Are spies made or born?

Are spies made or born?

Mimi swali langu la kwanza ni je, mtu anaweza kuingia kwenye hii system akiwa mtu mzima mathalani miaka 35-40 kwa mfumo wa hapa Tanzania?
Usalama wa nchi yetu ni jukumu la kila mtanzania iwe askari ama raia wa kawaida pasipo kujali umri, jinsia, dini au kabila.......
 
Mimi swali langu la kwanza ni je, mtu anaweza kuingia kwenye hii system akiwa mtu mzima mathalani miaka 35-40 kwa mfumo wa hapa Tanzania?
Swali la pili, je, mtu anaweza kufanyiwa closely invetsigations baadae akapotezewa hata kwa miaka 5-10 na kisha akaja kuchukuliwa tena au ukiona hivyo ndo ujue ni disqualified?

Sifahamu kwa Tz! Lakini kwa nchi za wenzetu umri sio hoja ili mradi tu kuna jambo unaweza fanikisha waweza tumika wakati wowote ule.

Mfano Eli Cohen alitamani sana kujiunga na Mossad lakini kila alipo apply alitolewa nje kuwa hana vigezo!(disqualified).
Baada ya miaka kadhaa walimtafuta wao wenyewe na kumsihi ajiunge nao kwa sababu hawakuwa na agent kabisa katika nchi za kiarabu na Eli Cohen alijua Kiarabu vizuri na Utamaduni wao.
Aliifanyia Israel mambo mazuri sana! ingawaje mwisho wake haukuwa mzuri.
 
Mkuu wale jamaa kwa nchi za wenzetu huwa wanazaliwa wakiwa na baadhi ya attributes/tabia fulani hivi kisha wanaongezewa tradecraft/ujuzi wa kimafunzo...baada ya hapo weeee wanakuwa ni moto wa kuotea mbali...!
Nami naamini kabisa katika traits anazozaliwa nazo mtuu kisha akiwa backed na trainings huyo atakuwa kila siku mambo yake anafanya kama novel movie fulani hivi...Talent kwamfano ya kujua mawazo ya mtu kabla hajafanya action, kujua outcome kabla hata tukio halijaanza i.e prediction ile precision ni capacity ya brain ku integrate vitu na ku connects dots ku produce outcomes...Unaweza kuwa trained lakink kama akili ni butu thubutu ndiyo kila mara unaishia kuumbuka
 
kuna siku baba aliniambia hivi'' you must be the right person not necessarily the best one''.....akaendela kusema they always look for the right person not the best one...ipo tfauti kubwa ya mafanikio ya darasani na kazi hii...sisemi elimu haifai lakini hapana lakini kuna vitu vingine vinaangaliwa kwenye mambo haya:..
kuna siku kuna kijana mmoja darasani alikuwa ana akil sana ya darasani..makaratasi yake ya mitihani yalionyesha ufaulu wa hali ya juu sana...basi mda mwafaka ukafika na nikaanza kumuliza tofauti ya shuguli na kazi, jibu na jawabu...nikamuuliza tena ili eneo flani liitwe kijiji linapaswa kuwa na sifa gani?.....majawabu yake yalishindwa kukidhi haja yangu ..kwa kifupi he was the best not the right one!!!

nimeona humu michango ya watu na kila mtu amechangia kwa namna anavyojua..nadhani huko nyuma kwenye thread hii nimeeleza watu wa kazi hiyo wanapaswa kuwa wa aina ipi...lakini nisema hivi kila eneo la kazi hii huwa linahitaji watu wa aina flani...wasomi na maprof wapo wana eneo lao..walevi,malaya, waongo, nk.....
hii kazi ni kazi yenye risk kubwa na faida pia ipo kubwa tu ya kuwa huko kikubwa ni kwamba unaishi kwenye kivuli mpaka mwisho, kila kinachopit mbele unajiuliza ni nini hiki na kwa nini kiwe hapa nilipo, humuamini mtu labda maiti tu, utulivu wa akili unatakiwa, uweo wa kutunza siri nk...
wapo watu hawana elimu kubwa lakini mambo yao wanayofanya ni makubwa balaa huko idarani...kuna mtoto wangu tangu akiwa mdogo nimemfundisha namna ya kuwasiliana na mimi..nimemfundisha karibu njia tano za namnaya kuongea na mimi..nimemfundisha pia namna ya kutambua nini kinaongelewa na watu wawili walio umbali flani nini wanaongea kwa kuwaangalia lips za midomo yao na ishara za mikono....hata kama hasikii sauti zao na mikono wakiweka mfukoni still anatambua nini kinaongelewa...
shida kubwa ni watu wengi kujaza uchafu mwingi kwenye vichwa vyao..kukosa utulivu wa nafsi, kutokuwa wadadisi, shidakuwa sehemu ya maisha yao, kufikiri jambo moja kila siku... kwa siku katika kichwa cha average person huwa kuna idadi ya mawazo 60,000 yanayokuwa processed...lakini 95% ya mawazo hayo ni yale yale aliyofikiri jana...mtu wa aina hii hawezi kuendelea katika jambo lolote
sasa kazi kama hizi zinahitaji watu makini wenye utulivu mkubwa wa akili, wanaojielewa nini wanakifanya....wengi wanazaliwa wakiwa watu wazuri tu wenye hizo mnazoita IQ kubwa lakini kadri wanavyokua na kujaza ucha mwingi kichwani ndivyo wanavyokosa sifa

jambo la mwisho aliloniambia baba ni alisema hivi '' your IQ is nothing to us, what matters to us is your i can''
MWAMBA de'levis popote pale ulipo, pokea salamu zangu.
 
Atakuwa anatumia akaunti zingine, mtu kama yule sio rahisi kupotea humu
Mkuu, leo nilichungulia status yake nikamuona online ingawa anaonekana sio mchangiaji sana. Inaonekana huwa anasoma tu na kuondoka.
 
nadhani ni katik thread hii niliwahi kutaja sifa za mtu anaefaa kuwa jasusi..nitazirejea kwa kifupi..
1. jasusi lazima awe na kumbu kumbu..hii ni sifa muhimu sana lazima akili yake iwe ina rekodi kila jambo na kila hatua anayopitia na kwa usahihi..kuanzia asubuhi ambo yoote unayofanya/unakpita unarekodi kisha jioni unaandika report ya kika kitu bila kuacha..na pia ukiulizw ajambo lililotokea wiki mbili zilizopita ulikumbuke kwa usahihi na kwa mapaa yake..kuna watu hawana kumbu kumbu yaani hat kushika namba5 za simu hawezi..binafsi sina jina la mtu yeyote kwene simu yangu bali namba tu na ninajua namba hii ni ya nani na hata kuitaja..niliifundisha akili katika hilo..so kumbu kumbu ni sifa muhimu
2.. lazima jasusi afikiri kuwa mantiki (logic)...lazima ujiulize kwa nini hik kiko hivi na ninaweza vipi kukibadilisha katika muonekano huu na kikawa kitu kingine, kufikiri kwa logic ni muhimu sana, na katika kufikiri lazima ujiulize , why, who, where, what etc...ukiwa mtu wa kukurupuka lazima uumie..
3.lazima awe mtu wa kuchunguza (observation)..haijalishi mahali alipo lazima achunguze mazingira na nini kinaendelea..ukiingia ndani ya nyumba lazima uichunguze kwa mda mfupi na kwa umahiri mkubwa ujue ina milango migapi, madirisha, nk nk..akili lazima iwe inarekodi..na lazima uangalie escape route iwapo kutatokea shida..mlango lioingia sio wa kuutegema sana..
4..jasusi lazima ajue kubadilika kulingana na mazingira au eneo alilopo..awajue watu wanaomzunguka wanataka nini na ni wa aina gani..jasusi laizma ajue kucheza na hisia za watu(sifa muhimu sana hii)
5..jasusi lazima ajue kusikiliza milango yote 7 ya fahamu(sio 5 ni 7)..katika ubongo wa mwanandam kuna maelekezo mengisana yanayomuonya mtu juu ya jambo flan.(wengine wanaita machale) machale haya humuonya mtu juu ya hatari iliyo mbele so ni lazima jasusi ajue namna ya kusukiliz amilango yake yote na kuchukua hata inayostahili kama yu katika hatari

hapo ni baadhi ya sifa anazopaswa kuwa nazo jasusi..sasa ukiangalia sifa hizo hakuna hata moja hapo ianayofundishwa darasani zote ni za kuzaliwa...na kwa kweli wote tunazaliwa tukiwa pure isipokuwa tunajaza uchafu mwingi kwenye ubongo na kuharibu nguvu ya akili...hata katika maisha ya mtu wa kawaida tu sifa hizo hapo juu ni muhimu sana..huwezi kuyatawala mazingira kama huna utulivu wa akali.... The mind is a good servant but a terrible master...lazim akili yako uitawala na uitume ifanya jemabo flani sio yenyewe ikutme wewe kufanya jambo flani..
sasa ukiw ana sifa hizo hapo juu na zingine ambazo sijazitaja kisha ukaingizwa darasana na kunolewa sawa sawa lazima ufnay mambo makubwa..

ndugu zangu mambo haya huwa hayaji hivi hivi ni lazima ujitume katika kuhakikisha akili yako inakuwa sawa mda wote na u-keep low profile,upayukaji hauhusiki, majigambo,nk...ukiishi kama mastaa wa movie hwezi chukua round ktik game hii...
kwenda kwenye vyuo vya mafunzo haya ,,,huko unaongezewa mbinu mfano za kutumia silaha za aina zote, namna ya kujihami, namna ya kugoma kuhojiwa iwapo utakamatwa....
mazingira ya ujasusi yamezungukwa na hatari, ukiwa, upweke na kivuli so nilazima jasusi ajifunze mbinu zoe za awali za kazi hii (tradecraft)...

kwa hiyo naweza kusema kuwa watu hawa sifa kubwa ni zile za kuzaliwa kisha wanaingizwa darasan/vyuoni ili kupewa mafunzo kufit mahitaji yaliyopo...

nimalize kwa kunukuu maneno ya mwalimu wangu:
1 when you control your thoughts, you control your mind, when you cotrol your mind you control your life; and once you reach a stage of being in total contolof your life you become the master f your own destine.

2..Alwys life favors the prepared mind
3.. in life there is no mistakes but lessons...sometime pain can be a good teacher

NB: mwambieni Invisible auweke uzii huu sticky maana kuna mda nautafuta siupati

The 7 Habits of Highly Successful Intelligence Analysts

Source: The 7 Habits of Highly Successful Intelligence Analysts
 
Kuna siku moja dogo mmoja mwanafunzi wa chuo alikuwa maeneo ya mjini katika mkoa flani akiwa na mwenzake wa kiume pia ghafla akajikuka mikononi mwa askari wawili wenye sare na mmoja amevalia kiraia tu (plain clothes) na kumwambia kuwa anahitajika katika ktuo cha polisi kuna malalamiko dhidi yake na ilibidi ayatolee maelezo yeye peke yake. Kwa kuwa yule kijana hakuwa ametenda kosa lolote la kihalifu wala hakubishana nao, yeye alienda nao tu moja kwa moja mpaka kituoni kisha mahojiano yakaanza kati ya askari hao na yule kijana katika chumba kidogo kilichopo ndani ya kile kituo kwa muda kama wa masaa 2 na nusu hivi kisha akaachiwa. Baada ya kama mwezi mmoja baada ya tukio, yule kijana aliwaaga wenzake kuwa anaenda nyumbani ameitwa kuna matatizo ya kifamilia kisha atarudi ndani ya muda mfupi. Alivyoenda ndio kimoja mpaka leo wenzake hawakumuona tena mpaka leo hii na hakuna anayejua wale askari walimwambia nini kwenye yale mahojiano.
"yasiyokuhusu ni kujaacha kama yalivyo"
Hao ni watu wakitengo au ni polisi?
 
mkuu, tunafutana tongotongo kwa hizi mambo za "lip reading" ...... mimi sijui kabisa kama kuna professions za namna hii hapa duniani. kweli ushamba ni mziggo
Hapa lazima mlango wa sita wa ufahamu utumike (intellect (manas)) hii ipo kihisia zaidi
 
Wanakuzwa wale kwa trainng toka wadg uwez chukua spy wa miaka 4 au 3 ni kwanzia miez na mwaka mmoja...pia huingia mkataba na familia ya huyo mtoto.
Mara nyingi hao wanaochukuliwa wakiwa wadogo lazima kunamtu wake wakaribu ambaye yupo kwenye system au mawakala mfano mzazi,kiongozi wa dini(mch,padri,shekh na kn),mwalimu au hata jirani wa muda mrefu (family friends) hawa watu wakaribu husaidia kumshape mlengwa ili aje kufit kwa kazi maalum hapo baadae bila yeye kujua Ila akionyesha kukengeuka au tabia ambayo ni mwiko kwa kitengo atakuwa disqualified watampotezea naitabaki stori nyumba ya njaa HIYO NILIKUWA NAWAZA TU
 
Back
Top Bottom