Mbappe tunamkubali sana lakini anahitaji jitihada beyond human limits, nidhamu, na muhimu kuliko yote kudra za Mungu kuweza kufika walau robo ya ambacho Messi na Ronaldo wameifanyia dunia ya mpira.
Mtu kama Messi kama ulibahatika kumuona wakati ana miaka 19, wakati anavaa jezi namba 30, baadae akavaa namba 19 long before hajaanza hata kuvaa namba 10, wakati anapiga hat trick mbele ya Madrid ilojaa wachezaji wakali wote ulokua unawajua, huwezi kumkweza Mbappe mapema hivi.
Mimi Messi nimeanza kumfuatilia game moja ya UEFA na Chelsea ilichezwa darajani, Chelsea ilikua na watu wana roho mbaya kuliko unavyoweza kudhania ila kijana miaka 19 alikua anaweza kutembea na mabeki hata wanne kwenye chaki na anafika anakokwenda fresh tuu, the rest ni historia.
Baada ya VAR kuwa introduced kwenye mpira na baada ya generation ya Messi na Ronaldo kupita, nitaacha rasmi kushabikia mpira, nitakua naangalia kama burudani halafu nitahamia tu UFC.