ANUNNAKI: Nadharia za Mungu, miungu, fumbo la sciencenscience na Teknolojia kubwa katika Dunia ya kale, kuanguka Kwa civilization na kuinuka Tena

ANUNNAKI: Nadharia za Mungu, miungu, fumbo la sciencenscience na Teknolojia kubwa katika Dunia ya kale, kuanguka Kwa civilization na kuinuka Tena

hahahaha kama mnazijua si mshare hapa mnaishia kupiga mbinja tu huko hamleti madini ya kukanusha,mpaka Leo hii navyo andika hapa Habari za Annunaki hazina ukakasi Bali zina shahidi za kihistoria na tafiti za kisayansi,wewe kama unadhani Watu wanajua au wewe unajua mbona wanaotoa hizi Habari ni wachache na wengi wanakua hawana information zaidi ya kusoma Kwenye mabandiko yetu hapa?
Kitu kingine tushakizungumzia hapa Watu wengi wanaoendesha Mifumo ya hii Dunia Wanakanusha Habari za Annunaki na kuziita Zina mkanganyiko huko wakiujua Ukweli lengo ni kuogaopa kuukiri Ukweli mchungu utakao sababisha kuvunjika Kwa historia za Uongo katika nyanja zote za kiutawala katika historia ya Dunia,Leo hii haya madai yakikanushwa kua ni kweli mathalani utakua mwisho wa ulaji wa taasisi nyingi zilizojijenga Toka mwanzo hasa kuanzia za kihistoria,dini,utamaduni,Sanaa na Kila Kitu na itasababisha mass haisteria,
Hilo lengo lilishajadiliwa na UNESCO akiwa kama kibaraka wa hizo Nadharia njama ya kwamba mambo yote na historia ya Dunia ya ukweli Pamoja na makumbusho na kumbukumbu zote zenye utata zilizojengwa na Annunak ziwe nyara na Watu wasiambiwe ukweli kamwe waendelee kua watumwa wa fikra na kuendeshwa Kwa manufaa ya Watu wachache,
Leo angalia media,majarida,vitabu na machapisho mbali mbali yanavyopotosha juu ya sites zote zenye utata mfano ni kupotosha ya kwamba pyramids za Giza zimejengwa na Mapharao na ni Makaburi ya mumiani,
Tukija wauliza kama makaburi tu yamedumu mpaka Leo tunaomba mtuoneshe majengo waliyoishi wanabaki na kiwewe
Yaani Kwa Akili timamu mtu ajenge makaburi makubwa Kuliko nyumba anayoishi Ina make sense?
Haya tukiuliza na Zile Pyramids za Mexico ni Makaburi ya Pharaohs Gani mtajibu Nini?
Mnaopinga either ni lack of information na knowledge mkijificha Kwenye kichaka Cha utata na Udini nje ya hapo hamna jipya Wala hoja zenu hazina nguvu zaidi ya kupinga bila fact

Alamsiki!
Hatuleti wapi? Wakati wewe umesoma! Sasa unatetea kitu usichokijua bro? Legeza ndonga mkuu.

Mtafsiri fulani ambae alitafsiri rekodi moja ambayo inasadikika kuwa ni ya Annunaki, alikuja kukosolewa na mgunduzi mwenzake(ambaye hakuwa annunaki[emoji23][emoji23]) haya mambo yanachekesha sana.

Ngoja bro nitafute ule mstar wa critique nikupatie[emoji16][emoji16]
 
Kuna kusoma na kuelewa mambo na kusoma na kufyonza kama dodoki,jamaa wanafikiria hizo habari za anunnaki watu hawazijui au hazienei.
Wanashindwa kupata picha kwa nini zinakosa nguvu hizo habari kwa sababu kimantiki zinakosa uhalali wa kudhibitishwa Kwenye nyanja mbalimbali.
Zinakosa uhalali kihistoria,kisayansi,zinabaki kuwa mythology.
Kuna critics nyingi sana na zina mashiko kuhusu anunnaki,ndio maana tunasema hizo ni
PSEUDOSCIENCE.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Shida ni kwamba watu wanapenda kushikamana na hoja dhaifu na kuzipa nguvu. Wakati asili yake ni udhaifu[emoji16][emoji16]
 
Shida ni kwamba watu wanapenda kushikamana na hoja dhaifu na kuzipa nguvu. Wakati asili yake ni udhaifu[emoji16][emoji16]
Na udhaifu unakuja pale unapojua hiki kitu nidhaifu afu ukakubali tu kwasababu wewe ni dhaifu...

Mungu yupo mmoja tu staki kujua mambo mengine ya kiwaki
 
hahahaha kama mnazijua si mshare hapa mnaishia kupiga mbinja tu huko hamleti madini ya kukanusha,mpaka Leo hii navyo andika hapa Habari za Annunaki hazina ukakasi Bali zina shahidi za kihistoria na tafiti za kisayansi,wewe kama unadhani Watu wanajua au wewe unajua mbona wanaotoa hizi Habari ni wachache na wengi wanakua hawana information zaidi ya kusoma Kwenye mabandiko yetu hapa?
Kitu kingine tushakizungumzia hapa Watu wengi wanaoendesha Mifumo ya hii Dunia Wanakanusha Habari za Annunaki na kuziita Zina mkanganyiko huko wakiujua Ukweli lengo ni kuogaopa kuukiri Ukweli mchungu utakao sababisha kuvunjika Kwa historia za Uongo katika nyanja zote za kiutawala katika historia ya Dunia,Leo hii haya madai yakikanushwa kua ni kweli mathalani utakua mwisho wa ulaji wa taasisi nyingi zilizojijenga Toka mwanzo hasa kuanzia za kihistoria,dini,utamaduni,Sanaa na Kila Kitu na itasababisha mass haisteria,
Hilo lengo lilishajadiliwa na UNESCO akiwa kama kibaraka wa hizo Nadharia njama ya kwamba mambo yote na historia ya Dunia ya ukweli Pamoja na makumbusho na kumbukumbu zote zenye utata zilizojengwa na Annunak ziwe nyara na Watu wasiambiwe ukweli kamwe waendelee kua watumwa wa fikra na kuendeshwa Kwa manufaa ya Watu wachache,
Leo angalia media,majarida,vitabu na machapisho mbali mbali yanavyopotosha juu ya sites zote zenye utata mfano ni kupotosha ya kwamba pyramids za Giza zimejengwa na Mapharao na ni Makaburi ya mumiani,
Tukija wauliza kama makaburi tu yamedumu mpaka Leo tunaomba mtuoneshe majengo waliyoishi wanabaki na kiwewe
Yaani Kwa Akili timamu mtu ajenge makaburi makubwa Kuliko nyumba anayoishi Ina make sense?
Haya tukiuliza na Zile Pyramids za Mexico ni Makaburi ya Pharaohs Gani mtajibu Nini?
Mnaopinga either ni lack of information na knowledge mkijificha Kwenye kichaka Cha utata na Udini nje ya hapo hamna jipya Wala hoja zenu hazina nguvu zaidi ya kupinga bila fact

Alamsiki!
Naomba jibu langu.
Kama Annuanak waliwafanyia chroning binadamu. Nani aliwafanyia chroning wanyama?. Maana nao walikuwa giant hapo zamani na Sasa nao wamepungua ukubwa.
Mfano tembo. Ni Nani aliwafanyia chroning???
Screenshot_20220510-081126.jpg
 
Umesema Annunaki ni wakongwe kuliko umri wa Mungu wa Ibrahim .

Upi umri wa Mungu wa Ibrahim kulinganisha na annunaki?

Annunaki asili Yao ipi ,wapi yaani imekuwaje wakawa wao(wameumbwa au wametokea tu ?)
 
hakuna hakika Juu ya Hilo mkuu maana mara ya mwisho habari zao kurekodiwa ni kule Mesoamerica hasa kwenye Maandiko ya wamaya na Aztec nk
Ukisoma baadhi ya vyanzo inadai Annunaki waliokua duniani walitofautiana wao Kwa wao sababu kubwa Ilikua ni jinsi ya kuwahandle binadamu Kuna baadhi Yao walitaka binadamu aendelee kua mtumwa wao Kuna wengine walidai binadamu anastahili kupewa ujuzi na maarifa makubwa afanane na wao,tofauti Ile ilikuja kuzaa vita kubwa kati ya pande mbili maana Enki aliyewafanya binadamu alitaka wakubalike na watambuliwe Katika jamii ya wanibiru ila ENLIL alikataa akidai lengo la binadamu ilikua ni kuwa vijakazi Katika Migodi Yao na baada ya mission kukamilika wanastahili kuondoshwa na kutoweshwa Katika tofauti zao wakakubaliana kuwaacha huru ila Kwa sharti wasipewe access ya advanced technology Bali wapate elimu ya ujuzi wa kawaida kama
Engineering,Music,uchimbaji madini mbali mbali,kufua vyuma nk yaani Ile nyepesi tu na baada ya hapo waliondoka kurudi Kwao Nibiru planet na hawajawahi rejea Tena baada ya kukaa duniani Kwa Miaka maelfu nyingi sana,huo ndio ukawa mwisho wa accient civilization za kale kama Sumerians, Assyrian, Babylon, Egyptian, Kush, Aztec, Maya, Peru, Indus valley kuanguka na binadamu Kuanza survive Katika Hali ya kawaida huku akibakia na dhana ya Mungu,Miungu kutoka juu akitumainia ipo siku watarudi kuwakomboa kwa shida zao,

Mfano kule mexico kwenye jamii ya Aztec na Maya walitoa kafara za binadamu Ili kutuma maombi Kwa Miungu hiyo irudi itatue shida zao mbali mbali
Angalia movie ya Apocalypto ya Mel Gibson utapata idea kidogo kwanini wale watu wanatoa kafara kwa Miungu jua au star gods ambao ndio hao ANNUNAKI!
ENLIL Alizaliw na ENKI km mtoto mkubwa wa kwanza wake na akapewa madaraka amabayo alifanya kinyume na babae, so babake akakasirika ule uamuzi alo fnya !! ENLIL akamuasi ENKI!baba yake! kwa muktadh huo ENKI ni=Mungu. ENLIL =shetani!

Yesu ana jina lake ila nimeshau!
 
ENLIL Alizaliw na ENKI km mtoto mkubwa wa kwanza wake na akapewa madaraka amabayo alifanya kinyume na babae, so babake akakasirika ule uamuzi alo fnya !! ENLIL akamuasi ENKI!baba yake! kwa muktadh huo ENKI ni=Mungu. ENLIL =shetani!

Yesu ana jina lake ila nimeshau!
Daah dunia wacha iende tu
 
Kwa anayetaka pia kujifunza kuhusu siri ya ujenzi wa Pyramids aangalie hii dicumentary hapa chini.Kuna maswali mengi sana mchambuzi anauliza,ila mwishoni utagundua Pyramid hazikujengwa na Egyptians kama Egyptology wanavyotuaminisha kwamba zilijengwa kwa kukata mawe kwa kugonga na kipande cha chuma kwa jiwe.
link hii hapa
 
ENLIL Alizaliw na ENKI km mtoto mkubwa wa kwanza wake na akapewa madaraka amabayo alifanya kinyume na babae, so babake akakasirika ule uamuzi alo fnya !! ENLIL akamuasi ENKI!baba yake! kwa muktadh huo

James Cameron [emoji3]
 
Mesopotamia waliwaita ANUNNAKI,huko Mesoamerica waliwaita Kwa majina mbali mbali
Ukienda Kwa Israelites waliwaita Nephilims/Watchers/Angeles
Nipe tofauti ya Mesopotamia ya kale na Israel (israelites-km ulivoiita)......wana wa ANAKI (kibiblia)wanatofautina vipi na ANNUNAKI!
 
Mwanzo binadamu hakupewa maarifa Juu ya lengo lake,alikua akitumika kuchimba Dhahabu akidhani ni kazi ya kawaida tu huku akiendelea na Maisha ya kawaida, walifanya biashara,ufugaji,kilimo,burudani mbali mbali na kuzaliana pia,
Walijenga vijiji na miji mikubwa iliyokua na facilities zote
Mathalani umewahi sikia ngano za uzuri wa miji ya Babylon,Eridu,Nippur, Nineveh nk ilikua ni Miji mikubwa Sana Katika accient world iliyokua na Kila kitu kama mabustani ya kumwagilia na mapumziko,majumba ya michezo mbalimbali,club za Pombe na majumba ya ngono na kamari hayo yote yametajwa kama vitu vya kawaida katika Dunia ya kale na Annunaki waliishi miongoni mwa binadamu kawaida tu huko wakijulikana kama gods/Lord's
Mfano wa viongozi hao ni Enki na Enlil pia walikua na ndugu Zao Moja kati ya bint wa annaki aliitwa Inana/Ishtar huyu Ndie aliyewafundisha wanawake style za kungonoka alikua ni Moja ya bint za ANU aliyependa starehe Sana Mpaka akajengewa Moja ya bustani nzuri ya Babylon zinazotiririsha
Maji Kwa Hali ya kustaajabisha kama sehemu ya ufahari na kuvinjari tu Kwa Malkia Huyo wa Mbinguni
Mpka Leo Hilo jengo limekua ni Moja ya maajabu ya Dunia ya kale,

Kwanini Annunaki ENKI na ENLIL waliokua viongozi wa mission duniani waliwaficha wanadamu waliowaumba juu ya ukweli huo huko wakiwaambia Mungu mkuu wa Mbinguni Ndie aliyewaumba?

Mosi ni kutaka binadamu asijue Asili yake maana Mwanzoni wakati ANNUNAK wanashuka duniani Kwa mara ya kwanza na kuanzisha migodi Yao ya Dhahabu,waliwatumia Igigi Aliens Moja ya jamii za Annunaki Kwenye machimbo Yao,kutokana na brutality za kina ENLIL ambao walikua viongozi wao walikuja goma kufanyishwa kazi na ikazaliwa vita kubwa sana ambayo katika maandiko ya kale ya Sumerian ndio vita ya kwanza Duniani iliyopata piganwa na ilileta madhara Sana na kuathili mission Yao,maana inahusishwa na nuclear weapons ENLIL akiwa kama master of mission aliendesha mission Kali ya kuwapoteza Igigi katika uso wa Dunia,
Inatajwa Enlil alitumia Nyundo kubwa yenye nguvu maradufu kuwasambalatisha adui zake
ANUNNAK ambao ni advanced katika science and technology walitumia siraha Bora Sana kupoteza maadui Ili waje na mpango mpya ambao utawawezesha kuendeleza mission Yao Ndipo Enki akaja na Wazo la kumfanya binadamu akitumia sample ya kiumbe aitwaye Enkidu ambaye alikua ni moja ya primitive ENKI alifanikiwa kumfundisha kiumbe yule ujuzi na maarifa huko alikifanyiwa majaribio na kuongezwa vinasaba Kwa kutumia Cloning technology ,
Pia kupitia kiumbe yule Enki akamtengeneza kiumbe Mwingine kama yule akitumia maabara za Kisasa na sayansi ya Hali juu Kwa kufanya majaribio mengi Sana mpaka akakamilika lengo ni kumpata kiumbe mwenye ujuzi na Kasi kubwa katika ufanyaji kazi migodini na mwishowe lengo linatimia Adamu wa kwanza anaumbwa na katika majaribio anawekwa katika bustani ya Eden iliyokua pembezoni mwa mji wa Eridu ambao ENKI anaishi,bustani hiyo iliyokua katikati ya mto Euphrates na Tigris ilitumika na Annunaki kama maabara na sehemu ya majaribio ya mbegu za Kisasa za mimea na wanyama Ili kukidhi haja ya chakula pindi binadamu atakapoishi na kufanya kazi katika machimbo ya dhahabu
(Bustani Eden/Aden ilikua sehemu ya kwanza binadamu kupata chakula,ambapo Miungu ilimtengenezea Mwanadamu pindi atakapoanza survive)

Sasa basi Annunaki baada ya kumaliza mission Yao na kuamua kuondoka duniani waliamua kuteua kizazi Cha Adamu na kuwapa siri ya mission Yao,kumbuka Annunaki walifanya genre ya Homo sapiens wa kwanza mosi ni Ile ya kumgeuza Enkidu/Primitive na nyingine ni Ile ya Adamu/ copy ya genre ya Primitive iliyofanywa maabara

Annunaki waliona yule waliyemfanya maabara Ni bora hivyo walimpa access ya kutunza Siri na ndio Loyal bloodline of Adam ambao kizazi Chao kimetembea Kwa Enoch,Noah,,Abraham,Isack,
jackobo na hatimaye Israelites hao ndio maana Toka kale walijitanabaisha ni Wana wa Mungu na ni choosen one,wao hujiona Bora kuliko watu Wengine Toka kale na mara nyingi wamejikuta wakikngia matatani Kwa baadhi ya jamii zile nyingine ambazo hawakupewa Siri na Miungu hao waliowapa Amri na sheria za kuiendesha Dunia Mpaka majira na nyakati zitakazowafaa na wakaahidi watakuja Rudi na kuifanya Dunia iwe paradise au Heaven N' Earth
Hizo ndio Siri zilifanya wahuni wachache wanaojua secret behind kuanzishia dini Kwa maslahi Yao
Binafsi ila tukiusema ukweli mchungu Kuna vibaraka wao ambao hafahamu ukweli wanakuja na mapovu kupinga hapa na nishajionea,
Msidhani hii Dunia ipo kama mnavyoiona everything is secreto for the befit of few people kama huamini kawabane wale viongozi wenu wa Dini wanaoendaga semina huko Vatikano na Madina hakika hutajuta kusoma bandiko langu!
Habari mkuu,samahani Naomba namba yako ya simu nikupigie nikuulize baadhi ya maswali ambayo naona nikiuliza kwa maandishi nawesa nisieleweke..maswali Kama
1.baada ya annunaki kumtengeneza binadamu ilikuaje wakamuwekea kifo?
2.Umesema Eden ilikua maabara ya majaribio je mtu wa ujuzi wa mema na mabaya upoje?
3.Baada ya annunaki kuondoka je waliahidi kurudi ili binadamu aendelee kuogopa kusaliti kazi aliyopewa ya kuchimba dhahabu?
4.Kwanini binadamu waliopewa hiyo Siri ya mission ya hao annunaki ambao umesema ni kizazi Cha Abraham au pure bloodline wao hawajihusishi na kuchimba dhahabu?
5.Vipi concept ya mtume ya mtume na yesu kristo nayo Ina uhusiano na annunaki?
Nijibu tu kwa upole mkuu[emoji120][emoji120]
 
Halafu kitu kingine Ankori hebu amka basi Swala la ANNUNAK sio la kiimani aisee mbona mnakua wagumu kuelewa hakuna mtu timamu atayesema ANUNAK walikua Miungu ila nyie ndio mliechukua nadharia za Uungu kutoka kwao na kumtengeneza modern GOD ambaye mnaemwabudu na hamjawahi kumwona hauoni kati yangu na wewe Kuna utofauti hapo?
Narudia hakuna kiumbe anaitwa 'MUNGU'
Bali Hilo neno linatumika kama title tu lenye maana ya
'Master of High Chamber'
Katika accient tablets za kale za Wasumeria huyo Master of high chamber aliitwa 'ANU'
Wayahudi na Israelites walimwita
Elohim/Elojim/YHW

Soma kuelewa Ankori!
Unasema sisi hatujawahi kumuona Mungu, Wewe umewahi kuwaona hao ANNUNAK ?? na sote tumewafahamu kupitia maandishi
 
Hizo za ukifa unaenda maisha ya eternal ni fiction tu walizolaghaiwa watu wa kale na hao watchers kiufupi hakuna kitu kama hicho mtu ukifa unakua decay unatoweka kabisa udongoni yaani unakua deadly infinity,
Hizo dhana zilianzishwa na ENLIL wakati ANNUNAK wanaondoka duniani na kurudi kwao waliwaambia hivyo maana walijua wanaondoka duniani na hawatarudi Ili kuwafariji wakawapa porojo za life after death Kumbuka
Annunak walicotrol man kind na walikua na akili sana walitunga sheria walizoziita dini Ili iwe faraja Kwa watu watakaowaacha huko wakiwaahidi ipo Siku watarudi na kuwachukua waende wakaishi nao juu mbinguni
(Nephilim 12th planet ) kwenye Raha za milele na anakoishi Mungu Mkuu ambaye ndie baba wa waanak yaani ANU
Kiufupi Ile ilikua danganya toto tu ukisoma maandiko ya Sumeria yanadai race ya binadamu ilikataliwa na jamii ya wanibiru kwamba haitakiwi huko kwao sababu lengo ilikua ni kuwatumia kama vijakazi wa kuwachimbia dhahabu tu mwisho wanatoweshwa ila kutokana na kuishi nao Kwa Upendo Kwa miaka mingi baadhi ya watchers waona waache tu wasurvive wakitumainia ipo siku watarudi kuwakomboa kwenye shida zao!

Kwahiyo jombi zile story zenu za Malaika kuonekana zamani na kuishi duniani kwenye dini zenu unajua kwanini Leo hawaji Tena Kwa maelfu ya miaka?

Mlilaghaiwa Aiseee poleni Sana waamini!
Unasema walidanganya watu kuwa watakuja kurudi na kuwachukua ??

Means ANNUNAK walikua viumbe wa propaganda pia na uongo uongo, Unantafakarisha kweli maana hata hayo maandishi ya kale ambapo unadai ndipo imefichuliwa siri za chanzo cha watu/binadamu wenda ilikua ni propaganda za hao hao ANNUNAK, Maana kama waliweza kudanganya watu waliowaumba kuwa wakifa kuna life baada ya hapo, na watarudi kwajili ya kuwachukua hapo hapo wakiwa wameacha maandishi ambayo yanaelezea mambo yote haya unayoyaandika,, unatuchanganya
 
Annunaki mara Yao ya mwisho ni miaka 450 BCE waliondokea kule Mesoamerica baada ya kuibeba dhahabu ya wahindu wekundu,Wamaya, Waaztec, waperu nk
Hahahaha dhahabu 'YA' wahindu, wamaya, Waaztec, waperu ????? Hahahahahaha ?? Watu walioumbwa wakawa ndio walimiliki wa hizo dhahabu tena hahahahahaha
 
Tulia upate elimu wewe acha kuishi kwa kuabudu mavitabu yaliyoletwa na wakoloni, we unadhani wakoloni wanatupenda? akuletee wokovu wakati alitaka asiondoke!! afaidi mali zetu! angalia walivyo na chuki na mtu mweusi! Mzungu na mwarabu sio watu kabisa!
Ajabu hao hao ndo wamekuletea na habari za kuhusu ANNUNAK, Hahahahahaha
 
Habari Wana JF na jukwaa la Intelligence natumaini mpo salama na tunasurvive chini ya jua kibishi,
Nimeona nilete hii mada ngumu kidogo kuhusu Accient civilization ya kale katika Dunia yetu,pamoja na nadharia mbali mbali za kuanguka na kupotea kwake,

Natumaini wale magreat thinkers watashashare idea zao kutoka vyanzo mbali mbali na natamani mjadala uwe endelevu na wale wenye watakaoweza kuweka rejea kutoka source mbali mbali wawe huru Ili mjadala uwe mpana kidogo hivyo uvumilivu unahitajika,
Note wafia Dini hamuhitajiki humu kama kitu hujui kaa kwa kutulia upate Somo na rejea mbali mbali,

Karibu!

Dunia ya kale ilipata kupitia katika ustaarabu mkubwa sana ambao Mpaka Leo unaacha utata mkubwa pamoja na fumbo kuu,
Wanasayansi,watu wa Dini,wanafalsa na wachunguzi huru wamejikuta kwenye sintofahamu juu ya ustaarabu ule uliopotea Huku wakibaki kwenye nadharia nyingi toka Hapo zamani,

Ushahidi kutoka maandiko ya kale ya Sumeria yaliyokutwa katika tablets za Mawe na michoro mbali mbali katika jamii nyingi za kale zimewataja viumbe walioitwa 'miungu'

"Miungu" au 'gods' tafsiri yake ikiwa na maana ya walioshuka kutoka 'mbinguni' au angani na Kushuka duniani,

Nadharia ya Miungu Katika Sumeria imewataja "ANUNNAKI"
Au Wana wa Annak
ANU =mtawala wa mbinguni na baba wa waanak na KI mother goddes mtawala wa Dunia,

Maandiko ya kale ya Wasumeria katika Mesopotamia yamewataja viumbe Anunak walipata Kuja duniani Miaka 450,000 BCE iliyopita,
Mtafiti wa mambo kale Zachariah Sitchin miaka ya 70's aliweza kutafsiri baadhi ya maandiko ya kale ya Wasumeria yanayodai Annunaki walipata Kuja pre human development yaani akiwa na maana Dunia ikikaliwa spicies ya Homo Elactus pekee,

Pia maandiko ya kale ya Sumeria yanadai Annunaki walitokea Sayari ya Nibiru ambayo huizunguka mfumo wetu wa Nyota ikiwa kwenye mhimili wake Kila baada ya miaka 3,600
Na maandiko hayo ya kale yanapata kuandika Annunaki ni intelligence being wenye high advanced science and technology na walipata kuja Duniani na Spaceships kwa lengo la kuchimba Dhahabu ikiwa kama metal ya mhimu huko kwenye sayari Yao ambayo waliitumia kurecover atmosphere ya anga lao,
Note hiyo ni according to Accient writings alizotafsiri Zachariah Sitchin,wanasayansi na Watafiti wa mambo kale kama Jesus Cediel,

Swali Wana jamii intelligence Inakuaje tablets kongwe na ya kale kuliko maandiko yoyote Yale yaani Sumerian iandike mambo kama hayo?

Fumbo!

Nitaendelea na mada karibuni Kwa mjadala!

ALALU:Mtangulizi wa mwanzo wa Annunaki
Katika accient tablets anatajwa Alalu huyu alikua ni agent kutoka Sayari ya Nibiru aliyepewa jukumu la kuzunguka Sayari mbali mbali kuangalia uwezekano wa kuwepo Kwa dhahabu,Alalu alifanikiwa kuifikia Dunia yapata miaka 450,000 BCE na kufanya tafiti mbali mbali Katika accient tablets anatajwa kama 'mungu' wa ugunduzi,Alalu alipata kutua Kush na akagundua hazina kubwa ya dhahabu,ugunduzi wa machimbo ya kale ya kush unathibitisha kugundulika Kwa dhahabu Kwa mara ya kwanza Katika uso wa Dunia ukifuatiwa ule wa South Africa na Maputo Msumbiji ambako miaka ya Hivi karibuni kuligundulika machimbo ya kale sana yalichimbwa Kwa ustadi Kwa kutumia vifaa vya kisasa unaoshangaza Dunia ya Leo,

Baada ya tafiti za Alalu walifuatia Wana wa Annak ENKI na ENLIL ambao walishuka na Spaceships s kubwa Wakiongozana na moja ya jamii ya Waanunaki waitwao IGIGI ambao waliotumika kama workers kwenye Migodi yote iliyoanzishwa huku wakiongozwa na ENKI na ENLIL kama viongozi,

Maandiko ya Sumeria yanadai baadae IGIGI walichoka kufanyishwa Kazi za machimbo ya dhahabu sababu ya brutality kitu kilichopelekea vita kubwa na ya kwanza Katika uso wa Dunia ikihusisha advanced weapons kama Nuclear weapons,
Baada ya resistance ya IGIGI
ENKI alikuja na Wazo la kumfanya Kiumbe awe replaced ndipo wakawafanya Nephilims (Wanefili) Hawa walikua ni Viumbe wenye mfanano na Annunak ila wakubwa na wenye nguvu,wakitumia Hybrid Nephilims walishindwa zaliana hivyo kuwapa mzigo ENKI kuwazalisha Kwa wingi kulingana na mahitaji na Kasi ya Kazi Katika Migodi maana walishindwa kuendana na Kasi sababu ya ukubwa na uzito wa miili Yao,

WAZO LA KUMFANYA BINADAMU,
Annunak Chronicles inaelezea mwanzo Dunia ilikaliwa na Viumbe waitwao Enkidu Katika Epic of Girgamesh wanamtaja Kiumbe Mtu Enkidu ambaye alikua spicies ya Homo Elactus walioishi duniani wakiwa hawana humanity waliishi pamoja na wanyama wa mwituni kama hayawani wengine,.
Enki alifikiria ni jinsi Gani atawafanya wale Enkidu wawe intelligence na akaja na Wazo la kuwaongezea vinasaba milini mwao Kwa kufanya DNA testing na walifanikiwa kufanya genre ya Homo sapiens wa kwanza,
Pia Maandiko ya Sumeria yanadai Annunaki walifanya human manipulation na cloning project na kumtengeneza mtu wa kwanza
ADAPA (Adamu)
Wakitumia DNA zao,manii na kupandikiza Kwa Kiumbe mke aliyekuja kuzaa genre ya Homo sapiens kamili iliyokamilika
(Sumeria tablets zinaelezea teknolojia ya Human cloning,human manipulation na sayansi nyinginezo kukamilisha Hilo)

Kwanini wamuumbe mtu Kwa mfano wao?
Ukisoma kitabu Cha Genesis kinadai Mungu alisema na tumfanye mtu Kwa mfano wetu
(Wale wa nadhari za Abrahamic Religion wajiulize ilikuaje Mungu aseme na tumfanye mtu Kwa mfano wetu)
Hiyo wetu inawakilisha uwingi ikiwa na maana ya "Gods"
(Walioshuka kutoka juu mbinguni na kuja Duniani)

NADHARIA ZA MUNGU NA MIUNGU/ KUUMBWA KWA BINADAMU WA KWANZA NA LOYAL BLOODLINE OF ADAM,

Mathalani umewahi sikia Nadharia kuhusu MUNGU au inawezekana ni mmoja unayeabudu nadharia hii ukiamini ni Supernatural power iliyoumba ulimwengu na vilivyomo,na nguvu hiyo Ipo ndani ya kiumbe aliyeketi kwenye kiti Cha enzi Cha Mbinguni na ni Mzee wa siku mwenye utukufu mkubwa akiwa kazunguka na wazee 24 wenye uhai,huko akihukumu Kwa haki jamii ya viumbe mbali mbali waliopewa majina ya Malaika,Maserafi,wanadamu nk

Nadharia hii ilitawala katika ulimwengu wa kale na wakisasa
Huko ikiwa na tofauti mbali mbali,

Mosi ni Ile Mungu hapo zamani alishuka Moja Kwa Moja mpaka duniani akiounga upepo katika bustan ya Eden Pahali anapoishi binadamu wa kwanza kuumbwa Adamu,
Ukisoma maandiko ya kitabu Cha Mwanzo kinadai Mungu alishuka wakati wa alasiri bustanini kuongea na kiumbe wake
(Code nitaelezea hapa Kwa kina)

Pia hapo kale Wana wa Mungu Walishuka mpaka duniani na kukutana na watu wa kale na kuishi nao maisha ya kawaida
(Refer Watchers/Angels)
Hiyo ilikua swala la kawaida tu bila shaka,


Pili:Nadharia za kisasa
Hapa tunaona katika zama Fulani miungu walikndoka duniani ni kama waliitelekezwa vile,sababu ya kufanya vile hatujui ila inakuja ibuka nadharia ya watu wanaojita Mitume na Manabii ya hapo kale wakijifanya ni maajent wa Mungu na wasemaji wake Kwa watu katika mambo Fulani Fulani,
Je ilikuaje yule Mungu na wale Malaika wake wasije Tena mpaka Leo hii toka zama zile na hata wakija wanafikia Kwa jamii Fulani Tena watu wa blodline Moja?
(Fumbo)

Leo ninaenda kukupa majibu ya hilo fumbo hapa hapa!


Tuendeleee

Maandiko ya Biblia kwa asilimia 99% hasa agano la kale limecopy Maandiko ya Sumeria ambayo ni makongwe Sana Kuliko maandiko yoyote yaliyowahi rekodiwa hapa Duniani,
Hili linaungwa mkono na jamii nzima ya Leo maana sumerian tablets ndio msingi wa ustaarabu wote wa Mwanadamu katika Historia ya Dunia,
Sumeria ilikua ndio sehemu ya kwanza Alphabet yenye character 600 +
Ikiiacha mbali Alphabet tuitimiayo yenye character 26 tu
Yaani ABC to Z basi
Pia Sumeria walikua na Mathematical table ya kushangaza Sana,
Wataalamu wa mambo kale Wanakiri endepo tutaweza gundua calculation na njia ya kufanya Hisabati kama wao tutapiga hatua Kubwa sana katika science and technology
Refer wanasayansi kushindwa fanya calculation za accient civilization zilizotumika katika ujenzi wa majengo kama Pyramids na site mbali mbali
(Mifano mnayo)

Sasa basi Bible ilicopy maandiko hayo sababu waliyanakiri na kucopy visa vile walikosa Information kuhusu Accient civilization hivyo kuoelekea kuunga unga visa vilivyokaa bila mpangilio maalumu yakiwa Randomly
(Wanatheolojia watanielewa)

Baada ya ugunduzi wa Sumerian tablets miaka ya 1880's na baadhi kuyatafsiri ndio tukajua zile information zote tata zimeelezewa Kwa ufasaha na kupangiliwa visa kuhusu Accient gods waliokuja kutoka Nibiru planet kutafuta dhahabu na hatimaye kumuumba Binadamu kama man power!
mjomba,utafanya wa2 waasi imani zao,hasa wenye kukosa kutafakari,v2 ivi haviwekwaji public kutokana na uwezo tofauti wa kutafakari v2 baina ye2{akili}...utapeteza wa2 mzee baba!!..ndo manake unaona kunavitabu vimefichwa kama the book of enoc....lakini kila serikali duniani huwa inafungia baadhi ya vitabu,sinema au nyimbo inazohisi vitaharibi jamii....sory 4 that bro!!
 
mjomba,utafanya wa2 waasi imani zao,hasa wenye kukosa kutafakari,v2 ivi haviwekwaji public kutokana na uwezo tofauti wa kutafakari v2 baina ye2{akili}...utapeteza wa2 mzee baba!!..ndo manake unaona kunavitabu vimefichwa kama the book of enoc....lakini kila serikali duniani huwa inafungia baadhi ya vitabu,sinema au nyimbo inazohisi vitaharibi jamii....sory 4 that bro!!
Hata chizi anatafakari pia na anajua uwepo wa Mungu mmoja
 
Back
Top Bottom