Apple kwenye Airpods mpya wapewe maua yao

Apple kwenye Airpods mpya wapewe maua yao

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
70,785
Reaction score
186,690
Kwenye tasnia ya music systems na vinu huwezi kukwepa Giants wa kijapani kama akina Kenwood, Sony, Pioneer na wamarekani kama Bose, JBL, Harman Kardon na wengineo.

Mimi ni music Enthusiast toka niko ng'aa na nimeshapitia mengi ila nikiri tu sijawahi kuwa fan wa products za Apple na accessories zao ila hivi karibuni nikiwa katika harakati za kutafta earphones ikiwa nilishatumia AKG by Samsung na kuzipenda nikaanza kuzisaka bila mafanikio zote zilikuwa famba.

Katika moja na mbili nikaamua nimenye za Apple japo kishingo upande ili niweze kuzitest nkapachika na kuset bluetooth na kuweza kuwasha walkman app yangu ikiwa kwenye default settings. Baada ya nyimbo ya kwanza tu kugonga nikawa so amazed nazo.

Kile ambacho nilikuwa nakitafuta nilikipata instantly. Sikuwahi kufikiri apple wanaweza kutengeneza earphone za kinyama namna hii hasa baada ya kusikiliza nyanga zao walizotoa before na watu walikuwa wanasifia nini hasa maana sikuona maajabu.


Kwenye hizi inner ear naomba niwape maua yao hawa vijana wa Tim cook. Kwa hakika wame cook earphones zenye kiwango cha Standard Gauge kwa sasa. Bass iko tight na acoustics ziko balanced. Earpods oyeee!!! 😀
images.jpeg
 
Kwenye tasnia ya music systems na vinu huwezi kukwepa Giants wa kijapani kama akina Kenwood, Sony, Pioneer na wamarekani kama Bose, JBL, Harman Kardon na wengineongi ila nikiri tu sijawahi kuwa fan wa products za Apple na accessories zao ila hivi karibuni nikiwa katika harakati za kutafta earphones ikiwa nilishatumia AKG by Samsung na kuzipenda nikaanza kuzisaka bila mafanikio zote zilikuwa famba....
Hujatumia nura mkuu

Hizo ni uchafu kwa nura
 
Shehe bwana cook ni shoga halafu unanunua earpods zake?
Kununua halihusiani na kusapoti ushoga ,hiyo pumzi anayovuta anaitoa yeye vipi kuhusu raw materials kazibandua mwilini mwake ? wakati mwingine hizo raw materials mpaka kuwafikia waafrica wamedhulumiwa sana na wengine kuuwawa migodini.
 
Mkuu,

Hii comment usiidharau. Ila endapo hizo zitaharibika nakushauri ujaribu na earpods za Oraimo.

Tafuta original kabisa na uzi utakaofuata itakuwa ni kuzisifia kwa viwango kuliko hizo za Apple.
Oraimo nimejaribu za waya jana zinagonga vizuri sema tu sababu ni Oraimo na sikutaka za waya. Nataka za Bluetooth. Huwa wanauzaje Pods zake?
 
Back
Top Bottom