Apple icon na dhana inayoleta maswali

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,891
Kuna mambo ambayo yanatokea humu duniani ambayo yanamfanya mtu yoyote yule ajiulize maswali mengi bila kupata majibu,kuna zile habari za vyama vya siri ambazo leo zinaonekana kama ngano kwa baadhi ya watu na kwa wengine zikiwa kama ni mambo ambayo yana uhalisia wake

Nimekuwa nikijiuliza sana kuhusu hii logo ya bidhaa zinazokwenda kwa jina la Apple,ni kwanini hiyo logo au icon inaonekana imeng'atwa?

Yaani linaonekana tunda hilo la Apple limeng'atwa kipande,kwanini iko hivyo?

Kuna nadharia nyingi sana kuhusiana na hili lakini ile ambayo inaonekana kupata nguvu ni ile ya tunda hilo kuwakilisha tunda lililoliwa pale Eden na Adam na Hawa kuashiria dhambi kuingia duniani,hili linaonekana kupata nguvu kwasababu ya mazingira yenyewe ya logo hiyo

Wenye kukubaliana na hii ya Eden wanaendelea kusema kuwa hili linawakilisha wenye bidhaa hizi kukubaliana na dhana ya shetani kutaka kumuokoa mwanadamu na 'udikteta" wa Mungu na kumpa uhuru hivyo wanaendeleza mapambano ya kumuondoa binadamu kutoka kwenye huo udikteta na ndio maana wanakubaliana na shetani

Hebu tazama hizi picha hapa chini ......



Hizo ndio logo za hawa jamaa,kama kuna mtu ambae ana maelezo ya kwanini ziko hivyo basi sio vibaya akatueleza hapa nasi tukaelewa maana kuna watu kama hawa hawa wanaendelea na dhana kama hizi;


Hebu tujaribu kuangalia na hili ili tuweze kupata majibu angalau kidogo ambayo yataweza kuturidhisha .....!!
 
interesting........

ishu za Freemasons na Illuminati ziko so confusing
sometimes hujui kipi cha kweli kipi uongo

mmara utasikia namba 6 ndo ya iluminati
mara namba 7 mara namba 9 mradi hujui ipi kweli au yote uzushi
 
interesting........

ishu za Freemasons na Illuminati ziko so confusing
sometimes hujui kipi cha kweli kipi uongo

mmara utasikia namba 6 ndo ya iluminati
mara namba 7 mara namba 9 mradi hujui ipi kweli au yote uzushi

Mkuu,

Haya mambo watu wanadai ni ya kufikirika lakini yana maswali mengi sana kuliko majibu na watu wameamua tu kuishia kusema ni hadithi kwasababu hawana majibu

Ni kweli haya mambo yanachanganya lakini yanashangaza sana

Sasa mfano hilo tunda,unaweza kujiuliza tu ni kwanini liwe limeng'atwa?

Kuhusiana na namba hilo nalo ni jambo lingine linaloshtua sana na kushangaza pia!
 
It's just a trademark,,, biashara hiyo mkuu...being different in business makes you unique...Hizo dhana nyingine ni watu wanatunga tu baada ya kushiba .

Mkuu yaani hivyo tu?
 
Mkuu yaani hivyo tu?

Masonic idea ni hila tu za kusumbua ubongo wa watu, mambo km haya uthibitishaji wake ni mgumu na nadhani kwa sababu hakuna mambo km hayo...fanya kazi kwa bidii, push yourself up to the limit then baada ya kupata mafanikio kiasi..kisha utasiki "He is a masonic believer" na jina lako la #Uledi litaogopwa kwamba la ki-freemason.
 
Eiyer ,
Kuna thread moja alishawahi kuchangia Kiranga aliandika kitu tofauti kidogo na hicho, nadhani anaweza akaja na kuchangia tena.
 
Last edited by a moderator:

Nafahamu kuna watu wavivu wa kufikiri ambao wanaogopa kufikiri vingine na mtu akifanikiwa tu wanamhusisha na Mason,lakini hii haina maana kuwa Mason hawapo kweli

Kusema tu "ishu za mason ni za kufikirika" unakuwa hujatendea haki yote haya na mengine ambayo yanathibitisha uwepo wa hawa watu
 
Kuna thread moja alishawahi kuchangia Kiranga aliandika kitu tofauti kidogo na hicho, nadhani anaweza akaja na kuchangia tena.

Nimeyasoma maelezo ya Kiranga na yanatoa mwanga angalau kwa kiasi fulani ...

Kwa maana hiyo,kampuni ya Apple ilikuwa dedicated kwa mashoga au?
 
Last edited by a moderator:

Kaka nisikupe shida, hayo maoni ni yangu na ndio mtazamo wangu.,hivyo daima nitakua hivyo and there is nothing you can do persuade me believe in what you and your fellow friends believe...I say there is no such a thing, It's just a myth like any other.
 
Sidhani kama ni sahihi karibu kila kitu chenye mafanikio makubwa kuhusishwa na imani za ki-masonic. Apple wamejaribu kuleta bidhaa zenye muonekano tofauti na wengine ndo maana wanakuwa na mafanikio makubwa. Logo ya apple ni njia ya kuwa unique kama wengine wanavyofanya na hata wangeweka logo ya aina nyingine ungeuliza maswali kama haya.
 
Lakini Kabla Ya kuanzisha kampuni Steve jobs alikuwa anakula sana apples pia alikuwa analima kabisa Na ikafikia muda alikuwa Hali Chochote zaidi Ya Apple me nikahisi aliita Apple Na kuweka logo Ya Apple coz mwili wake wote ulikuwa ni Apple Na akili aliweza kuitumia vizur coz Ya Apple tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…