Apple yashinikizwa na China kuondoa app maarufu ya Quran

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Shirika la Apple limechukua uamuzi wa kushangaza wa kufuta apu hiyo yenye Qur'ani Tukufu kwa lugha asili ya Kiarabu na pia tarjuma kwa lugha nyinginezo pamoja na mafundisho mengine ya Kiislamu. Apu hiyo imefutwa kwenye jukwaa la App Store lenye kubeba aplikesheni zote za simu za iPhone na iPad.

Kampuni ya Apple imedai kuwa imechukua hatua ya kuondoa apu ya Quran Majeed katika bidhaa zake nchini China ili kutiii amri ya serikali ya Beijing. Hata hivyo serikali ya China haijatoa maelezo yoyote kuhusiana na madai hayo.

Apu mashuhuri ya Quran Majeed hutumiwa sana kwa ajili ya qiraa ya Qur'ani na masuala mengine yanayohusiana na Swala kama kujua upande wa kibla, nyakati za Swala, dua, maeneo ya misikiti iliyo karibu na mtumiaji na kadhalika.

Shirika la Apple limetaka Shirika la Pakistan Data Management Services ambalo ndio mtegenezaji wa apu ya Quran Majeed kuwasiliana na wasimamzii wa intaneti China ili kusuluhisha tatizo hilo.

Katika miaka ya karibuni China imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusiana na ukiukaji wa haki za Waislamu hususan jamii ya Uighur katika jimbo la Xinjiang. Hatahivyo serikali ya China imekanusha kuwalenga Waislamu na inasema inakabiliana na watu wenye misimamo mikali ya kidini.
 
Ni Ujinga na Ujuha kukaaa kujadili mambo ya Dini. Miafrika sijui fyuzi gani haikuunganishwa vizuri yaani upuuzi mtupu. Maaamuzi afanye China kuuumia aumie Mpemba wa Mchambawima.

Mbona na wao wanaingilia mambo ya huku Africa au na wao kuna fuse hazijaunganishwa
 
Yet Waislamu huwa wanaiona Marekani na nchi nyingi za Magharibi kuwa ni maadui wakuu wa Uislamu (ajabu ni kwamba pale US Waislamu hawabaguliwi yofauti na kule China).

Iko siku watelewa adui yao halisi ni nani.
Mchina anauchukia uislm live
Marekani kna misikiti
China jaribu uweke uone

Ova
 
Safi sana!

China hapendi utahira wa kitaliban nchini kwake
 
Toka Mchina arushe mwezi fake watu wakala Idd mi na hamu nae.
 
Shirika la Apple limechukua uamuzi wa kushangaza wa kufuta apu hiyo yenye Qur'ani Tukufu kwa lugha asili ya Kiarabu na pia tarjuma kwa lugha nyinginezo pamoja na mafundisho mengine ya Kiislamu. Apu hiyo imefutwa kwenye jukwaa la App Store lenye kubeba aplikesheni zote za simu za iPhone na iPad.

Kampuni ya Apple imedai kuwa imechukua hatua ya kuondoa apu ya Quran Majeed katika bidhaa zake nchini China ili kutiii amri ya serikali ya Beijing. Hata hivyo serikali ya China haijatoa maelezo yoyote kuhusiana na madai hayo.

Apu mashuhuri ya Quran Majeed hutumiwa sana kwa ajili ya qiraa ya Qur'ani na masuala mengine yanayohusiana na Swala kama kujua upande wa kibla, nyakati za Swala, dua, maeneo ya misikiti iliyo karibu na mtumiaji na kadhalika.

Shirika la Apple limetaka Shirika la Pakistan Data Management Services ambalo ndio mtegenezaji wa apu ya Quran Majeed kuwasiliana na wasimamzii wa intaneti China ili kusuluhisha tatizo hilo.

Katika miaka ya karibuni China imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusiana na ukiukaji wa haki za Waislamu hususan jamii ya Uighur katika jimbo la Xinjiang. Hatahivyo serikali ya China imekanusha kuwalenga Waislamu na inasema inakabiliana na watu wenye misimamo mikali ya kidini.
Je nikienda simu yangu yenye hiyo app toka uswaz watanifanya nini
 
Back
Top Bottom