...ahami mtu hapa, atahama yeye AW! π‘
Haswaaaaaaaaa,kuhama timu eti wachezaji wameondoka tu,ujue wewe simpenzi wa kweli wa mpira.
tutahama pale ARSENAL itakapofutwa kwenye ulimwengu wa soka duniani.
Usiwe shabiki tumbowazi!!
Mbaya sana hizi habari kwetu sisi wapenzi nguli wa Arsenal
Sijajua kwanini Wenger amekua na hii tabia ya kuuza wachezaji wazuri lakini anashindwa kununua wachezaji wazuri.
Na Arsenal itabaki na hili tatizo siku zote hasa pale msimu unapokuwa mzunguko wa pili na utakuta majeruhi kibao tena wachezaji muhimu sana. Tatizo kubwa la Arsenal ni kwamba wakati timu nyingine zina vikosi viwili ambvyo vinaweza kucheza mechi zake na kushinda yenyewe Arsenal ina kikosi kimoja tu, ndio ukweli Arsenal haina subsititute tofauti na Manchester United na Chelsea. Ndio maana sintoshangaa sana kama itatolewa kwenye top four! Nimeshaji-tune hivyo kwa kuwa naipenda sana hii timu toka enzi za akina Ian Wright, David Seaman na wengineo.
Lakini pamoja na upungufu huu Arsenal will always be my best team kwa mpira mzuri inaocheza ambao hakuna timu nyingine ya Uingereza inacheza mchezo huo.
Tupo pamoja mkuu.
hatuhami na wala hututaacha kuipenda hii timu.
Ila ninachokiona hapa siyo wenga bali ni uongozi na hasa huyo anaejiia bilionea wa kirusi.huyo hana mtizamo wa mpira ndio anasababisha haya yote.
Timu inapokuwa na wachezaji nguli ni lazima nawe uwaangalie katika suala zima la maslahi na pia ni lazima ujipange kutafuta vifaa vingine vya kujazia hapo na kuiongeza unguli wa timu.
Gunners forever!
Hiyo timu iko nchi gani?Szombathelyi Haladas 0- Arsenal 5
habari ndio hizo kolo toure kashaenda man city kwa pound mil 15 na atakula mshahara pound 120,000 kwa wiki.kazi hipo hapa.
Kashatua City?wakubwa kolo toure kashaenda man city kwa pound mil 15.
Mhe Kisoda hapa umenena
Kuhama tim kwa kuwa wachezaji fulani wameondoka ni sawa na kuhiama familia yenu kwa kuwa dada yako ameolewa.
Arsenal itaendelea kuwa chama langu siku zote hata kama itashuka daraja achilia mbali kuondolewa kwenye top four, sio kitu mpira unadunda na hata huyo Man City nae anatafuta mafanikio ambayo Arsenal amekuwa nayo miaka nenda miaka rudi,
Kwanini tusijifunze kwa mashabiki wa Juventus na Newcastle ambao pamoja na timu zao kushuka daraja kwa vipindi tofauti lakini bado waliendelea kuishabikia timu na kwenda uwanjani kushangilia kwa nguvu zote.
Tatizo sisi tuna mapenzi ya mpira ule wa Simba na Yanga kwamba siku Simba aun Yanga wanacheza na Toto Affirca hakuna shabiki wala mwanachama wa timu hizo anayekwenda uwanjani hadi siku ya mechi ya Simba na Yanga ndio uwanja ujae
Ukipenda mpira ndugu zangu hata ukipita ukakuta ule wa mchangani unachezwa utasimama na kuutazama pasipo wewe kujua umesimama. Sasa kama mpira wewe ni mpaka siku ya Man U na Chelsea au Arsenal na Man U basi wewe sio mpenzi wa mpira ila mdokozi wa mpira
Nawasilisha
wakubwa kolo toure kashaenda man city kwa pound mil 15.
Manchester United manager Sir Alex Ferguson says Manchester City "are a small club with a small mentality
How Arsene develops his team will be his biggest test.
The one thing we know about Arsenal is that they will play some of the best football you will see and create chances. They could easily re-establish themselves and challenge for the league again."
kaondolewa kwenye pre season karudi kujakudiscuss terms na kufanya medical.Kashatua City?
Beki wa kati amebaki huyo aliyetoka Ajax na Song atachezeshwa bekiwakubwa kolo toure kashaenda man city kwa pound mil 15.
Kila mchezaji akiondoka mnamponda, wa kulaumiwa ni WengerHabib Toure akwende zake. Anaonekana mzito mno siku hizi. Kuna possibility kubwa alidanganya umri.