Anza mapema kuwafundisha watoto wasitoe siri za ndani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Sisi tunaoishi kwenye nyumba za kupanga. Kuna wanaopenda wajue umekula nini leo, na maisha yako kwa ujumla.

Kama umepanga vyumba viwili, chumba cha watoto weka double decker, sofa moja na coffee table. Hii coffee table ndiyo dining table pia.

Pembeni weka meza ya jiko la gesi na chini ya meza ndiyo ndoo za unga na mchele.

Ukimaliza kupika na kuwaandalia watoto, mbariki chakula, mkimaliza kula unawaambia kabisa watoto, ya ndani yanabaki ndani atakaeuliza mmekula nini mjibu muulize mama.
 
Hofu za kijinga hizo hivi mtoto akiulizwa umekula nini na akisema nimekula makande we inakukwaza nini? .. yaani huo muda wa kuwawahofia jirani masikini mnaupata wapi? .. huko ni kuwaandaa watoto kuwa waongo na roho mbaya .. malezi mabaya sana hayo
 
Huo utunzaji wa siri hautaishia kwenye kula tu bali utawajengea watoto tabia ya kutunza siri za ndani hata watakapokuwa wakubwa. Hivi mtoto akisema 'muulize mama' atakuwa amesema uongo gani? Roho mbaya hapo iko wapi? Au ndio wale pingapinga kila kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja, ndio ile ya wakati wa kula mtoto anaambiwa waambie wenzako wakacheze. Uchoyo tu na ubinafsi.
Hofu za kijinga hizo hivi mtoto akiulizwa umekula nini na akisema nimekula makande we inakukwaza nini? .. yaani huo muda wa kuwawahofia jirani masikini mnaupata wapi? .. huko ni kuwaandaa watoto kuwa waongo na roho mbaya .. malezi mabaya sana hayo
 
Hofu za kijinga hizo hivi mtoto akiulizwa umekula nini na akisema nimekula makande we inakukwaza nini? .. yaani huo muda wa kuwawahofia jirani masikini mnaupata wapi? .. huko ni kuwaandaa watoto kuwa waongo na roho mbaya .. malezi mabaya sana hayo
Una watoto kalagabaho Katika ulimwengu huu kuna mambo mengi Why MTU mzima atake kujua WANAO Leo wamekula nn........ au mtoto wa jirani yako kuuliza watoto wako wamekula nn unajua Iowa watoto inauma kiasi gani ukisikia kwenu kila siku chakula kile kile huku marafiki zako kila siku wanabadilisha milo (watoto kwa watoto wakiulizana).....kuna mawili hapa inawezekana hujamwelewa VZR mtoa au hujakulia maisha ya nyumba za kupanga au life la social economic differences
 
Khantwe,
Wakianza kutunza siri hivi wanaweza kukuepusha na mabalaa mengi. Hata ukiachishwa kazi ukawa nyumbani wanaweza kusikia maongezi yenu watu wazima lakini nje wasijue yanayoendelea.
 
Umewahi kuishi kwenye maisha ya kupanga na ukiwa na mtoto?
Umeshawahi kukutana na hadha wa wapangaji ambao hawajali maswali ya msosi ya watoto wao? Yan mzazi anajali vipindi vya uhondo, na leo tena hapiki chakula na kukwambia ka
Naunga mkono hoja, ndio ile ya wakati wa kula mtoto anaambiwa waambie wenzako wakacheze. Uchoyo tu na ubinafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umewahi kuishi kwenye maisha ya kupanga na ukiwa na mtoto?
Umeshawahi kukutana na hadha wa wapangaji ambao hawajali maswali ya msosi ya watoto wao? Yan mzazi anajali vipindi vya uhondo, na leo tena hapiki chakula na kukwambia ka

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna bwana mmoja alipata matatizo kazini na kuwekwa ndani. Mama aliwaambia watoto Baba yenu amesafiri. Majirani walisikia tetesi wakaanza kuuliza watoto, watoto walijibu Baba amesafiri. Baada ya miezi mitatu alipotoka gerezani hakukua na tafrani sana.
 
Hofu za kijinga hizo hivi mtoto akiulizwa umekula nini na akisema nimekula makande we inakukwaza nini? .. yaani huo muda wa kuwawahofia jirani masikini mnaupata wapi? .. huko ni kuwaandaa watoto kuwa waongo na roho mbaya .. malezi mabaya sana hayo
Sio kweli itakuwainakuhusu hii, watu sio wazuri wanapenda sana Uchunguza lif ya watu.
 
Mkuu umepost kitu muhim sana, now maisha si kama zaman ule urafiki na ujiran wakweli kama zamani hamna bt umebaki wakinafiki tu.....
mtu atajiulizisha kwa watoto ili apate chakukusema bt ukiwafunza siri watoto unaandaa familia bora itakayokusitiri na aibu hata pale unapokwama
 
Hofu za kijinga hizo hivi mtoto akiulizwa umekula nini na akisema nimekula makande we inakukwaza nini? .. yaani huo muda wa kuwawahofia jirani masikini mnaupata wapi? .. huko ni kuwaandaa watoto kuwa waongo na roho mbaya .. malezi mabaya sana hayo
kuna vitu vi 2

1. una ujuaji ulio pitiliza

2. hujui/hujui maisha ya uswahilini na tabia za hovyo za sisi wabongo.

huwa haiishii kwenye kuuliza mmekula nini tu, huenda hadi "baba yako na mama yako wanapigana ndani'. nasikia wanasemaga wewe/flani sio mtoto wa baba yule.

kifupi wanaichimba familia kila idara, sidhani kama kuna mtu yuko tayari kuanikwa maisha yake ya ndani kuanzia kula,kulala, ugomvi, mahusiano kwa kusema siwahofii majirani ujinga mtupu
 
kwani kuna tatizo mtu kujiproud na alichokianya? haina haja ya kutengeneza Inferior children katika jamii
 
Back
Top Bottom