Huge explosions rocked an ammunition dump at an army camp in Tanzania's commercial capital Wednesday, killing three people and injuring more than 150, officials said.
Haya maswala ya makazi kuchanganyika na kambi za jeshi, zifikie maala uongozi wa nchi kuangalia upya. Miaka 30-40 nyuma idadi ya wakazi wa Mbagala haikuwa kubwa kiasi cha kuwa karibu sana na kambi hizi za jeshi.
Hali imekuwa tofauti na sasa... Mji unapanuka watu wanafikia kuishi just few yard kutoka kwenye kambi za jeshi.
Hii yote ni kutokana na mipango miji kuwa mibovu. Wataalam wetu huwa wanashindwa kufanya makadirio ya ongezeko la idadi ya watu kwenye miji mikubwa kama DSM. Ni bora sasa ilo linalo itwa
ammunition dump aidha liamishwe na kubakia just infantry with out so called
ammunition dump au
wakaazi wa eneo lililo karibu na makazi ya jeshi waamishwe na kulipwa fidia ya usumbufu na mali zao.
Hizi mbinu za nchi za kijamaa jeshi kukaa karibu na raiya ili kuweza kulitumia jeshi pindi tu watu watakapotaka kufanya mapinduzi au maasi, inaonekana sasa imepitwa na wakati.
Hatuhitaji tena tena kambi za jeshi kuwa karibu na raiya, ukizingatia kuwa kambi zenyewe ndizo hizo hizo zenye kuifadhi
expired ammunition.
Tena kwenye Ghala lililo zungushiwa mabati kama sikosei kama si under ground. Tz ni kubwa sana katika nchi za East Afrika, kuna maeneo Tz tangia kuumbwa kwa hii dunia binadamu hajawai kukanyaga huko. Kwanini serikali/Jeshi lisihamue kupeleka huko mbali kabisa na kwenda kuangamiza hayo mabomu na ammunition zinazo semekana zimepitwa na muda wake...(!?) Hapa mi nashindwa kupata picha halisi... Hivi ni kweli this so called Ammo zinafikia ku'expire ni zile ambazo zipo tangia enzi ya kina Tip tip na Mkwawa au ni zile zilizo tumika kwenye vita vya maji maji?
Ninavyo fahamu mimi Ghala la siraha linakuwa kept clean, cool and dry na kufia mpaka those Ammo kuwa expire may take many, many years to reach a point of unsuitability, hapa tunazungumzia kuanzia miaka 50-70 or longer.
Sasa hizi ambazo zinafikia mpaka kuripuka tu, mbona haiingii akilini? Au ndio zile ambazo wakati wa production ndizo zilizo kuwa rejected, kisha tukazi nunua kwa bei ya kutupa...!? Na hata hii sidhani kama inakubalika.
Au ni zile ambazo tulizirithi toka mkoroni!? Nashindwa kuelewa...! I'm shocked.
This is serious matter tena ime'involve maisha ya raiya, bora yangewakumba hao hao wanajeshi tungesema ajali kazini. Lakini kuwakuta raiya wasio juwa hata mbinu za kujihokoa pindi maafa kama haya yakitokea ni jambo kubwa sana hili.
Tufikie wakati sasa tusema kuwa TUMECHOKA HATUTAKI TENA.
Kwani hii ni dhurma kubwa sana kukatiza uhai wa raiya na wakazi wasio na hati.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un... Tuna wapa pole sana wakazi wa mbagala kwa maafa yalio wakuta. Insha'Allah M'Mungu azipokee roho za marehemu na kuzipumzisha kwa Aman.
Ila sisi ambao bado tu HAI tusimame sasa kwani wahenga walisema Amkani si shwari tena. Ni lini itafikia kipindi tutasema BASI.