Anza hivi Kucheza kwenye draft, utasumbua sana.

Hahaaa kumbe nawewe kiwalani unakupata freshi
nakujua sana mchezo wa Draft umenikutanisha na wengi...........!!! Kiwalani kulikuwa na watu kama Kedi sasa hivi ni chizi........enzi hizo Buguruni chama.........sasa hivi Kiwalani na Chanika kuna vijana wana mauwezo balaa........Labda uwe na uwezo kama mimi Farisi ndiyo utawazeza..................!!!
 
Pale buguruni nilikua naogopa kucheza, kuna siku nilikua napita nikakuta kitoto kinawakalisha watu wazima afu mabingwa
 
Hahaa , mkuu unajikubali!!. Kungekuwa na online la kibongo ningekutafuta nikukalishe.
 
Acheni ujinga. Drafti halina formula. Mie mtu anayecheza kwa formula huwa nampenda sana, maana namvuruga mapema halafu anabaki anahaha tu.

Drafti la formula umkute mtu anayependa formula. Ila ukinikuta mimi nisiyependa formula nakuchezea mchezo wa kukatakata mistari yako yote inabaki na mapengo halafu ndani ya muda mfupi tunabaki na kete tano tano kila upande.

Hapo sasa ndo nitakuona ufundi wako ukoje.
 
Napendaga mara mojamoja kuwa pembeni tambo za hapo ni balaa.
 
Ndiyo zangu hizo,nakatakata zikibaki chache ndiyo nakomaa,sema hii ni rahisi mtu kutoa sare
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Draft kuanza ni rahisi, kumalizia ndo shida, lakini kuna wataalamu ukianza tu anakuambia huo mchezo ni droo..[emoji23]
 
Ukikata sana kama hauko makini unaweza kujikuta unafungwa super
 
Utasikiaaaa heeee mkwe huyooooo...ona mama huyu. Napiga mpaka chumbani hii..mkamateni jamani asikimbie....lete gazeti aseee,,vp tukupe kijii aaaaa huyo huyo anakujaaaa.


Hatari sana

Sent using iphone pro max
 
Mangwelele nilikuwa namwona sana manyanya akichapa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…