Arab contractor wanakabidhi bwawa la umeme, watu elfu 11 wameshiriki kulijenga, ndio Mradi Mkubwa wa kiuhandisi kuwahi kutokea Tanzania

Arab contractor wanakabidhi bwawa la umeme, watu elfu 11 wameshiriki kulijenga, ndio Mradi Mkubwa wa kiuhandisi kuwahi kutokea Tanzania

Kazi nzuri sana.
Pamoja na mapungufu na maneno maneno lakini mradi umekamilika.
Katika hili nimpongeze rais John Pombe Magufuli kwa kusimama imara kuhakikisha bwawa linajengwa.
Rais lazima uwe na msimamo, usimamie maono ya nchi na watu wako.
Kuhusiana na kukatika katika umeme hiyo ni ajenda nyingine.
Tuanze sasa kujenga njia mpya za kusafirisha umeme ili hatimaye umeme huu umfikie mlaji.
 
Hiyo hesabu unayonifundisha ni ya dunia hiihii au
namsaidia mtoa mada.

Katika kazi za engineering, person-hour (saa-mtu) ni kipimo cha juhudi za kazi, kinachowakilisha saa moja ya kazi inayofanywa na mtu mmoja. Person hour Inatumika kupima jumla ya muda unaohitajika kukamilisha kazi fulani kulingana na idadi ya watu wanaofanya kazi hiyo.

Mfano:
  • Ikiwa kazi inahitaji 10 person-hours, inaweza kufanywa na mtu mmoja kwa saa 10, au watu 5 kwa saa 2 kila mmoja.
  • Inasaidia katika kupanga muda, bajeti, na rasilimali kwa miradi mbalimbali.

tukirudi kwenye hoja

haya masaa ya kazi milion 72, yamepatikana kwa kujumlisha masaa ya kazi ya watu wote elfu 11, ambayo ni sahihi.

watu elfu 11 wakifanya kazi kwa masaa kumi tu kwa siku ni sawa sawa na person hours laki moja na elfu kumi, sasa hayo masaa laki moja na elfu kumi ni ya siku moja tu. je wakifanya miaka mitano utapata masaa mangapi ?

ndivyo jinsi tunavyo calculate masaa ya kazi kwenye engineering projects
 
Kuna miradi ilikamilika na haikuweza ku-deliver kama ilivyokusudiwa...pesa zilipigwa haswa, mradi chini ya usimamizi wa serikali ya JK, ufadhili wa IMF.

Huu pia, pesa zimepigwa haswaaa, na kama wamefikia hatua ya kukabidhi basi angalau DSM yote na ukanda wote wa pwani tungeanza kuona faida za uwepo wa umeme! Ila ndo unakatika kuliko kawaida.
Wewe unaishi Dar ipi ambayo umeme unakatika kuliko kawaida au unafanya siasa?
 
Mradi umekamilika kwa 100% kwa matilion ya pesa na kuharibu ecosystem
je utaleta manufaa gani kwa mwanachi maskini?

count down..tunasubiri kuona ufanisi na uendeshwaji wake kama unatija kwa Taifa.
 
umeme unakatika sababu ya Transmission na distribution lines, Arab contractor hawakuja kujenga transmission line, hivyo mpaka leo transmission line na distribution line ni zile zile za zamani ndio zinasafirisha umeme wa bwawa, hivyo zinazidiwa nguvu sababu uwezo wake ni mdogo na zimechoka, ni kazi ya Tanesco kubadilisha transimission lines
Ni sababu nzuri, nakubali.

Watumiaji walioungwa kwenye mfumo walikuwa ni wengi kuliko uzalishaji, hii ndio ilikuwa hoja nambari moja.

Wakati huo miundombinu ilikuaje?
Transmission lines, una maanisha grid sio?
  • Ina maana tuliamua kujenga Power Plant ya 2.115GW tukitegemea transmission line iliyopo?
  • Msongo wa kilovolts ngapi unasafirishwa kutoka Bwawani? 400 au 220?
  • Tanesco walikuwa na mpango wa kusambaza umeme kupitia 33kV/0.4kV badala ya 11kV/0.4kV, walitekeleza hili?

Kama walifanikisha, sioni shida inatokea wapi, maana unapofanya maboresho ni lazima uzingatie future.

Hivi, substation za kupooza kutoka njia kuu, huwa zinajengwa kila mkoa au wilaya? Najua Dar zipo kadhaa, mikoani ikoje?
- Hakuna namna kukawa na substation ya mkoa, kama ni ya zamani, ikaboreshwa/upgraded kupokea umeme mkubwa na kusambaza kwingineko kwa ku-cover eneo lote la mkoa?

Kama mikoa yote haijaungwa kwenye grid, hiyo ni changamoto! Na ndio maana Grid huwa inaanguka mara kwa mara, maana grid sio ringi...mwaka jana mwishoni, imepiga chini mara kadhaa.
 
namsaidia mtoa mada.

Katika kazi za engineering, person-hour (saa-mtu) ni kipimo cha juhudi za kazi, kinachowakilisha saa moja ya kazi inayofanywa na mtu mmoja. Person hour Inatumika kupima jumla ya muda unaohitajika kukamilisha kazi fulani kulingana na idadi ya watu wanaofanya kazi hiyo.

Mfano:
  • Ikiwa kazi inahitaji 10 person-hours, inaweza kufanywa na mtu mmoja kwa saa 10, au watu 5 kwa saa 2 kila mmoja.
  • Inasaidia katika kupanga muda, bajeti, na rasilimali kwa miradi mbalimbali.

tukirudi kwenye hoja

haya masaa ya kazi milion 72, yamepatikana kwa kujumlisha masaa ya kazi ya watu wote elfu 11, ambayo ni sahihi.

watu elfu 11 wakifanya kazi kwa masaa kumi tu kwa siku ni sawa sawa na person hours laki moja na elfu kumi, sasa hayo masaa laki moja na elfu kumi ni ya siku moja tu. je wakifanya miaka mitano utapata masaa mangapi ?

ndivyo jinsi tunavyo calculate masaa ya kazi kwenye engineering projects
Unadhani tutakuelewa?
 
Ni miaka zaidi ya 8000 yani mtoa mada anamaanisha bwawa limejengwa kabla ya Kristu hadi leo alafu anasema limejengwa haraka
Katika muktadha wa ujenzi, "person-hours" (saa za mtu) ni kipimo kinachoonyesha jumla ya muda wa kazi uliotumika kwenye mradi fulani, kwa kuzingatia idadi ya wafanyakazi na muda waliotumia kufanya kazi.

Kwa hiyo, "72 million person-hours" (saa milioni 72 za mtu) inamaanisha kwamba kazi ya ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere imetumia jumla ya saa milioni 72 za kazi, ikiwa tunajumlisha muda wote ambao wafanyakazi wote wametumia kwa pamoja kwenye mradi huo.

Mfano wa kuelewa hii:

Ikiwa wafanyakazi 10,000 walifanya kazi kwa saa 8 kila siku kwa miaka 3, hesabu yake inaweza kuwa:
10,000 × 8 × 365 × 3 = 87,600,000 person-hours

Kwa hivyo, saa milioni 72 za mtu zinaonyesha kiwango kikubwa cha kazi na juhudi zilizowekwa kwenye mradi huo mkubwa wa taifa.
 
kuna tofauti kati ya uzalishaji wa umeme na miundo mbinu ya kusafirishia umeme, sasa hilo la miundo mbinu ya kusafririshia umeme raisi samia ndiyo angepaswa kulitatua, umeme tayari upo …
Exactly watu hawaelewi , kuwa na umeme na kusambaza ni vitu viwili tofauti, transformers kubadilisha nchi nzima na nguzo ni costly siyo zoezi la siku mbili, ni mkakati endelevu, ila kwa mradi huu imapaswa kujipongeza kama nchi, nchi nyingi afrika ikiwemo mwenye uchumi mkubwa southafrica hawana umeme wa kutosha ila tanzania tumeweza
 
Person-hours/man-hours ni masaa ambayo watu wamefanya kazi, hivyo unachukua idadi ya watu zidisha kwa masaa waliofanya kazi
Sawa mkuu. Hapo nimeelewa

Sasa tuje kwenye data kwa mujibu wa taarifa za mleta mada

Watu 11,856
Person - Hours 72,000,000 ÷ Watu 11,855 = Masaa 6,072

Kwa hiyo masaa halisi ni 6,072.

Masaa 24 = Siku 1
Masaa 6,072 = Siku ngapi?
6,072 ÷24 = siku 253

Kwa hiyo kwa siku 253, ikiwa wafanyakazi 11856 walifanya kazi masaa 24 kila siku, kwa siku 253 jumla ya hizo person hours ni 71,989,682.
 
Back
Top Bottom