Argentina yatwaa ubingwa Kombe la Dunia - Qatar 2022

Argentina yatwaa ubingwa Kombe la Dunia - Qatar 2022

Brazil wanatimu kali sana na group simple sana watafika ata fainali ila kuna vijana mule hawajitambui wakileta utoto tena safari hii watazngua sana aswa yule dogo neema uwa ana utoto sana
Sio Neymar tu Kuna Vinicius Jr hata Richarlison utoto mwingi sana.
 
France anaishia group stage ,hii ni laana ya world cup winner ....

Kawaulize German ,Spain baada ya kuchukua world cup .....
Benzema, Kante, Pogba, hawapo, iko kazi
Hao wachezaji ndio walikuwa key katika ubingwa wa 2018
 
D5034E7C-0895-480E-894B-E90EDDDB5D00.jpeg
 
View attachment 2383741

Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kufanyika kuanzia November 20 mpaka December 18 mwaka huu. Michuano ya mwaka huu ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kufanyika katika nchi ya Kiarabu lakini ni mara ya pili kwa michuano hiyo kufanyika katika bara la Asia mara baada ya Korea Kusini na Japan kuandaa kwa pamoja mwaka 2002.

Pia michuano ya mwaka huu, ni kwa mara ya kwanza kufanyika nje ya utaratibu uliozoelekea wa mwezi May, June au July. Michuano ya safari hii itafanyika mwezi November mpaka December kutokana hali ya hewa kuwa rafiki tofauti na joto kali la miezi ya May, June au July.

Qatar ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, itakuwa ni mara yao ya kwanza kufuzu toka Kombe la Dunia lianzishwe. Hivyo wametumia vyema nafasi ya mwenyeji kufuzu automatic.

Kombe la Dunia la mwaka huu 2022 litakuwa la mwisho kushirikisha timu 32 kama ilivyo katika utaratibu wake.
Kuanzia michuano ijayo ya mwaka 2026 itakuwa inashirikisha timu 48.

Mpira wa Kombe la Dunia la mwaka huu, unajulikana kama "Al Rihla" ikiwa na maana ya " the journey " safari kwa kiswahili. Ni mpira maalum ambao umetengenezwa na Adidas huku ukiwa umefungwa kifaa maalum cha kusaidia kugundua offside kwa haraka zaidi.

Michuano hiyo itafanyika katika viwanja vinane ndani ya majiji matano. Kiwanja mojawapo ambacho ni kivutio ni "Stadium 974" ambapo kimetengenezwa kwa kutumia makontena 974 na kitavunjwa punde baada ya kumalizika kwa michuano hiyo.

Vikosi vya timu vitaanza kutangazwa mapema mwezi ujao wa November na kila timu itatakiwa kuwa na wachezaji 26 badala ya 23 kama ilivyozoeleka.

Mechi ya ufunguzi tarehe 20 Nov itamuhusisha mwenyeji ambapo itakuwa ni Qatar Vs Ecuador.

Kwa raundi mbili za mwanzoni katika hatua ya makundi, mechi zitapigwa katika majira yafuatayo; Saa 7:00 mchana, Saa 10:00 jioni, Saa 1:00 Usiku na Saa 4:00 Usiku.

Baada ya hapo, mechi za raundi ya mwisho za makundi, mechibza mtoano mpaka Fainali zitakuwa zikipigwa Saa 1:00 usiku na Saa 4:00 usiku.

Masaa ya Qatar ni sawa kabisa na masaa ya hapa Afrika Mashariki, hivyo muda utakuwa unafanana.

Tutashuhudia mechi zote 64 kupitia DStv. Kwa wale wa kustream, Hesgoal.com itakuwa chaguo sahihi kwako.

Updates zote za vikosi vitakavyoitwa, ratiba za mechi, jezi, uchambuzi na mengineyo utayapata hapahapa kwenye uzi huu.

Karibuni sana...
View attachment 2383805

UTABIRI WA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA...

Baada ya kusikiliza na kufuatilia wachambuzi wa soccer wakubwa duniani wa kwenye media kama BBC, SKYSPORT wakitabiri matokeo ya kombe la dunia mwaka huu Qatar nimekuja na hitimisho kama ifuatavyo

Timu zinatabiriwa kuchukua kombe la dunia ni 👇

1.BRAZIL
2.ARGENTINA
3.FRANCE
4.GERMANY

Kiukweli 😀😀kwa kikosi walichonacho Brazil chenye world class players washindwe wao tu maana wapo kundi rahisi sana tena zaidi ya kundi la Argentina na ndo maana wanapewa nafasi kubwa kutwaa kombe la dunia mwaka huu , wakifuatiwa na Argentina ambao nao wapo kundi zuri sana na ndo muda wa Messi kuthibitisha ni mchezaji bora wa dunia.

Timu zinazoweza kumaliza hatua ya makundi kwa kushinda mechi zote ni 👇

1.Brazil
2.Argentina

Timu ambazo ni dhaifu na wanaweza kuondoka bila point au na point 1 na watu watajipigia mi naziita underdogs 👇

1.Iran
2.Saudi Arabia
3.Qatar

Timu Kutoka Africa ambayo ni pekee itafika hatua ya makundi ni 👇

1. SENEGAL

Wafungaji Bora wa Kombe la Dunia ni 👇

1.Messi
2.Neymar
3.Mbappe

Na napenda kuwapa matokeo ya mechi za kadhaa tu za hatua ya makundi

1. Belgium vs Canada
Atashinda Belgium

2.Brazil vs Serbia
Atashinda Brazil

3.Portugal vs Ghana
Atashinda Portugal

4.Senegal vs Netherlands
Atashinda Netherlands

5.England vs Iran
Atashinda England

6.Argentina na Saudi Arabia
Atashinda Argentina

7.France vs Australia
Atashinda France

8.Spain vs Costa Rica
Atashinda Spain
 
Luis Enrique:
"If Busquets was the extension of Del Bosque in the field, what is yours?

Ferran Torres is mine,
if not my daughter cuts my head off”
 
Back
Top Bottom