App za mikopo kama YakoMkopo, PesaSasa kupotea Play Store – hii ni hatua sahihi?

App za mikopo kama YakoMkopo, PesaSasa kupotea Play Store – hii ni hatua sahihi?

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
5,473
Reaction score
757
Wakuu,
Nimegundua jambo la kushangaza – baadhi ya app za mikopo kama YakoMkopo na PesaSasa hazionekani tena kwenye Google Play Store. Uki-search zinaonyesha “This app isn’t available.”

Swali ni:
Je, hii ni hatua ya makusudi dhidi ya hizi app? Kama ni kweli zinafanya udhalilishaji, riba kubwa au unyanyasaji kwa wateja, basi hii ni hatua nzuri sana kwa ulinzi wa watumiaji. Lakini sasa kuna upande mwingine muhimu zaidi:

Vipi kuhusu watu ambao tayari walishachukua mikopo?
•Mikopo mingi ilichukuliwa kupitia app hizo
•Malipo yalikuwa yanafanyika ndani ya app husika
•Sasa app haipo – utalipaje?
•Au apps hizi zimefungiwa kwa muda tu na zitarudi?

Na pia kuna issue kubwa: Watu wengi wanaendelea kupokea simu na SMS za vitisho hata kama app yenyewe haipo tena.
Je:
•Ni sahihi kuendelea kudai deni wakati mfumo wao haupo rasmi?
•Malipo yafanyike wapi ili mtu awe salama kisheria?
•Au kuna hatari ya kulipa kwa "agent" asiye rasmi na ukapoteza pesa?

Mtazamo binafsi:
Kama kweli hizi app zimeondolewa kutokana na ukiukwaji wa sheria au sera, basi mamlaka zinapaswa kutoa mwongozo wazi:
•Nani ana dalka ya kukusanya deni
•Njia rasmi ya kulipa
•Na ulinzi wa mtumiaji dhidi ya vitisho

Kwa sasa, inaonekana kuna mkanganyiko mkubwa kwa wakopaji.
Wadau, mwenye uelewa zaidi atujuze:
👉 Hizi app zimefungiwa kabisa au ni kwa muda?
👉 Na walio na madeni wafanye nini ili kuepuka kutapelewa zaidi?
1000389685.jpg
ka matatizo ya kisheria?
 
Ukiingia ktk wavuti wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) utaona kuwa hizo app ulizotaja na nyingine kadhaa, jumla zipo 115, zimeorodheshwa kama app ambazo hazijaidhinishwa na BOT kutoa mikopo mitandaoni.
Hivyo inaweza kuwa zimekuwa disabled/Kufutwa na BOT ili kulinda raia dhidi ya utapeli.
Kama BOT wamefanya hivyo litakuwa ni Jambo jema na nawapongeza. Kama nchi ni lazima tujifunze kuishi ki halali badala ya kuwaumiza watu kitapeli Kwa sababu ya umasikini wao.
 
Kama Apps hizo zimekuwa disabled kwangu ni jambo jema maana badala ya kunitapeli kwa riba zao kali na muda mfupi sana wa marejesho nakuwa nimewapiga wao kwa kutofanya rejesho la tumikopo twao.
Sitishiki kwa sms zao za vitisho
 
Wakuu,
Nimegundua jambo la kushangaza – baadhi ya app za mikopo kama YakoMkopo na PesaSasa hazionekani tena kwenye Google Play Store. Uki-search zinaonyesha “This app isn’t available.”

Swali ni:
Je, hii ni hatua ya makusudi dhidi ya hizi app? Kama ni kweli zinafanya udhalilishaji, riba kubwa au unyanyasaji kwa wateja, basi hii ni hatua nzuri sana kwa ulinzi wa watumiaji. Lakini sasa kuna upande mwingine muhimu zaidi:

Vipi kuhusu watu ambao tayari walishachukua mikopo?
•Mikopo mingi ilichukuliwa kupitia app hizo
•Malipo yalikuwa yanafanyika ndani ya app husika
•Sasa app haipo – utalipaje?
•Au apps hizi zimefungiwa kwa muda tu na zitarudi?

Na pia kuna issue kubwa: Watu wengi wanaendelea kupokea simu na SMS za vitisho hata kama app yenyewe haipo tena.
Je:
•Ni sahihi kuendelea kudai deni wakati mfumo wao haupo rasmi?
•Malipo yafanyike wapi ili mtu awe salama kisheria?
•Au kuna hatari ya kulipa kwa "agent" asiye rasmi na ukapoteza pesa?

Mtazamo binafsi:
Kama kweli hizi app zimeondolewa kutokana na ukiukwaji wa sheria au sera, basi mamlaka zinapaswa kutoa mwongozo wazi:
•Nani ana dalka ya kukusanya deni
•Njia rasmi ya kulipa
•Na ulinzi wa mtumiaji dhidi ya vitisho

Kwa sasa, inaonekana kuna mkanganyiko mkubwa kwa wakopaji.
Wadau, mwenye uelewa zaidi atujuze:
👉 Hizi app zimefungiwa kabisa au ni kwa muda?
👉 Na walio na madeni wafanye nini ili kuepuka kutapelewa zaidi?View attachment 3595691ka matatizo ya kisheria?
hata hivyo nao wamepigwa na kulizwa sana tu na watu wasiojali udhalilishaji wao 🐒
 
Kwahiyo wanaodaiwa inakuwaje? Maana kama App haipo sasa watalipaje au wawatumie hao wanaowasumbua kwenye simu? Ambapo naona si sawa
 
Nami ni mhanga alinipa 248000 baada ya siku sita nilipe 400k wananidhalilisha mno kwa ndugu simu hazikomi wanapiga mfululizo napandwa na pressure jamani na Sina hela ya kuwalipa kwa sasa
 

Attachments

  • IMG_20260607_165104 (2).jpg
    IMG_20260607_165104 (2).jpg
    949.1 KB · Views: 32
Back
Top Bottom