Argentina yatwaa ubingwa Kombe la Dunia - Qatar 2022

Argentina yatwaa ubingwa Kombe la Dunia - Qatar 2022

View attachment 2383741
Kombe la Dunia linatarajiwa kuanza mwezi ujao hapo nchini Qatar.

Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika kuanzia November 20 mpaka December 18 mwaka huu. Michuano ya mwaka huu ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kufanyika katika nchi ya Kiarabu lakini ni mara ya pili kwa michuano hiyo kufanyika katika bara la Asia mara baada ya Korea Kusini na Japan kuandaa kwa pamoja mwaka 2002.

Pia michuano ya mwaka huu, ni kwa mara ya kwanza kufanyika nje ya utaratibu uliozoelekea wa mwezi May, June au July. Michuano ya safari hii itafanyika mwezi November mpaka December kutokana hali ya hewa kuwa rafiki tofauti na joto kali la miezi ya May, June au July.

Qatar ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, itakuwa ni mara yao ya kwanza kufuzu toka Kombe la Dunia lianzishwe. Hivyo wametumia vyema nafasi ya mwenyeji kufuzu automatic.

Kombe la Dunia la mwaka huu 2022 litakuwa la mwisho kushirikisha timu 32 kama ilivyo katika utaratibu wake.
Kuanzia michuano ijayo ya mwaka 2026 itakuwa inashirikisha timu 48.

Mpira wa Kombe la Dunia la mwaka huu, unajulikana kama "Al Rihla" ikiwa na maana ya " the journey " safari kwa kiswahili. Ni mpira maalum ambao umetengenezwa na Adidas huku ukiwa umefungwa kifaa maalum cha kusaidia kugundua offside kwa haraka zaidi.

Michuano hiyo itafanyika katika viwanja vinane ndani ya majiji matano. Kiwanja mojawapo ambacho ni kivutio ni "Stadium 974" ambapo kimetengenezwa kwa kutumia makontena 974 na kitavunjwa punde baada ya kumalizika kwa michuano hiyo.

Vikosi vya timu vitaanza kutangazwa mapema mwezi ujao wa November na kila timu itatakiwa kuwa na wachezaji 26 badala ya 23 kama ilivyozoeleka.

Mechi ya ufunguzi tarehe 20 Nov itamuhusisha mwenyeji ambapo itakuwa ni Qatar Vs Ecuador.

Kwa raundi mbili za mwanzoni katika hatua ya makundi, mechi zitapigwa katika majira yafuatayo; Saa 7:00 mchana, Saa 10:00 jioni, Saa 1:00 Usiku na Saa 4:00 Usiku.

Baada ya hapo, mechi za raundi ya mwisho za makundi, mechibza mtoano mpaka Fainali zitakuwa zikipigwa Saa 1:00 usiku na Saa 4:00 usiku.

Masaa ya Qatar ni sawa kabisa na masaa ya hapa Afrika Mashariki, hivyo muda utakuwa unafanana.

Tutashuhudia mechi zote 64 kupitia DStv, Star times, Canal Plus bado sijajua kwa AzamTv. Kwa wale wa kustream, Hesgoal.com itakuwa chaguo sahihi kwako.

Updates zote za vikosi vitakavyoitwa, ratiba za mechi, jezi, uchambuzi na mengineyo utayapata hapahapa kwenye uzi huu.

Karibuni sana...
View attachment 2383805
Asante kwa maelezo mazuri
 
Hawa tbc sidhani Kama wataonyesha mechi zote. Wanagimba weeh halafu wanaishia kuonyesha mechi 30 tu [emoji23][emoji23]
Wamesema watarusha mechi 28 kwenye tv

Mechi 64 kwenye kutangaza

Ni wababaishaji tu ikifika muda wa hotuba wanatabia ya kukatisha mpira kupisha hotuba mpaka iishe ni kama huwa wanacheza na hisia za watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamesema watarusha mechi 28 kwenye tv

Mechi 64 kwenye kutangaza

Ni wababaishaji tu ikifika muda wa hotuba wanatabia ya kukatisha mpira kupisha hotuba mpaka iishe ni kama huwa wanacheza na hisia za watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani katika mechi 64 wataonyesha 28 tu? Hizo zingine tutaishia kusikiliza kwenye radio yao? Mbona wamechagua kuonyesha mechi chache sana, si wangesema hata 40 jamani.
 
David De Gea ameachwa katika kikosi cha wachezaji 55 wa awali wa Spain licha ya kuitwa kwa magolikipa watano.

Kikosi hiko kitapunguzwa hadi wachezaji 26.
Mimi Man U ila kwa kweli DeGea simkubali, licha ya kutuokoa kwenye baadhi ya mechi lakini kwa misimu mingi amekuwa akifanya makosa ya wazi na kuigharimu timu .
 
Pogba atakosa fainali za kombe la dunia baada ya kuumia tena
A4AF4184-8764-4A8F-B95C-E0620AE1EC62.jpeg
 
Team samba nipo hapa..Brazil akikosa chukua hili kombe kwa sasa,atakua hana bahati tu
.
 
Back
Top Bottom