hakuna hakika Juu ya Hilo mkuu maana mara ya mwisho habari zao kurekodiwa ni kule Mesoamerica hasa kwenye Maandiko ya wamaya na Aztec nk
Ukisoma baadhi ya vyanzo inadai Annunaki waliokua duniani walitofautiana wao Kwa wao sababu kubwa Ilikua ni jinsi ya kuwahandle binadamu Kuna baadhi Yao walitaka binadamu aendelee kua mtumwa wao Kuna wengine walidai binadamu anastahili kupewa ujuzi na maarifa makubwa afanane na wao,tofauti Ile ilikuja kuzaa vita kubwa kati ya pande mbili maana Enki aliyewafanya binadamu alitaka wakubalike na watambuliwe Katika jamii ya wanibiru ila ENLIL alikataa akidai lengo la binadamu ilikua ni kuwa vijakazi Katika Migodi Yao na baada ya mission kukamilika wanastahili kuondoshwa na kutoweshwa Katika tofauti zao wakakubaliana kuwaacha huru ila Kwa sharti wasipewe access ya advanced technology Bali wapate elimu ya ujuzi wa kawaida kama
Engineering,Music,uchimbaji madini mbali mbali,kufua vyuma nk yaani Ile nyepesi tu na baada ya hapo waliondoka kurudi Kwao Nibiru planet na hawajawahi rejea Tena baada ya kukaa duniani Kwa Miaka maelfu nyingi sana,huo ndio ukawa mwisho wa accient civilization za kale kama Sumerians, Assyrian, Babylon, Egyptian, Kush, Aztec, Maya, Peru, Indus valley kuanguka na binadamu Kuanza survive Katika Hali ya kawaida huku akibakia na dhana ya Mungu,Miungu kutoka juu akitumainia ipo siku watarudi kuwakomboa kwa shida zao,
Mfano kule mexico kwenye jamii ya Aztec na Maya walitoa kafara za binadamu Ili kutuma maombi Kwa Miungu hiyo irudi itatue shida zao mbali mbali
Angalia movie ya Apocalypto ya Mel Gibson utapata idea kidogo kwanini wale watu wanatoa kafara kwa Miungu jua au star gods ambao ndio hao ANNUNAKI!