Arnold Schwarzenegger: Heaven is 'Fantasy' and 'Nothing' happens when we die

Arnold Schwarzenegger: Heaven is 'Fantasy' and 'Nothing' happens when we die

Ukitaka kusema mwanadamu exists unatakiwa uthibitishe katokea wapi, wewe ni mwanadamu, do u exists? Umetokea wapi? Thibitisha umetokea kwa nyani
Huyo maku hawezi kukujibu,yupo kwenye mtanziko wa kifikra akidhani ana fikra jadidi,muulize pia ikiwa ana akili,akikwambia anazo mwambie athibitishe,uone anavyojibu,atarukaruka tu,Mimi Alisha ni-ignore baada ya mjadala kumzidia
 
Tukiwa wazima huwa tunatamba na kuongea vyovyote kwa mbwembwe, subri tuelekee kwenye point of no return hapo balaa linaanza.

Katika Ulimwengu huu mwanadamu ni punje ndogo sana kuliko mchanga wa bahari, anajifanya mjuaji wakati hata 0.00000001% ya Ulimwengu huu haijui.

Ukimuuliza habari za baharini hata 10% hajui halafu anatunishiana misuli na MUNGU MKUU SANA aliyeumba vyote hivyo na kuviwekea mfumo wa kujiendesha


Kama yupo anayeweza kujiongezea japo miaka walau afikishe 2500 basi nitaelekea kusikiliza hoja zaje, nje ya hapo ni mpango wa Shetani na wafuasi wake waliouza nafsi zao kwa Lucifer kuwahadaa wana wa Mungu eti hakuna maisha baada ya kifo au Mungu hayupo ili mwisho wawe wengi huko motoni.
 
Wakikaribia kufa ndo kauli zao hizo,hiyo yote hofu maana ananusa harufu ya mauti na maisha yake yote alimsahau Mungu,Sasa duniani ana bangalows huko anakoenda anaona kabisa Hana kitu...hakuna Mungu yaani universe imejileta tu na sayari dunia imekua habitable(kukalika) by chance tu!!..ni kutofikiri
Wakikaribia kufa huwa wanamkumbuka Mungu wa imani gani?

Vipi kama siku ya kufa we ukawa unamkumbuka Allah wakati kule juu yupo Yahweh, je hiyo itakuwa na manufaa yeyote kwako?

Sasa kwa mantiki hiyo ukiambiwa saizi uanze kumuabudu Yahweh utakubali kwasababu ya kuogopa siku yako ya kufa?
 
Tukiwa wazima huwa tunatamba na kuongea vyovyote kwa mbwembwe, subri tuelekee kwenye point of no return hapo balaa linaanza....
Kifo ni ushahidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Kifo kinaumiza watu, kinatenganisha watu, kinaleta majonzi.

Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao kifo kinachotenganisha watu wanaopendana sana, kinachowatenganisha kwa huzuni kuu na maumivu yasiyomithilika kiwezekane?

That is a contradiction.

Unaweza kutatua hii contradiction?
 
Mwanadamu akisha kua na pumzi kila kitu anaweza kusema

Ila subiri aumwe na kichwa tu atahangaika kuutafuta Uzima bcz anaogopa kifo
Kuumwa na kichwa nako ni ushahidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeumba ulimwengu ambao magonjwa yanawezekana.

Mungu huyo, kwa sifa zake hizo, si mkatili hivyo.

Uwezekano wa watu kuumwa ugonjwa wowote ni ushahidi kwamba huyo Mungu hayupo.

Unaelewa hilo?
 
Utahakikishaje hizo hadithi za "spiritual" zinaeleza mambo ambayo yapo kweli na si tungo za kihadithi tu zisizo na ukweli?

Unaruhusiwa kuwa na imani yako, lakini, ukianza kusema imani yako ipo kwenye ukweli, unatakiwa uthibitishe hilo.
Nisibitisheje wakati ninacho kiona ww ukiaangalia hukioni
 
Back
Top Bottom