Hahaha.Mimi mdada akishabikia Mpira nafurahi sana, huyo Carlos Tevez ni Muargentina, labda kama ulimmaanisha Roberto Carlos [emoji23]Yani toka elfu mbili na ushee nashabikia brazil enzi hizo kina kaka,kina Rivaldo,kina carlos tevez,kina ronaldinho,kina wengii kwa kipindi tofauti tofauti. Ronaldo de Lima alikua na sura personal lakini tulikuwepoo. [emoji38]
Ameonywa sanaaaa...ameambiwa kabisa aache u childish[emoji23]Brazil wanatimu kali sana na group simple sana watafika ata fainali ila kuna vijana mule hawajitambui wakileta utoto tena safari hii watazngua sana aswa yule dogo neema uwa ana utoto sana
Nigeria hajawahi vuka 16 boraWamewahi mara moja enzi za okocha
Tbc ya wapi inayoonyesha mechi zote mkuu? Hii ya Tanzania itaonyesha mechi 28 tu πππTbc sio watupange kuwa wataonyesha game zote halafu siku ya siku Argentina wako uwanjani halafu wakatize mechi wajiunge na Ikulu Dsm Raisi anazindua madarasa ya uviko 19. Sintowasamehe kabisa
Labda TANESCO wafanye yaoTutaanzia hapo kwenye sherehe huku tukisubiri mechi
Msimu huu sitaki kupitwa na chochote kwenye haya mashindano
Oooh yess umeonaa ee tuvumilieni tuu kaka zetu π π π π eee yule mwenye vigimbii mfupi kweli kweliHahaha...Mimi mdada akishabikia Mpira nafurahi sana, huyo Carlos Tevez ni Muargentina, labda kama ulimmaanisha Roberto Carlos [emoji23]
Ila Big up
Mc Garab ni misuti yake ile kashafika huko?View attachment 2383741
Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kufanyika kuanzia November 20 mpaka December 18 mwaka huu. Michuano ya mwaka huu ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kufanyika katika nchi ya Kiarabu lakini ni mara ya pili kwa michuano hiyo kufanyika katika bara la Asia mara baada ya Korea Kusini na Japan kuandaa kwa pamoja mwaka 2002.
Pia michuano ya mwaka huu, ni kwa mara ya kwanza kufanyika nje ya utaratibu uliozoelekea wa mwezi May, June au July. Michuano ya safari hii itafanyika mwezi November mpaka December kutokana hali ya hewa kuwa rafiki tofauti na joto kali la miezi ya May, June au July.
Qatar ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, itakuwa ni mara yao ya kwanza kufuzu toka Kombe la Dunia lianzishwe. Hivyo wametumia vyema nafasi ya mwenyeji kufuzu automatic.
Kombe la Dunia la mwaka huu 2022 litakuwa la mwisho kushirikisha timu 32 kama ilivyo katika utaratibu wake.
Kuanzia michuano ijayo ya mwaka 2026 itakuwa inashirikisha timu 48.
Mpira wa Kombe la Dunia la mwaka huu, unajulikana kama "Al Rihla" ikiwa na maana ya " the journey " safari kwa kiswahili. Ni mpira maalum ambao umetengenezwa na Adidas huku ukiwa umefungwa kifaa maalum cha kusaidia kugundua offside kwa haraka zaidi.
Michuano hiyo itafanyika katika viwanja vinane ndani ya majiji matano. Kiwanja mojawapo ambacho ni kivutio ni "Stadium 974" ambapo kimetengenezwa kwa kutumia makontena 974 na kitavunjwa punde baada ya kumalizika kwa michuano hiyo.
Vikosi vya timu vitaanza kutangazwa mapema mwezi ujao wa November na kila timu itatakiwa kuwa na wachezaji 26 badala ya 23 kama ilivyozoeleka.
Mechi ya ufunguzi tarehe 20 Nov itamuhusisha mwenyeji ambapo itakuwa ni Qatar Vs Ecuador.
Kwa raundi mbili za mwanzoni katika hatua ya makundi, mechi zitapigwa katika majira yafuatayo; Saa 7:00 mchana, Saa 10:00 jioni, Saa 1:00 Usiku na Saa 4:00 Usiku.
Baada ya hapo, mechi za raundi ya mwisho za makundi, mechibza mtoano mpaka Fainali zitakuwa zikipigwa Saa 1:00 usiku na Saa 4:00 usiku.
Masaa ya Qatar ni sawa kabisa na masaa ya hapa Afrika Mashariki, hivyo muda utakuwa unafanana.
Tutashuhudia mechi zote 64 kupitia DStv. Kwa wale wa kustream, Hesgoal.com itakuwa chaguo sahihi kwako.
Updates zote za vikosi vitakavyoitwa, ratiba za mechi, jezi, uchambuzi na mengineyo utayapata hapahapa kwenye uzi huu.
Karibuni sana...
View attachment 2383805
Ratiba kamili ya Mechi za Kombe la Dunia 2022 Qatar
Kumbuka: Muda wa Mechi ni kwa saa za Afrika Mashariki HATUA YA MAKUNDI RAUNDI YA 16 ROBO FAINALI NUSU FAINALI FAINALIwww.jamiiforums.com
Mungu sikia kilio chetu baba.....Dominika ya Leo huko Agerntina imetumika kuombea Messi na Agentina wafanye vizuri kwenye kombe la dunia
Mimi napenda mpira ila messi alinifanya niupende zaidi mpira
Mungu hatukupangii ila tunaomba bahati iwe upande wa Agentina
Naamini pia Pope Fransis leo huko Rome katika misa ya St Peters ameiombea heri Agentina
Na ghana 2010Nigeria hajawahi vuka 16 bora
Africa ni Senegal na Cameroon tuu ndio walifika robo toka tournament zianzishwe
Walipigwa na kitu kizito....Van P mtu mbadiMashabiki wa Spain msijisahaulisheView attachment 2422041
Acha kabisa ikikaribia tarehe hamu inakataπππ Marejesho ya mikopo jau Sana....
Na ghana mzee umesahau 2010 Gyan akatulaza na viatu kwenye tutaNigeria hajawahi vuka 16 bora
Africa ni Senegal na Cameroon tuu ndio walifika robo toka tournament zianzishwe
Acha tuu sijui tulikuwa na gundu gani mkuuNa ghana mzee umesahau 2010 Gyan akatulaza na viatu kwenye tuta
hawaonyeshi game zoteTbc sio watupange kuwa wataonyesha game zote halafu siku ya siku Argentina wako uwanjani halafu wakatize mechi wajiunge na Ikulu Dsm Raisi anazindua madarasa ya uviko 19. Sintowasamehe kabisa
Mc Garab ni misuti yake ile kashafika huko?