Yani toka elfu mbili na ushee nashabikia brazil enzi hizo kina kaka,kina Rivaldo,kina carlos tevez,kina ronaldinho,kina wengii kwa kipindi tofauti tofauti. Ronaldo de Lima alikua na sura personal lakini tulikuwepoo. [emoji38]
Brazil wanatimu kali sana na group simple sana watafika ata fainali ila kuna vijana mule hawajitambui wakileta utoto tena safari hii watazngua sana aswa yule dogo neema uwa ana utoto sana
Tbc sio watupange kuwa wataonyesha game zote halafu siku ya siku Argentina wako uwanjani halafu wakatize mechi wajiunge na Ikulu Dsm Raisi anazindua madarasa ya uviko 19. Sintowasamehe kabisa
Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kufanyika kuanzia November 20 mpaka December 18 mwaka huu. Michuano ya mwaka huu ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kufanyika katika nchi ya Kiarabu lakini ni mara ya pili kwa michuano hiyo kufanyika katika bara la Asia mara baada ya Korea Kusini na Japan kuandaa kwa pamoja mwaka 2002.
Pia michuano ya mwaka huu, ni kwa mara ya kwanza kufanyika nje ya utaratibu uliozoelekea wa mwezi May, June au July. Michuano ya safari hii itafanyika mwezi November mpaka December kutokana hali ya hewa kuwa rafiki tofauti na joto kali la miezi ya May, June au July.
Qatar ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, itakuwa ni mara yao ya kwanza kufuzu toka Kombe la Dunia lianzishwe. Hivyo wametumia vyema nafasi ya mwenyeji kufuzu automatic.
Kombe la Dunia la mwaka huu 2022 litakuwa la mwisho kushirikisha timu 32 kama ilivyo katika utaratibu wake.
Kuanzia michuano ijayo ya mwaka 2026 itakuwa inashirikisha timu 48.
Mpira wa Kombe la Dunia la mwaka huu, unajulikana kama "Al Rihla" ikiwa na maana ya " the journey " safari kwa kiswahili. Ni mpira maalum ambao umetengenezwa na Adidas huku ukiwa umefungwa kifaa maalum cha kusaidia kugundua offside kwa haraka zaidi.
Michuano hiyo itafanyika katika viwanja vinane ndani ya majiji matano. Kiwanja mojawapo ambacho ni kivutio ni "Stadium 974" ambapo kimetengenezwa kwa kutumia makontena 974 na kitavunjwa punde baada ya kumalizika kwa michuano hiyo.
Vikosi vya timu vitaanza kutangazwa mapema mwezi ujao wa November na kila timu itatakiwa kuwa na wachezaji 26 badala ya 23 kama ilivyozoeleka.
Mechi ya ufunguzi tarehe 20 Nov itamuhusisha mwenyeji ambapo itakuwa ni Qatar Vs Ecuador.
Kwa raundi mbili za mwanzoni katika hatua ya makundi, mechi zitapigwa katika majira yafuatayo; Saa 7:00 mchana, Saa 10:00 jioni, Saa 1:00 Usiku na Saa 4:00 Usiku.
Baada ya hapo, mechi za raundi ya mwisho za makundi, mechibza mtoano mpaka Fainali zitakuwa zikipigwa Saa 1:00 usiku na Saa 4:00 usiku.
Masaa ya Qatar ni sawa kabisa na masaa ya hapa Afrika Mashariki, hivyo muda utakuwa unafanana.
Tutashuhudia mechi zote 64 kupitia DStv. Kwa wale wa kustream, Hesgoal.com itakuwa chaguo sahihi kwako.
Updates zote za vikosi vitakavyoitwa, ratiba za mechi, jezi, uchambuzi na mengineyo utayapata hapahapa kwenye uzi huu.
Tbc sio watupange kuwa wataonyesha game zote halafu siku ya siku Argentina wako uwanjani halafu wakatize mechi wajiunge na Ikulu Dsm Raisi anazindua madarasa ya uviko 19. Sintowasamehe kabisa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.