April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses


GT huwa unavuta?
 
Mawasiliano yamekatika mbagala, mitandao yote down jamani wanamombi muda ndo huu chonde chonde kuna dogo wangu alikuwa board maeneo ya huko....ibada zenu muhimu wanajamii. Hili ni janga kwa kweli
 
Poleni watanzania wenzangu kwa hili tukio. Kwa waliofikwa na mauti,wapumzike kwa amani na majeruhi wapate kupona.
 

Mbwana Gembe

kwanza unakubaliana na mimi kwamba huu ni uzembe? Na hiyo milipuko isingeweza kutokea kama watu wahusika wangefanya kazi yao kwa uangalifu.

Kutokana na uzembe huo, Wahusika wooote kuanzia wazili wa ulinzi, na mkuu wa majeshi tunataka kuona kikwete anawapiga chini.

Wameshindwa kazi.

La sivyo Tanzania we need A BIG LEADERSHIP CHANGE
 
Kutokana na taswira ya medani ya kisiasa, wengi wamekuwa wakisema kuwa nchi inaelekea pabaya. Jee hii ndiyo yenyewe? Yaani kuna watu wamelipua ghala ya silaha hapa dar ili pengine wafanze mambo yao? -- you know what I mean. Mkuu wa kaya yuko wapi?

Ni tukio lazima arudi kokote aliko, nadhani Arusha.
 
Mkuu Invisible mbona kama post zinajirudia rudia kwenye hii thread. What has happened? au ni macho na computer yangu????

Asante sana kwa kutujuza kwenye hili kweli JF ni kiboko wa kwanza kujua.

Bomu li-papa limeshalipuka. Lile kubwa lao?
 
Wafuatao wanatiwa kuwajibika mara moja kwa kosa la uhifadhi mbovu wa milipuko na kuhifadhi mabomu yaliyokwisha muda[expired]

1]mkuu wa majeshi
2]waziri wa ulinzi
3]naibu waziri
4]maafisa wa jeshi wanaohusika

huu ni uzembe mwingine kwa amiri jeshi mkuu.,kwani mwaka juzi ulitokea mlipuko mdogo jesihini maeneo ya gongolamboto..ambao haukuwa na madhara .,waliunda tume na wakaahidi kukagua hifadhi ya milipuko mara kwa mara.....inaonekana hawakujifunza kwa ule mlipuko mdogo wa mwaka juzi........ingekuwa bora mabomu kabla hayajaaribika wangekuwa wanayafanyia mazoezi..kuliko kuleta maafa!!

PIA TUJIFUNZE ...MAKAMBI WAKATI MWALIMU ANAYAJENGA YOTE YALIKUWA MBALI SANA NA MAKAZI HATA LUGALO ....ILIKUWA MBALI ....KAWE ILIKUWA MBALI...LEO MAKAMBI YAMEZUNGUKWA NA MAKAZI ...NI MAAFA...

LUGALO NI BARABARA..NI HATARI..ISIYO NA SIKU.....!!

NADHANI KOSA LA MAKAZI KUWA KARIBU NA MAKAMBI NI LA WATU WA JIJI NA MIPANGOO MIJI ..KWANI KAMA NILIVOSEMA ...MAKAMBI YALIPOBUNIWA YALIBUNIWA ANGALAU YAWE KILOMETA 2...KUTOKA MAKAZI YA RAIA KWA MAKAMBI YA MIJINI.....YALE MAKAMBI HATARI YA MISITUNI NDIO YAPO HADI KILOMETA 50 KUTOKA KWA RAIA..
 
Jamani kile kitengo maalum cha maafa ndo kinaamka kutoka usingizini, hawana maelezo ya tukio wanasubiri kutoka jeshini....vichekesho kweli hii nchi. Hawa jamaa wanakula gud time huku watanzania wanakufa kibudu pumbufu zao. Eti wenyewe walisikia tu walidhani radi ujinga gani huu jamani???
 
Kila siku zikisonga mbele nchi iinakumbwa na misukoko isiyo tarajiwa tuombe salama. lakini pia ikumbukwe ipitayo si ndwele ndwele ijayo.
 


Nakuunga mkono

Hawa watu lazima wajiuzulu, kama kweli Rais Kikwete anataka kuonyesha kuwa kweli yupo pale ikulu kulinda maslay ya watanzania.
 

Waziri wa ulinzi na naibu wake ni wanajeshi kitaalamu au ni kama yule daktari bingwa wa mifupa aliyekuwa waziri wa ulinzi enzi zile?
 
Jamani TUMEPIGIWA SIMU MARA TATU NA WIZARA KUEVACUATE: naondoka now sooon online wakubwa.
 
Hivi kweli hamna mwenye taarifa kamili na hili.

Janjaman ni habari gani zaidi unazotaka?


Kwa sasa hali si shwari maeneo ya Mbagala, watoto wametapakaa wanalia hovyo wakiwatafuta wazazi wao. Mtoto mmoja mwenye umri kati ya mwaka na miaka miwili ameumia shingoni na anapelekwa kituo cha polisi tayari kwa kwenda hospital. Vibaka kadhaa wamekamatwa, vitu kama TV, Radio e.tc vimeibwa toka majumbani. Kusema kweli hali si shwari
 
Nimeongea na Mdau aliye Mbagala, kuna bomu limeanguka kwenye makazi ya watu, kuna sehemu inaitwa Magengeni kama kwenye junction ya Mbagala na maji matitu, kuna watu wameumia na kupoteza maisha...

Naambiwa ni uzembe, mabomu yallikuwa yameexpire badala ya kuteguliwa jamaa wakadhalau sasa yamejilipua, juhudi zinafanyika kutafuta hata askari waliostaafu lakini wajuzi wakutegua mabomu kwenda jeshini kunusuru hali....

Namtafuta mh Nchimbi sasa hivi....ingawa hapokei simu!
 
Nimeletewa mssg na mdau mmoja toka nyumbani, ni kwamba watu wawili wamepoteza maisha na kiasi cha wananchi 100 wamepelekwa Temeke hospitali.
Inavyo onekana hali si nzuri sana, sivyo vile jeshi lilivyotarajia.

...X-paster, kwani jeshi lilitarajia nini? (wamefanya kusudi nini hawa?)


...kama 9/11 walivyomkurupusha Bush, huenda mkuu yupo kwenye 'Air force one' yetu ya Bongo, au wamemkimbiza kwenye Bunker! 'hawaaminiki' hawa, (wana-mapinduzi daima.)
 
aliyesema ni nchimbi????

Deputy Minister for Defence and Security Emmanuel Nchimbi has cautioned residents to stay away from the area and to vacate all tall buildings.

hapo utaona tatizo lipo wapi?Na mie sioni haja ya watu kujiuzuru,waendelee kuwepo tu kwa kuwa wao siyo source ya tatizo..tuwaache tu!waacheni waendelee
 

Mkuu, kwani chazo kimeshajulikana?
 
Huu ni uzembe tu wa watu wa chache

Tunataka kuona wanajiuzuru,

Selikali yetu imeshindwa hata hilo jambo dogo la kulinda silaha zake kwa uangalifu.

TANZANIA ITS TIME FOR A CHANGE IN LEADERSHIP

ndio maana marekani wanasema kuna nchi hazitakiwi kuwa na silaha laki kwa sababu hawana uwezo wa kuzihudumia wala kuzitunza.....nafikiri jeshi letu limejisahau kazi ....wanaonesha uwezo mdogo hata wa kutunza milipuko....je tungekuwa na nuclear au atomic ..si dunia ingeteketea..thats why america hawataki silaha za hatari ziendele kusambaaa....

AU ISIJEKUWA PIA TUMEUZIWA SILAHA ZINAZOKARIBIA EXPIRED DATE BILA KUJUWA ...MAANA NJAA MBAYA SANA!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…