Aprili 12 ni Siku ya Watoto Waishio Mitaani Duniani

Aprili 12 ni Siku ya Watoto Waishio Mitaani Duniani

Dkt. Gwajima D

Minister
Joined
Nov 28, 2015
Posts
966
Reaction score
6,019
Salaam nyingi za za upendo kwenu wote.

Aprili 12, kila mwaka ni Siku ya Mtoto wa Mtaani Duniani.
Kaulimbiu Mwaka huu ni ‘TUWAJIBIKE’.

Uwajibikaji uanze ngazi ya familia kwa wazazi/ walezi kutimiza jukumu la kulea. Sheria ya Mtoto Sura ya 13 kifungu cha 6 – 13, kila Mlezi/ Mzazi anawajibika kuwalinda Watoto na kufanya familia mahali salama. Kutotimiza wajibu huu ni kosa kisheria na adhabu yake ni faini isiyozidi milioni 5 au kifungo miezi 6 au vyote viwili.

Vilevile, ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kijiji, Kata, Halmashauri, Tawala za Mikoa, Taasisi za Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia, Viongozi wa Dini, Wazee wa Kimila na Watu binafsi watekeleze sheria, ufuatiliaji na kutoa huduma za usaidizi kwa watoto na familia zenye changamoto. Aidha, waelimishe jamii kufahamu madhila ya watoto kuishi mitaani na kuzuia vihatarishi vinavyochochea watoto kuondoka majumbani na watoe taarifa ofisi za Serikali pale penye vihatarishi na dalili za mtoto kutoweka nyumbani. Ikitokea ametoweka, taarifa zitolewe kwa hatua stahiki.

Wadau pia waunganishe nguvu kuelimisha jamii umuhimu wa malezi ya watoto na vijana ndani ya familia. Wizara tutaimarisha ufuatiliaji wa utekelezaji na kutoa mrejesho kwa jamii.

Julai 2021 hadi Aprili 2024, jumla watoto 6,459 (Wavulana 4,356, Wasichana 2,103) walitambuliwa katika mikoa sita (6) yenye idadi kubwa ya kundi hilo (Dar, Mwanza, Arusha, Mbeya, Iringa na Dodoma ambapo;

Watoto 1,346 (Wavulana 919, Wasichana 427) waliunganishwa na familia zao na kati ya hao;

1. Watoto 816 (Wavulana 605, Wasichana 211) waliunganishwa na mafunzo ya ufundi stadi na kupatiwa mitaji na vifaa vya vya kazi waweze kujitegemea,

2. Watoto 3,427 (Wavulana 2,301, Wasichana 1,126) walipewa vifaa vya shule na mahitaji mbalimbali,

3. Watoto 273 (Wavulana 175, Wasichana 98) walipewa huduma ya kuimarisha uchumi wa kaya,

4. Watoto 597 (Me 356, Ke 241) wako kwenye Vituo maalum na Makao ya Watoto wakiandaliwa kwa ajili ya utengamao.

Athari za watoto kuishi mitaani; kukosa mengi ikiwemo malezi ya kiroho, matunzo, afya, elimu, kufanyiwa ukatili, kutumia dawa za kulevya na kujihusisha na uhalifu.

Wanahabari, naomba tuendelee kutoa taarifa za elimu kwa jamii. Jamii ipige pia Simu za Wizara Na. 0262 160 250 / 0734 986 503, na kuandika ujumbe 0774 112 233 / 0769 608 130 / 0766 400 168.

PAMOJA TUKIWAJIBIKA; INAWEZAKANA.🇹🇿

Ahsanteni.

7417db1c-bcc8-4303-b381-48b992c3fbab.jpeg
 
  • Ahsante Mungu kwa malezi niliyopata.
  • Wanyama na ndege wanatunza watoto wao, ila binadamu anatelekeza damu yake.
  • Huku watu wengine wanahaha usiku na mchana kupata watoto, wengine wanawatupa. Binadamu ni kiumbe mtata sana.
 
Aah mi nkikumbuka kipindi upo wazir wa afya kipind cha Rais Magufuli nakata tamaa kabisa na wew. Yani sina imani na wew cjui kwann
 
Muheshimiwa!
Maeneo ya posta na ndani ya panton kuna biashara inayoendelea ya watoto chini ya miaka 15 wanadhurula na mzazi wao, wanatumika kuomba hela kwa watu, hili tatizo ni la muda mrefu sana.

Kama Waziri mwenye dhamana una mpango upi wa kutokomeza hio tabia kwasababu kuomba hela sio shida lakini watoto wale wanatakiwa wawe madarasani wanasoma.
Kama ulivyoona takwimu ni kuwa, serikali inafanya mikakati ya kuwaondoa lakini baadhi ya jamii wanakoishi hao watoto kamati zao za kijamii zenye wajumbe wa kijamii za ulinzi wa watoto zinawajibika kidogo au hakuna kabisa. Na kama unavyoona, mfumo unaanzia mamlaka ya serikali ya mtaa, Kijiji, kata, halmashauri na mkoa husika, mpango wangu kuhusu taarifa hii ni sasa hivi nawasilisha kwa Mhe Mkuu wa Mkoa husika na Wilaya husika kwa hatua stahiki na kujumuishwa kwenye mipango na mikakati kwa matokeo kama ulivyoona hiyo taarifa hapo juu.

Aidha, naomba jamii tuendelee kushirikiana kwenye kuzuia zaidi kuliko kusubiri waingie mtaani. Hatua za kufanya Ili kuzuia zimeelezwa hapo kwenye taarifa.

Ahsante sana kwa mchango wako wa maoni.
 
Aah mi nkikumbuka kipindi upo wazir wa afya kipind cha Rais Magufuli nakata tamaa kabisa na wew. Yani sina imani na wew cjui kwann
Mimi Nina Imani kubwa na wewe kwamba utashirikiana kwenye kudhibiti na kutokomeza kabisa watoto wa mtaani na ukatili wa kijinsia na kwa watoto na ajenda zingine zote tunazozileta kwenye jamii. Shukrani
 
Dr, Mungu akubariki sana.
Kuna Post yako ya X jinsi ya kuasili mtoto, tumeijadili baada ya miaka miwili tutaifanyia kazi.
 
  • Ahsante Mungu kwa malezi niliyopata.
  • Wanyama na ndege wanatunza watoto wao, ila binadamu anatelekeza damu yake.
  • Huku watu wengine wanahaha usiku na mchana kupata watoto, wengine wanawatupa. Binadamu ni kiumbe mtata sana.
Ndiyo ajabu ya sisi binadamu.
 
Mimi Nina Imani kubwa na wewe kwamba itashirikina kwenye kudhibiti na kutokomeza kabisa watoto wa mtaani na ukatili wa kijinsia na kwa watoto na ajenda zingine zote tunazozileta kwenye jamii. Shukrani
Ni kweli kwa hili la watoto yatima linahitaji malezi bora kuanzia ngazi ya familia ambapo wananchi tunatakiwa kua na mchango mkubwa ili serikali isiwe na mzigo mkubwa hapo baadae katika nyanja tofauti ikiwepo watoto hao kufkia kujiajiri au kujiwezesha kimaisha.
 
Dr, Mungu akubariki sana.
Kuna Post yako ya X jinsi ya kuasili mtoto, tumeijadili baada ya miaka miwili tutaifanyia kazi.
Ahsaysana kwa ufuatiliaji wa habari za wizara ya Jamii. Mwenyezi Mungu awe pamoja nanyi katika kuifanyia kazi🙏🏽🤝
 
Walitabiri mvua tarehe hii na inapiga kweli aisee
 
Mungu akusimamie katika utendaji wako

umekua si mtu wa kujikweza, unawasikiliza watanzania bila kubagua ni jambo jema kwa kweli
 
Mawaziri wote wakiwa hivi kuna mahali pazuri tutafika kama taifa. Mitandao ya kijamii ni sehemu muhimu na rahisi zaidi kuwa na mjadala na jamii kubwa kwa wakati mmoja kwa sasa. Viongozi wengine waone hili.

Barikiwa sana Mheshimiwa Dkt. Gwajima D
 
Huu ujumbe pia uwafikie wazazi wanaotelekeza watoto hadi kupelekea kuongezeka watoto wa mitaani
 
Saiv pia Kuna familia za Mitaani wakina mama wanawatuma Watoto kuomba fedha. Watoto wa Road April mwaka huu tuna jambo letu
 
Back
Top Bottom