App zinazotoa mikopo mitandaoni zina riba kubwa sana, ukichelewa rejesho wanatuma SMS kwa namba zote ulizowasiliana nazo

Kwanini ulikopa mikopo kichefuchefu? Bora ungehazima kwa mtu wako wa karibu kuliko kufedheheshwa!
 

Hawa wanachofanya ni udhalilishaji
 
Wakati unakopa, ulikubaliana na ‘Terms and Comditions’ zao?
Mkuu ushayasikia matangazo yao?

Kwanza hayo matangazo ni kero maana yamejazwa kwenye ads za kila app, hata kama hutaki, wao wanainterrupt bila hiyari yako.

Pia masharti mepesi tu, nikitambulisho cha taifa account ya kurushiwa hela na namba ya mdhamini kwisha.

Marejesho na riba vimegubikwa na utapeli wa kufa mtu.

Kuna wakati nilitest zali kama 5k ili nione ipoipoje.

Ebanaee, baada ya kuombana utambulisho wa namba pamoja na account ya AT, viliingizwa ghafla kwa makato ya ajabu!
Toka 50000 niliyoomba nikapewa kitu kama 18000 na kutakiwa kullipa hiyo fifty na riba juu.

Kwanza nikacheka sana.
Mpaka leo walishachoka kunifuatilia.
 
Naomba kujua kama kuna aliyewahi kupata mkopo kupitia Pesa X.

Naona kama wanakusanya taarifa zetu, wanapoomba vitambulisho, namba za Mawasiliano halafu mwisho wa siku hupati mkopo.

Mamlaka zinataarifa na hizo app!?
View attachment 2874286
Hawa nili kopa waka nipa 80k wali nitafuata waka choka wao ..hamna sehemu wata kupeleka wala hawana cha kukufanya

Afu mna lalamika wana tafuta ndugu wakati mme waweka kama wadhamini ..mimi wadhamini nili weka no. Zangu zingine nilkua nawaona tu wanavyo nitumia mdhamini mimi sms za biti
 
Ila kama inasaidia kama wahitaji pesa ya chap chap
Tukumbuke ukikopa DAWA NI KULIPA TU!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…