Nimewasikiliza wachambuzi wa ule mchezo wakiongozwa na Michael Owen wote wamesema lile goli lilikuwa ni halali. Kanuni ya off side ni kuwa, kuwa off side siyo kosa kikubwa ni kuwa mchezaji aliyeko off side asiingilie/asiathiri uchezaji wa huo mpira.
Tukija kwa Griezmann, ule mpira ulomkuta akiwa off side na hakuathiri uchezaji wa ule mpira, yeye alitulia tu.
Mabeki wakawa wanaokoa ule mpira, na Griezmann akondoka eneo la off side, hivyo anakuja kukutana na ule mpira akiwa on side na kufunga. Tafsiri ya off side ya mwamuzi ndio imeleta utata zaidi.