Apps kila kona!!

Apps kila kona!!

Guus

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2013
Posts
1,139
Reaction score
842
Wiki kadhaa niliingia CRDB na shida zangu kama mteja. Baada ya kukutana na wafanyakazi na kuwaeleza shida yangu ikawa kama mteja mkorofi. Jamaa nikashangaa wanakuwa wakali, eti "unatakiwa uwe na CRDB App". Nilipowajibu siitaki ikawa kama nimewaambia wasinihudumie, hii imenishangaza kwa kweli.

Anyway, siku nyingine nikaingia Equity Bank nifungue account, walivyomaliza kunifungulia wakaanza nao kunihubiria kuwa na Apps, (bahati nzuri hawa hawakuwa na sura ya kuifanya ulazima, walinielewa).

Imenibidi nifikiri, kwamba sasa natakiwa niwe na CRDB App, App ya Equity, Maji App (ya Wizara ya Maji), NIKONEKT ya TANESCO, DStv App/AZAM Max, MPESA/Tigo Pesa App, Air Tanzania App, etc?? Kwa lugha nyepesi ni kuwa katika hii nchi tunatakiwa tuwe na App ya kila ofisi na wala hatuwezi kuwa na App moja tukapata huduma zote??!!! Masikini nimeitazama simu yangu yenye 64GB nimechoka kabisa😳

Kuna mtu kanionesha Wechat App ya China, inafanana kabisa na WhatsApp. Amenionesha jinsi inavyopiga "miguu yote". Kwa Wachina, wakitaka hela toka kwenye akaunti yao ya benki (pasipokujali benki yake) anaihamisha kwenda Wechat, na akiwa nayo Wechat anawezaihamisha kwenda benki. Na pia wanawezakuitumia Wechat kulipia umeme, maji, usafiri, na pia wanaweza kuitumia Wechat kuchat tu, kama ilivyo WhatsApp.

Sasa kwa nini kwetu CRDB wanikabe kuwa na App yao, Equity Bank waniulizie App, MPESA waniambie kuangalia salio bila App wananikata hela zaidi ya nikiwa na App (kunilazimisha), Tigo Pesa vilevile, etc?!! Wataalamu wetu wa teke linalokujia namna gani wajameni??
 
Hayo ndiyo mambo mazuri ya kujifunza kutoka nchi za wenzetu lakini wahusika wenye mamlaka za kudeal na bunifu kama hizi wapo wapo tu.!
 
Back
Top Bottom