dah!
mara nyingi kunakuwepo na viashiria ambavyo vinaweza onekana tangu udogoni.
viashiria hivi vinaweza kuwa kutambuliwa na mtu wa familia ambaye tayari yuko kwenye system. ikitokea hivi na huyo mtu wa familia akaona utafaa basi anaweza akawa "anakulea" na kukujenga ili baadae iwe rahisi kukushawishi kuingia huko.
aidha viashiria hivi vinaweza kuonekana katika mfumo wa makuzi na elimu, mfano mwalimu wako, jirani yako, ndugu wa rafiki yako n.k.
pia wapo wataalamu kutoka ofisi kuu ambao nao wanajukumu la kutambua vipaji (potential candidates).
baada ya "kuonekana" unafaa inakuja ushawishi na kukujengea mazingira ya utakapo fuatwa na kuombwa kujiunga usisite kukubali. miaka ya awali chuo kikuu na jkt vilikuwa viwanja vya mawindo kwa watu wa "taaluma". mkufunzi kutoka makao makuu alikuwa na "warsha" ya siku moja na wanafunzi wa mwaka wa kwanza kuwaelezea umuhimu wa usalama hii ilikuwa ni mbinu ya kuwatayarisha wanafunzi kifikra ili wanapofuatwa wasisite kujiunga (ikumbukwe wakati huo chuo kikuu kilikuwa kimoja tu, hivyo hapo ndio palikuwa na jumuiko la wasomi wetu). idm mzumbe pia ulikuwa uwanja wa ajira(ingawa wakati huo haikuwa chuo kikuu)
kwa maneno mengine mtu anazaliwa na viashiria lakini viashiria hivyo lazima viboreshwe. usisahau kila sehemu hawa watu wapo kuanzia walimu, madaktari, wahandisi, wachumi, wahasibu, viongozi wa dini, wanasiasa nk. hata watu wasio na taaluma mahususi pia wapo. japokuwa kama alivyosema mchangiaji moja hapo juu sio kila mwenye viashiria ameajiriwa au ameonwa. wengine wanaviashiria husika lakini mazingira ya malezi/makuzi yao yamefanya wawe na viashiria vingine vyenye nguvu zaidi hivyo kuwa disqualify.
naamini nimekusaidia kidogo