi. Hajatuuliza, hajauliza mwenyeji yoyote! Anahamisha aliyobuni Simiyu na kuyapanda hapa dodoma. that is foolishness!

Hizo BRN, etc. hazikuwa sera za elimu labda una hasira yako ktk familia. Taja kibaya unachokiona ktk sera ya elimu uoneshe kinavyoharibu elimu. Huenda hata hujawahi iona!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…