April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

Capo Fisadi Tanil Somaiya chini ya RA walisupply defective bombs, ammunitions na vitu kadhaa vilivyoexpire kutoka nchi za East Europe early 2000s na kulipwa hela nyingi kwani walidai silaha hizo ni kutoka UK, US na ni za gharama sana.

Sasa najua ni mapema lakini uwezekano wa wao kuzilipua hili kuzima soo ni mkubwa. Tusubiri tutaona mengi.
 
Capo Fisadi Tanil Somaiya chini ya RA walisupply defective bombs, ammunitions na vitu kadhaa vilivyoexpire kutoka nchi za East Europe early 2000s na kulipwa hela nyingi kwani walidai silaha hizo ni kutoka UK, US na ni za gharama sana.

Sasa najua ni mapema lakini uwezekano wa wao kuzilipua hili kuzima soo ni mkubwa. Tusubiri tutaona mengi.


Moelex kaka yangu pray usiombee mabaya!....
 
Capo Fisadi Tanil Somaiya chini ya RA walisupply defective bombs, ammunitions na vitu kadhaa vilivyoexpire kutoka nchi za East Europe early 2000s na kulipwa hela nyingi kwani walidai silaha hizo ni kutoka UK, US na ni za gharama sana.

Sasa najua ni mapema lakini uwezekano wa wao kuzilipua hili kuzima soo ni mkubwa. Tusubiri tutaona mengi.

Hapo ndio ujue kwanini Sophia Simba, Mkuchika na sasa Lipumba kabla ya wengine wengi kufuata kuwatetea kina Tanil. Hii ni hatari sana. Yaani hawa ndio wanaoagiza magari, helikopta (mbovu) etc za jeshi letu!!!! Na sasa haya tunaambiwa na silaha!!!! Silaha!!!! Silaha!!!! Uwiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!! Jamani tunakwenda wapi? Tumetoka wapi? Mungu amrehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye mzimu wake bado upo na utaendelea kuwatafuna. Alikufa mwaka 1999, kabla ya hayo hapo juu!!!! Baba hebu agiza mzimu wako utulinde na kutuzindua Watanzania. Tusali kwa dini zetu, kwa mizimu yetu, halafu tujiangalie tuendako na tutokako
 
...X-paster, kwani jeshi lilitarajia nini? (wamefanya kusudi nini hawa?)



...kama 9/11 walivyomkurupusha Bush, huenda mkuu yupo kwenye 'Air force one' yetu ya Bongo, au wamemkimbiza kwenye Bunker! 'hawaaminiki' hawa, (wana-mapinduzi daima.)

Yaani miripuko/milipuko (!?) hisingekuwa mikubwa hivyo... ukizingatia kuwa mabomu yalipita muda wake...(kama kweli!)... Hapa tusibiri taarifa rasmi tu toka wizara ya ulinzi na usalama kabla hatujaanza kulalamika baadhi ya viongozi na wahusika wajiuzuru, I am afraid kuwa hatuna hutaratibu wa kujiwajibisha.
 
Mbaya zaidi, huko mbagara ndiko kwenye kikosi cha mizinga ya masafa ya kati na mbali (missiles) short range and long range... ndio maana hata walio mbali kidogo na tukio wanaaswa wajihadhari.
Na Tz sidhani kama kuna eneo la ku'dismantle hivi vitu.

Tuombe M'Mungu tu kusiwe na maafa zaidi.
 
Hapo ndio ujue kwanini Sophia Simba, Mkuchika na sasa Lipumba kabla ya wengine wengi kufuata kuwatetea kina Tanil. Hii ni hatari sana. Yaani hawa ndio wanaoagiza magari, helikopta (mbovu) etc za jeshi letu!!!! Na sasa haya tunaambiwa na silaha!!!! Silaha!!!! Silaha!!!! Uwiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!! Jamani tunakwenda wapi? Tumetoka wapi? Mungu amrehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye mzimu wake bado upo na utaendelea kuwatafuna. Alikufa mwaka 1999, kabla ya hayo hapo juu!!!! Baba hebu agiza mzimu wako utulinde na kutuzindua Watanzania. Tusali kwa dini zetu, kwa mizimu yetu, halafu tujiangalie tuendako na tutokako

Kaka Halisi acha kuwa mshirikina....Tudiscuss Janga..msimpe Marehemu Mwl.Julius mamlaka ambayo hakuwa nayo na wala hatokuwa nayo...Mwl.Julius nae yupo answarable mbele ya Muumba huko aliko kwa yale aliyoyafanya...!!!
 
jamani ndo maana tulipiga kelele kuhusu vipaumbele vya serikali hii.shughuli za kijamii hazipewi umuhimu( refer thread ya ukistaajabu ya musa... kuhusu kujengwa chuo cha zimamoto) Ebu tizama hii picha inatoa maelezo zaidi ya 100.

1241008818_img_4494.jpg

...askari wa Kikosi cha zimamoto wakielekea eneo la tukio(picha kwa hisani ya GP)
 
Ni nyongeza kidogo ya kile ambacho tunajua hadi hivi sasa; bila ya shaka tutajua zaidi baadaye.

Ghala la silala lalipuka; Dar yatikisika (KLHN International)
3 wafariki, 150 wajeruhiwa

Watu watatu wamethibitishwa kufa na wengine 150 kujeruhiwa katika milipuko mikubwa ya mabomu imetokea leo huko Mbagala katika ghala ya silaha ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, milipuko ambayo imesababisha wasiwasi mkubwa kwa wakazi wa Jiji la Dar na vitongoji vyake. Habari za awali zinasema kuwa milipuko hiyo siyo jambo la mazoezi bali ni ajali.

Hadi hivi sasa idadi taarifa za awali zinasema watu watatu wamekufa na wengine wengi kujeruhiwa na kukimbizwa kwenda hospitali ya Temeke na hospitali nyingine za jirani. Taarifa za awali za kijeshi zilitoa wito kwa wananchi walioko ndani ya usawa wa kilomita 25 kuhama maeneo yao na muda mfupi uliopita Naibu Waziri wa Ulinzi Bw. Emmanuel Nchimbi amerudia wito huo kupitia ITV na kuwataka watu waliokuwa kwenye majengo marefu kuteremka.

Milio na mtikiso wa mabomu hayo umesikika hadi maaeneo ya Msasani upande mwingine wa Jiji la Dar huku maofisi na maeneo ya makazi baina ya pande hizo mbili yakiwa katika hali ya wasiwasi, na watu wakipata na mshtuko.

Kufuatia mlipuko huo Polisi wametoa maelekezo kuwa mtu yeyote akiona kifaa cha chuma ambacho kimeangukia kwenye nyumba yake au eneo lake asijaribu kukihamisha bali kutoa taarifa Polisi kwani kuna mabomu mengine yamerushwa katika mlipuko huo lakini bado hayajlipuka.

Vivyo hivyo, serikali imeahidi kuwahudumia bure wale wote ambao wamejeruhiwa katika mlipuko huo na kusaidia katika kukarabati makazi ya wale ambao nyumba zao zimeharibiwa kufutia mlipuko huo mkubwa. Vyanzo mbalimbali vya habari vinadokeza kuwa wengi wa waliojeruhiwa ni pamoja na watoto wa shule ya Msingi ambayo iko jirani na eneo hilo na wakazi ambao nyumba zao zimelizunguka ghala hilo.

Juhudi za uokoaji na udhibiti wa hali zinaendelea kukiwa na ushirikiano kati ya Jeshi la Wananchi, Polisi na vyombo vingine vya usalama pamoja na vyombo binafsi vya uokoaji kama Ultimate Security.

Jiji la Dar ambalo lina wakazi karibu milioni tatu lina kituo kimoja tu cha Uokoaji na haijulikani kama Jeshi la Wananchi wa Tanzania linakituo chake cha Zimamoto kwani katika eneo la Dar na Pwani Jeshi hilo lina kambi mbalimbali, mahospitali pamoja na vikosi vingine mbalimbali.

Kwa upande wa JWTZ, kuna wanajeshi ambao wamekufa kishujaa katika jitihada za kukabiliana na mlipuko huo ili kuzuia mabomu yasidhuru jamii zaidi. Kwa hesabu yoyote leo itakuwa ni siku ya majonzi makubwa kwa Taifa kwani idadi ya waliokufa inaweza kuwa kubwa sana na ya wale waliojeruhiwa kupita hata ukadiriaji wa haraka. Madhara kwa nyumba na vitu mbalimbali inakadiriwa kupitia mabilioni. Tunaombea hilo halitakuwa hivyo vumbi zima likishatulia.

KLHN na wasomaji wake wote tunaungana na serikali kutoa wito kwa wananchi kufuata maagizo yote yanayotolewa na vyombo vya usalama wakati huu na kuhakikisha kuwa wakati kama huu kama kitu kimoja tunaweka tofauti zetu pembeni na kuhakikisha tunasaidiana. Tusimame pamoja na kuzuia uporoji wowote ambao unaweza kutokea kwenye nyumba za wale walioathirika na tusikubali watu wachache watumie tukio hili kama nafasi ya kufanya uhalifu.

Tunatoa taasisi mbalimbali ambazo zinauwezo kuanza mara moja kutoa misaada ya kiutu kusaidia wale wote walioathirika, kujeruhiwa au kupoteza vitu mbalimbali kwani tukio hili japo tutajua zaidi chanzo chake hapo baadaye ni msiba wa taifa letu na kimguse kila mmoja kama tulivyoguswa na mambo ya kipuuza ya zeutamu!

Hili ndilo tukio la kutuunganisha Watanzania wote wakati huu na mambo ya nani awajibike au asiwajibike yaje baada ya kuhakikisha kuwa hali imerudishwa katika usalama, waliojeruhiwa wanajulikana na hatua madhubuti zimechukuliwa kuhakikisha usalama wa eneo hilo. Kutoka hapo, ndipo sauti zetu zipae juu ya jinsi gani tukio hili lingeweza kuzuiliwa kwani wengine tuliandika mambo haya karibu mwaka mzima kwa sababu tunaamini Jiji la Dar limekaa katika hali ya majanga makubwa sana. Na hili yawezekana ni dokezo tu.

Tutasema zaidi baadaye.

Tunawaombea rehema wale waliopoteza maisha yao, unafuu na uponyi wale waliojeruhiwa na ujasiri na moyo wa kujitoa zaidi kwa wale ambao wanasimama kuhakikisha usalama wa Taifa letu.
 
Habari zaidi zinasema kamati maalum imeaundwa kuwanagalia majanga yaliotokea na kuanza kuhesabu walioumia na kujeruhiwa....katka hospitali ya muhimbili na temeke inasemekana watu 340 wameumia kati ya hao 100 watoto wa shule na 240 watu wazima....katika tukio la zakhem bomu moja lillolipuka liliingia nyumbani kwa mama mmoja na kumkata kiuno na marehemu amefikishwa monchwari muhimbili dk chache zilizopita............hospitali zinazotumika ni lugalo.muhimbilia.temeke amana yoyote mwenye kuhisi maumivu ama kujisikia mfadhaiko kutokana na tukio hili tunaomba waende hospitali hizo na serikali itagaramia ........alisema mh lukuvi
 
Mwananchi akipiwa kutokana na wizi wa mbagala...loh watanzania...
 
Wanataka ku diffuse hilo bomu kubwa linaweza kushambulia hadi km1...ni kubwa sana.lolote laweza tokea...
 
Jamani tuhabarisheni yanayojiri maana leo hakuna kulala jinsi tulivyo na wasi wasi
 
Jamani tuhabarisheni yanayojiri maana leo hakuna kulala jinsi tulivyo na wasi wasi

UKO MBAGALA NINI!!!!HAKUNA KULALA LEO....KUNA MAWILI BADO HAYAJALIPUKA....
MUNGU ............MAMA MMOJA AMEKATWA KIWILIWILI NA MWINGINE MAMA AMEPOTEZA MTOTO MASKINI WA MUNGU....MUNGU WAEPUSHE ZAIDI
 
Deadly blasts rock Tanzanian city
BBC News Online

BBC News reader Amor Esry said the building shook as he took this shot
An ammunition dump on the outskirts of the Tanzanian city of Dar es Salaam has exploded killing at least three people.

The BBC's Vicky Ntetema in Dar es Salaam says hundreds of people have been injured as they fled in panic.

Police say several buildings in the area were set alight by debris from the blasts at Mbagala army base.

Shockwaves from at least three explosion were felt throughout the city where the authorities advised workers to vacate their offices.

Many feared a repeat of the deadly bombing linked to al-Qaeda that rocked the country's main commercial centre in 1998.

Polycalypo Makunja was on his way to a market three kilometres away when the explosions began.

"The first thing I did was run. Everybody around me was running away," he told the BBC News website.

"I passed people with injuries - broken arms, bleeding heads. Fires were burning. It was very bad."

'Raining fire'

The armoury next to the army camp, which lies 14km (nine miles) outside the city centre, is thought to have contained large amounts of ordnance, including mines and artillery shells.

This brought back memories of the US embassy explosion in 98. It felt exactly the same way

BBC News website reader Ahmad


UK medic's first day from hell
Tanzania explosions: Eyewitnesses
Our correspondent says nearby Temeke hospital is overwhelmed with casualties and the death toll is expected to rise.

The area affected by the raining debris is large, she says.

She said she saw bomb fragments and the body of a person killed by shrapnel about 15km from army base.

Near the scene of the blast, senior police officer Paul Chagonja told the BBC's Focus on Africa programme they had received an unconfirmed report some children had drowned after jumping in a river while fleeing in the panic after the blast.

He said that a number of houses in the area had been damaged in the explosions.

"Most of them have developed very, very big cracks and some slums have collapsed," he said.

The BBC's John Ngahyoma in the city centre says the blast caused a tremor which was felt at the BBC's offices near the harbour.

Parent fears

Several BBC News website readers in Dar es Salaam said the blast reminded them of the bombing nearly 11 years ago.

"This brought back memories of the US embassy explosion in '98. It felt exactly the same way," e-mailed Ahmad, who was 40km (25 miles) from the site of the ammunition dump.

Others said it seemed like an earthquake.

"It was so powerful that our building shook and the windows were forced open by the impact," wrote Nipun from the city centre.

"We all stood still for a while wondering if it was an earthquake or something else."

Deputy Minister for Defence and Security Emmanuel Nchimbi has cautioned residents to stay away from the area and to vacate all tall buildings as a precautionary measure.

Residents say the evacuation has lead to deadlocked streets.

"The city is in complete chaos as all persons in skyscrapers and other tall building have been ordered to evacuate causing huge traffic jams and confusion," Niklas Rogers told the BBC.

Other Dar es Salaam residents told the BBC there is a school in the area of the explosion.

"They are told to evacuate, [but] the confusion is for those who don't know where their children are," said Henry Amos Tandau.
 
Babu,

Sidhani kama kujiuzulu ndio jibu sahihi hapa! Ila hatua gani zinazochukuliwa kuhakikisha janga hili halileti maafa zaidi ndio jambo la msingi kwa sasa. Moja kuhakikisha sababu za kina zinapatika zilizoleteleza mlipuko. Pili, kuhakikisha hayo mabomu ambayo hayajalipuka hayalipuki. Tatu yale mabomu yaliyorushwa nje ya kambi yanasakwa na jeshi kwa msaada wa wananchi yanapatikana. Nne, misaada ya kihisani iende kwenye jamii kuhakikisha wahanga hawaendelei kudhurika na janga lililetelezwa na jeshi. Tano, baada ya mambo kutulia, hatua zichukuliwe dhidi ya waathirika. Kabla ya hapo, kila mtanzania, kila kiongozi ndani ya serikali na jeshini, lengo liwe moja tu kuhakikisha usalama wa rai na mabomu kutolipuka zaidi.
 
Back
Top Bottom