Mkuu unafahamu maana ya SERA.
Unafahamu kuwa Usimamizi wa uendeshaji wa Shule za Msingi upo Chini ya TAMISEMI?
Unafahamu kuwa TAMISEMI kimkoa inaongozwa na Mkuu wa Mkoa
Unafahamu pia majukumu ya kuhakikisha Ufauku katika shule za msingi mkoa ni la Tamisemi?
Suala la ratiba ya kutoka limewekwa na wizara ya Elimu , Lakini suala extra time au makambi kwa madarasa ya mitihani si Suala la kisera mkuu, Ni suala la Mikakati ya Ufaulu ndani ya mkoa.Kama halileti shida Wizara ya elimu haipaswi kuintervine sababu linaihusu TAMISEMI.
Woengi tunasahau kuwa Ofisi ya Mkuu wa mkoa ipo chini ya TAMISEMI kimkoa. Nilitegemea Ummy Mwalimu kuliingilia hili si Ndalichako sababu suala la uendeshaji wa Shule za Msingi ni ka TANISEMI
Tutafute maana ya SERA ya elimu kwanza ndo turudi
Wewe ndiye hufahamu kitu...
Sera ya elimu ni moja tu nchi yote. Hakuna kipande cha sera ya elimu kwa ajili ya RC Mtaka na mkoa wa Dodoma...!!!
Kutoka kwenye sera ya elimu tunapata KANUNI na MIONGOZO mbalimbali ya kielimu ya namna ya kuitekeleza sera hiyo...
Miongozo hii hutolewa na nani?
Hutolewa na wizara yenye dhamana ya elimu Tanzania chini ya waziri husika. Kwa sasa wizara hii ya elimu iko chini Waziri Bi. Joyce Ndalichako na kamwe siyo RC Anthony Mtaka...!!
TAMISEMI (ukiwemo mkoa wa Dodoma chini ya RC Mtaka) kamwe hazijihusishi na utoaji wa miongozo na sheria zao wenyewe. Wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa ni LAZIMA na SHARTI watekeleze miongozo itolewayo na serikali kuu kupitia wizara za kisekta....
Ni upumbavu na ujinga wa kukosa ufahamu kutumia ubovu wa shule za serikali za walala hoi kutaka Ku - justify uvunjaji wa sheria, miongozo na kanuni za usimamizi wa elimu unaofanywa na RC huyu...
Anachokifanya RC Mtaka ni vurugu and pure insubordination dhidi ya mamlaka iliyo juu yake and he deserves to be punished...
Ni ujinga tu na upumbavu wa wananchi wa kutoelewa kama wewe ndiyo maana hawaoni tatizo la RC huyu. Hii ni Magufuli mentality ya kufanya mambo nje ya utaratibu...
Serikali za mitaa chini ya TAMISEMI i.e halmashauri, miji, manispaa na majiji ni wakala (agencies) kwa ajili ya kutekeleza maelekezo ya kisera za kisekta toka serikali kuu...
Jukumu kubwa na la kipekee la serikali za mitaa ambalo wanaweza kufanya ni kutunga sheria ndogo ndogo (bylaws) ili kuwezesha utekelezaji wa sera za kitaifa za kisekta mfano elimu, afya, ulinzi na usalama nk na kamwe siyo kwenda nje ya mstari...
This is undeniable fact. Ukubali ukatae RC Mtaka, amevuka mstari wa uwajibikaji kwa alichokisema ili kumshambulia Waziri wa elimu Bi Joyce Ndalichako kijinga bila sababu...