Je ni sawa watoto wadogo (chini ya miaka 5) kutumia simu janja na mtandao?

  • Ndiyo ni Sahihi

    Votes: 12 21.1%
  • Si sahihi

    Votes: 31 54.4%
  • Inategemea, mambo yote yana uzuri na ubaya wake

    Votes: 14 24.6%

  • Total voters
    57
Ni vile tunalea watoto kwa uzungu mwingi ila mtoto sio vizur kushika simu.

Simu yangu haishikwi na mtu yeyote zaidi yangu, mtoto haruhusiwa hata kuigusa labda nimtume ailete, nikiwa karibu yake haruhusiwi kutupia jicho kwenye simu yang, ole wake aonekane ananyenyemea kuichungulia ataipatapata fresh.

Tv ni kwa ratiba maalum sio kila akijiskia yeye, ataangalia jioni akimaliza vikazi na homework muda huo anasubiri chakula.
Akishakula basi hiyo ni ticket ya kwenda kulala.
 
Haswa. Ili kuepusha lawama ni bora mtoto akae mbali kabisa na simu. Lakini ikifika umri fulani inabidi umfundishe namna ya kutumia tena kwa ratiba kali sana na ujue anapopita mtandaoni kwasababu simu ni kama kompyuta, inatumika kwenye maisha ya kila siku.

Pia ni bora wewe mzazi umfundishe matumizi bora ya simu, asije akajifunza kwa mwingine akawa kama hawa watu wazima wanaokesha mtandaoni wakifuatilia vitu visivyo na tija yeyote kwenye maisha yao.
 
Mtoto wangu ajaweza ongea kwa ufasaha ana umri miaka 3.5,lakini anajua kutaja 0ne hadi ten, anajua ABC hadi Z anajua kutaja colour 10 kwa msaada wa katuni za kufundishia.
Kupitia game ya simu anajua kuendesha gari kuingiza gia, kata kona, rivasi, forward, nk.
 
Ni vizuri ameweza kufanya hivyo. Je anatumia muda gani kwenye simu?
 
Simu , tv si nzuri kwa watoto kwa sababu hazina program mtiririko. Tv ni Mwalimu asiye na syllabus. Yaani ufundisha mtoto chochote tu bila mpangilio
 
Simu , tv si nzuri kwa watoto kwa sababu hazina program mtiririko. Tv ni Mwalimu asiye na syllabus. Yaani ufundisha mtoto chochote tu bila mpangilio
Na hii ndio shida kuu. Hivi vitu havina mpangilio utakaofanya ubongo wa mtoto kupata mambo tofauti. Ndio maana wazazi inabidi wawe makini sana kuhakikisha matumizi ya haya mambo hayazidi.
 
Naona lengo lako kubwa ilikuwa hapo chini.
 
Hii video ni mfano wa madhara ya matumizi ya simu na mitandao kwa watoto wadogo.
 
Nimefurahi kuona asilimia kubwa ya wapiga kura wanakubali si sahihi kwa watoto wadogo kutumia simu. Hii inaonyesha kuwa wazazi/walezi wengi hawajatekwa na wimbi la kufuata mkumbo wa utandawazi wenye matokeo hasi.
 
Msiache kuendelea kupiga kura kwenye poll yetu, ili tupate mawazo ya watu mbalimbali kwenye jamii kuhusu malezi ya watoto na simu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…