Logo ya kwanza ya Apple ilikuwa designed mwaka 1976 na mtu aliyeitwa Ronald Wayne, ambaye wakati mwingine anafahamika kama mwanzilishi wa tatu wa Apple. Logo hiyo ya kwanza ilikuwa na picha ya Isaac Newton akiwa amekaa chini ya mti huku tunda la Apple likiwa mtini juu ya kichwa cha Isaac Newton.
Logo ya pili ilikuwa designed mwaka 1977 na designer aliyefahamika kwa jina la Rob Janoff. Kwa mujibu wake (Rob Janoff) alisema kuwa idea ya kuweka logo yenye apple lililong'atwa ni kwa sababu ya kulitofautisha na matunda mengine ambayo yanafanana na apple, for example: cherry fruits and others. Na hilo linaweza thibitishwa kwa 'size' ya sehemu iliyong'atwa kwenye apple.
Hiyo ni nadharia ya kwanza, wakati nadharia ya pili kuhusu icon ya apple ni kwamba mnamo mwaka 1954 mmojawapo ya wataalamu wa kompyuta aliyefahamika kwa jina la Alan Turing alifariki dunia huku pembeni ya kitanda chake kukiwa na apple lililong'atwa. Hali iliyopelekea watu kuhisin aliwekewa sumu kwenye apple. Turing alikuwa 'gwiji la kompyuta' kwani alikuwa vizuri sana kwenye coding na pia ana mchango mkubwa sana katika maendeleo ya teknolojia ya kompyuta, hivyo kitendo cha Rob Janoff kuweka alama ya apple iliyong'atwa ni kama kumuenzi Janoff aliyefariki huku pembeni ya kitanda chake kukiwa na Apple lililong'atwa.
Nadharia ya mwisho inayofahamika kuhusu logo ya apple ni hiyo ambayo mtoa mada amekuja nayo, kuhusu Apple ambalo kipande chake kiling'atwa na Hawa kwenye bustani ya Eden.
Sina jibu kamili lakini kupitia nadharia tatu nilizoorodhesha hapo juu unaweza kupata mwanga wa kuchimba zaidi
'dig deep' kisha atakayepata jibu kamili asisite kuja kutupa mrejesho humu jukwaani.