April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

Babu,

Sidhani kama kujiuzulu ndio jibu sahihi hapa! Ila hatua gani zinazochukuliwa kuhakikisha janga hili halileti maafa zaidi ndio jambo la msingi kwa sasa. Moja kuhakikisha sababu za kina zinapatika zilizoleteleza mlipuko. Pili, kuhakikisha hayo mabomu ambayo hayajalipuka hayalipuki. Tatu yale mabomu yaliyorushwa nje ya kambi yanasakwa na jeshi kwa msaada wa wananchi yanapatikana. Nne, misaada ya kihisani iende kwenye jamii kuhakikisha wahanga hawaendelei kudhurika na janga lililetelezwa na jeshi. Tano, baada ya mambo kutulia, hatua zichukuliwe dhidi ya waathirika. Kabla ya hapo, kila mtanzania, kila kiongozi ndani ya serikali na jeshini, lengo liwe moja tu kuhakikisha usalama wa rai na mabomu kutolipuka zaidi.
 
Haya wadau tuendelee na maombi nimetoka kucheck habari sasa TBC Mnadhimu mkuu ametoa angalizo kuwa bado hatari iko kwani kuna makombora mengine yanaweza kulipuka na kwenda umbali wa KM hadi 21 tunazungumzia Dar nzima wajameni. Yule bwana mdogo wangu tumewasiliana yuko salama japo taarifa ya sasa imeniweka mashakani. Nawashauri watu tusilale majumbani mwetu kwa usiku wa leo maana taarifa za hao wakubwa zinapishana. Nchimbi na Lukuvi wanadai mambo ni shwari wakati wataalam kutoka JWT wanatoa tahadhari. eee mola tukimbilie wapi sisi....heri yeni mnaofuatilia tukio kwenye mtandao.
 
What if all this was deliberately executed by a certain group of people to send a message to a certain group of people?

What if it has something to do with a "warning" to a road-to-2010?

What if.....
 
Tunaomba wahusika watujulishe kama kesho tunaweza kwenda kazini.Walitoa tamko kuwa tuondoke mjini sasa tunaomba maelekezo zaidi.Je waathirika wa Mbagala wamepatiwa mahitaji muhimu kama malazi, chakula na mengineyo kwani leo wamekuwa kama wakimbizi.
Vingozi jamani tuoneani huruma sisi wote ni binadamu tuwasitiri wenzetu

nawakilisha
 
What if all this was deliberately executed by certain group of people to send a message to a certain group of people?

What if it has something to do with a "warning" to a road-to-2010?

What if.....

Terrorist attack?

What if.....?
 
Ndege Ya Obama Yawakimbiza Maofisini Wakazi wa New York

Eneo la Manhattan jijini New YorkTuesday, April 28, 2009 6:01 AM
Baadhi ya wakazi wa New York waliyakimbia majengo yao na ofisi zao kwa kuhofia zahama jingine la septemba 11 baada ya ndege moja ya rais Obama ambayo hawakuitegemea kuzunguka karibu na majengo yao kwa dakika 30.Ndege hiyo Boeing 747 ilizusha hofu na kuwakumbushia wakazi wa New York kasheshe ya septemba 11 mwaka 2001 ambayo ndege za magaidi ziliyagonga na kuzidondosha Twin Towers na kuua watu 3000.

Ndege hiyo iliyokuwa ikisindikizwa na ndege zingine mbili zilizunguka maeneo ya kusini mwa Manhattan na Hudson River kwa takribani dakika 30.

Wafanyakazi wa maofisini walioshindwa kuiona alama ya nembo ya Urais kwenye ndege hiyo, walivikimbia viti vyao na kutoka nje ya majengo yao.

"Niliona kila mtu akikimbia na mimi ikanibidi nikimbie, moyo wangu hadi sasa bado unadunda" alisema mfanyakazi mmoja Jurgens Bauer.

Bauer alisema kwamba chumba chake hakina dirisha hivyo hakuweza kuiona ndege hiyo ambayo imepakwa rangi ya nyeupe ikiwa na rangi ya bluu kwenye pua yake.

Tukio la ndege hizo lilielezewa na maafisa wa Obama kuwa lilikuwa si la dharura na lilikuwa na lengo la kupiga picha maeneo hayo.

"Nilikuwa kwenye tukio la septemba 11 na niliona maelfu ya watu wakifariki, sijapenda kuona tukio hilo la kupiga picha likifanyika bila kupewa taarifa" alisema Bauer.

Polisi walithibitisha kwamba maofisi kadhaa yalikuwa matupu baada ya wafanyakazi wake kukimbia, lakini hawakusema ni ofisi ngapi.

"Nadhani watu walipaniki" alisema msemaji wa polisi.
 

Umesema jambo la akili kweli
 
Polisi walithibitisha kwamba maofisi kadhaa yalikuwa matupu baada ya wafanyakazi wake kukimbia, lakini hawakusema ni ofisi ngapi.



KUMBE HADI NJE;NILIFIKIRI DAR PEKE YAKE WATU WAMEYAKIMBIA OFISI
 
Umesema jambo la akili kweli

WAMESHATANGAZA HALI NI SHWARI MKUU TAARIFA YA HABARI YA ITV;KUANZIA MBAGALA KWENYEWE NA KWINGINEKO
 

Sasa tutajua huruma na upendo wa viongozi wetu.


Baada ya tukio la aina yake hapa Mbagala bila shaka wote tumefungua macho kuona jinsi gani seriklali itakavyolichukulia jambo hili.

Kwa miaka mingi viongozi wetu wamekuwa wakithamini tu maisha yao na ya watu wakubwa na sio sisi wanyonge. Mnyonge hana thamani kabisa katika nchi hii. Akipata ajali iwe kazini, kwenye treni au basi au meli malipo ya fidia ni sawa na hamna kitu. In fact, ni sawa na kutukanwa na kuambiwa wewe na panya au nyoka porini hamna tofauti!

Je, serikali ya awamu ya nne tofauti na zile za waliojithamini na kujipenda wenyewe itakuwa tofauti? Watu watalipwa fidia kutokana na uzembe wa serikali kutoona mbali na kuchukua hata za kuhamisha makambi ya majeshi mbali na makazi ya watu kama inavyopaswa kuwa?

Na, je, serikali itatatuta uzembe ulitokea wapi na kutupa ukweli badala ya kuanza kutulilia machozi ya mamba kama kawaida yao?

Tunasubiri tuone!

Akili
 
Kwa kweli nimehuzunishwa sana na utaratibu wote uliotumika kuwaondoa watu Mbagala, mjini na mengineyo.Kwa tanzania wananchi wa kawida hawadhaminiwi hata kidogo.Sasa hivi ndiyo serikali inakurupuka na kusema kuwa wahanga watatibiwa bure.Askari waliokuwa kwenye tukio walishindwa nini kugrab busses za kuwapeleka wanafunzi au raia kutoka sehemu ya tukio na kuwasogeza mbali.Walikuwa pale kuwafukuza tu watu wasogee mbali.Inasikitisha
hata tuliokuwa magorofani tulitegemea kungekuwa na askari watakaokuwa barabarani kusimamia magari yanayotoka mjini hata yapite lane zote ili watu wapungue mjni. Matokeo yake tulikwama kwenye foleni ndefu na frustrations.It is a shame
Tusubiri tamko kutoka kwa MKUU mwisho wa mwezi kama kawaida. Na litazungumziwa juu juu tu kimzaha.jamani uuuuuuwiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Haya wadau tuendelee na maombi nimetoka kucheck habari sasa TBC Mnadhimu mkuu ametoa angalizo kuwa bado hatari iko kwani kuna makombora mengine yanaweza kulipuka na kwenda umbali wa KM hadi 21 tunazungumzia Dar nzima wajameni. Yule bwana mdogo wangu tumewasiliana yuko salama japo taarifa ya sasa imeniweka mashakani. Nawashauri watu tusilale majumbani mwetu kwa usiku wa leo maana taarifa za hao wakubwa zinapishana. Nchimbi na Lukuvi wanadai mambo ni shwari wakati wataalam kutoka JWT wanatoa tahadhari. eee mola tukimbilie wapi sisi....heri yeni mnaofuatilia tukio kwenye mtandao.

KAZI KWELI KWELI.....TULALE WAPI AMA TURUDI MAOFISINI...
 
Wee acha ndugu yangu!
Majira kama saa 7 nilikuwa nyumbani, wakati nasubiri usafiri nipate kurudi kazini likaingia wimbi la hao watu toka mbagala. Wametembea kwa mguu wakiwa hawajui wanaelekea wapi, bahati nilipo pana kivuli wakaamua kupumzika kwenye kivuli kidogo. Ndipo nilipowafuata na kuwauliza wao ni kina nani na wametoka wapi, du!, moyo uliniuma. Kumbe ndio wametoka mbagala toka saa ili ya milipuko ile mikubwa, ikabidi niagizishe maji ya kunywa ndoo 2. Kati yao kuna watoto wa mpaka miaka kama 6 na 8 hivi, nikajiuliza wametembeaje umbali wote huu. Wenyewe walikuwa busy kuhadithiana jinsi walivyokimbia. Nikawaomba jamaa wawapeleke serikali za mitaa, maana niliona walitaka kuendelea na safari wakati wana watoto wadogo ambao hawafahamiani. Hofu yangu wazazi wao watawatafuta sana, nasikia baada ya mimi kuondoka likaja wimbi jingine. Nalo pia limepelekwa huko huko serekali za mitaa. Sijui wamekwisha rudishwa kwao, au ndio watalala hapo!, watahitaji chakula wale. Jamani msikie tu habari za wakimbizi, kama ule ndio mfano wake Mungu atunusuru. Wengi wako peku, na kuna baadhi ya kina mama wamekuja vifua wazi.
 
What if all this was deliberately executed by a certain group of people to send a message to a certain group of people?

What if it has something to do with a "warning" to a road-to-2010?

What if.....

Interesting angle! However, expand it further not only to be on election of 2010, could be any other intention in relation to home security question! But, that will mean you will need to explore army politics! You will need to ask yourself, what could be the goal of the threat! Home security has never been an agenda in Tanzania politics! That is american politics! Now the intention of harm, especially citizens, will not make any sense at all!

Unless, if the state want to expand its arm base or build partnership with other countries, and so they bomb to justify the need of alliances for home security! But that will not make sense at all, as the state will portray to its citizen it does not have power to protect them. Not only that, state does not have the tradition of taking citizens political view on security questions.

May be there are power center's in the army and their playing around with each other to create balance of power, but that is not practical as the arm has other means of elimination without harming the public. So as much i found this angle interesting, i found no rationally for incident as an organized act.

Personally, for now i will take it as irresponsible act from officials, however, the thought of irresponsibility is so scary, which make your doubts interesting angle for an escape. I will also look into technical conditions - life time of the bombs, test faults, storage conditions, environmental factors - which off set the bombs.
 

Litaundwa BARAZA - kuchunguza tukio

Na hiyo ripoti ya BARAZA itapelekwa kwenye tume maalum.

Cheki mmoja wa hawa wachunguzi alivyosema kuhusu nini kifanywe baada ya kutoa ripoti yake bungeni juzi:

BOT Management should investigate the circumstances in which a sum of Tshs. 7.3 billion was paid to an Insurance Broker in respect of Insurance Premiums of BOT Headquarter Buildings project without sufficient and appropriate supporting documents.
Wakimaliza kuji-investigeti wenyewe, bado independent investigator, bado Tukukuru... aaaaaaah!
 
Last edited:
SHRAPNELS zimefika hadi temeke about 6km from the scene na zingine hadi Kipawa over12km away.Nyumba moja iliyojengwa bila viwango imecollapse Temeke
 
Date::4/29/2009
Milipuko ya Mabomu:Majeruhi wafurika hospitali za Dar

Na Peter Edson na Jackson Odoyo
Mwananchi

ZAIDI ya watu 300 waliojeruhiwa katika mlipuko wa mabomu walifurika katika hospitali za Temeke, Amana, Muhimbili, Lugalo, vituo vya afya vya Sabrina na Charambe kupata matibabu.

Kumiminika kwa majeruhi hao katika hospitali hizo kuliwafanya madaktari na manesi kuacha kuwahudumia wagonjwa wa magonjwa mengine ili kunusuru maisha ya wananchi hao.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Dk Aisha Mahita alisema hadi kufikia saa 11.00 jioni walikuwa wapokea majeruhi zaidi ya 100.

"Kama unavyoona mwenyewe, tunaendelea kupokea majeruhi pamoja na miili ya marehemu, na hivi sasa hatuna mahali pengine pa kuwahifadhi kwa kuwa hospitali imejaa," alisema Mahita

Alisema pamoja na majeruhi hao Dk Mahita alithibitisha kupokea maiti za watoto watatu ambao alisema hawajatambuliwa.

Hata hivyo alisisitiza kuwa wanajitahidi kwa kila hali kuhakikisha kuwa wanawahudumia vizuri majeruhi waote waliofika hospitalini hapo.

Naye Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, Silvia Mamkwe alisema mbali na majeruhi waliofikishwa katika hospital hiyo, wengine 300 wamehifadhiwa katika Kituo cha Afya cha Sabrina na kwamba, wauguzi kadhaa na daktari mmoja wa hospitali hiyo walipelekwa katika huko pamoja na vifaa muhimu kwa ajili ya kuwahudumia majeruhi hao.

Alisema wagonjwa wengine wamehifadhiwa katika kituo cha afya cha Charambe ambao alisema hali zao zinaendelea vizuri na wengi wao walipata matibabu na kuruhusiwa.

"Taarifa zetu za awali zinaeleza kuwa majruhi wengi waliaofikishwa katika hospitali hizi ni wale waliopata mshituko wa mabomu na siyo waliojeruhiwa," alisema Mamkwe.

Mwandishi wa mwananchi aliyefika katika eneo la tukio alishuhudia maiti ya mama mmoja na mtoto wake zikifikishwa katika kituo cha polisi tayari kupelekwa katika hospitali ya Temeke.

Mama huyo alikatwa shingo na bombo huku mtoto wake akiwa amefunuliwa kichwa na ubongo kuwa nje.

Habari kutoka katika hospitali ya Amana, zinaeleza kuwa watu wawili wajeruhiwa katika tukio walifikishwa kwa ajili ya matibabu na wengine zaidi ya 24 walipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baadhi yao wakiwa katika hali mbaya.

Kitengo cha mifupa cha Muhimbili kulikuwa na majeruhi 17 na mmoja amelazwa katika kitengo cha ungalizi maalumu wagonjwa ICU, mmoja amekatika mguu na mmoja mama mjamzito ambaye hali yake mbaya.

Akizungumza na Mwananchi Afisa Uhusiano wa Moi, Almas Jumaa alisema baadhi yao ni mbaya na kwamba wengine wanaendelea vizuri.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Jerome Bwanausi aliyefika katika hospitali ya Temeke, alisema tukio lililotokea jana ni kubwa na linaigharimu wilaya hiyo.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuwa watulivu na kusubiri vyombo vya usalama vikifanya kazi yake.
 

Well, good analysis, thanks man.
 
Kwa hali ya mambo ilivyo katika nchi yetu, mara nyingine ni ngumu kujua kama hii ni ajari au ni uzembe uliosababisha watu kuumia na kupoteza maisha, pamoja na mali nyingi kuteketea.Mbagala wanaishi wananchi wa kawaida.I try to imagine the structures I normally see there if they could withstand such powerful blast forces.All in all, kama huku kwingine kuna uozo mkubwa katika mambo ya kiutawala sitaki kuamini kama na jeshini kuna matatizo hayo maana tutakuwa tunapoteza maisha ya wapiganaji wetu kila kukicha. Kule karibu kila kitu ukikifanya ndivyo sivyo kinageuka na kuleta balaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…