Artequine zanipeleka balaa

Artequine zanipeleka balaa

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Nina siku ya nne leo tokea nimalize dozi ya siku tatu ya Dawa za malaria aina ya Artequine toka Swiss. Nilishairiwa ni njema na makini kwa malaria ili isijirudie. Hata hivyo nilipomaliza tu dozi nikaanza kupata kizunguzungu kikali sana, moyo ukawa unaenda kasi kama BP imepanda na mwili ku chill. Leo siku ya nne kizunguzungu sio sana ila nipo restless mwili kama umepigwa shot ya umeme; unashtuka hata kusikua kelele za mlango; sijisikii vyema kusikiliza watu wakiongea; kichwa kizito na napoteza umakini (concentration).
Nimeonana na Tabibu anasema ni hali ya kawaida.

Wataalamu wa Afya mnaoifahamu hii dawa tafadhali naomba ushauri...au kwa waliopata kutumia.
 
Pole ndugu ngoshwe ,kwa sasa jitahidi kunywa kiasi kikubwa cha maji mara kwa mara, Hiyo hali itakwisha baada ya muda.
 
Last edited by a moderator:
Kunywa maji na pia soda aina ya Fanta kurejesha sukari iliyoisha mwilini. Dawa za malaria hushusha sukari mwilini kama njia ya kupambana na vidudu
 
Kunywa maji kwa wingi lakini pia jaribu kupata Juice ya Cranberry ya Ceres au ya masafi (sina kumbukumbu vizuri ya jina hl kama ni Safi au Masafi)

Juice hz zipo supermarkets lkn kama waweza pata cranberry yenyewe kwenye hizi supermarket itakuwa poa zaidi

Nice recovery brethren
 
Hii dawa inajulikana kwa kusababisha matatizo kwenye moyo na hilo ndilo lilikokusababishia kuhisi moyo unapepesuka (palpitation). Tatizo hili hupimwa kwa kutumia ECG (electrocardiogram) ambayo huonesha electrical conductivity of the heart.

Kama bado unajisikia vibaya basi kamwone dokta afanye ECG ....Na kama mfumo wa utendaji kazi wa moyo umeathirika basi kuna dawa ambazo unaweza kutumia kama Clopidogrel + coated asprin. Zinasaidia sana kurekebisha matatizo ya moyo kupepesuka.
 
Waliokuuzia walikudanganya!kuugua malaria kuko palepale kama hujikingi kung'atwa na mbu.Kwa sasa hakuna dawa inayoweza kutumika na usiugue maralia muda mrefu.Binafsi nimetumia dawa nyingi kama hiyo Artequin,Artequick,Duo cotexin,Metakefin,Fansidar,ALU,na Artemether inj. lakini maralia inajirudia tu baada ya mwezi!Nilikuja kupata dawa inayoitwa Arco nikaipenda sana kwani licha ya kumeza x moja tu sikusumbuliwa na maralia muda mrefu.Nimeitafuta tena hivi majuzi nimeambiwa ati haipo kabisa nchini sijui kwa nini maana hata taarifa huwa hazipo rasmi.Kwa sasa nimetumia Chloroquine imenisaidia vizuri mno ingawa nayo ilipigwa marufuku kisiasa tu ili wajanja watengeneze ulaji.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Niliambiwa chloroqiluine hazipo sokoni. Zinapatikana wapi kwa Dar?
Artequick na Arco inasemekana zimeondolewa sokoni kutokana na kufanya wagonjwa wa malaria kujenga usugu wa dawa. Kwa kiasi cha dozi ya mara moja au mbili haziui vyema wadudu wa malaria. Hii ipo kwa Metacalfin nazo za dozi moja (za Italia). Dawa kama Fancida, Amodiaquin na qunin zimepoteza ubora wa kupambana na malaria kwa ukanda wa kitropoki hasa Pwani. Wtaalamu wanadai zitaingizwa kwa tiba ya dozi ya kuanzia siku 3. Dawa za malaria imekuwa ni majaribio sasa...

Waliokuuzia

walikudanganya!kuugua malaria kuko palepale kama hujikingi kung'atwa na mbu.Kwa sasa hakuna dawa inayoweza kutumika na usiugue maralia muda mrefu.Binafsi nimetumia dawa nyingi kama hiyo Artequin,Artequick,Duo cotexin,Metakefin,Fansidar,ALU,na Artemether inj. lakini maralia inajirudia tu baada ya mwezi!Nilikuja kupata dawa inayoitwa Arco nikaipenda sana kwani licha ya kumeza x moja tu sikusumbuliwa na maralia muda mrefu.Nimeitafuta tena hivi majuzi nimeambiwa ati haipo kabisa nchini sijui kwa nini maana hata taarifa huwa hazipo rasmi.Kwa sasa nimetumia Chloroquine imenisaidia vizuri mno ingawa nayo ilipigwa marufuku kisiasa tu ili wajanja watengeneze ulaji.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Niliambiwa chloroqiluine hazipo sokoni. Zinapatikana wapi kwa Dar?
Artequick na Arco inasemekana zimeondolewa sokoni kutokana na kufanya wagonjwa wa malaria kujenga usugu wa dawa. Kwa kiasi cha dozi ya mara moja au mbili haziui vyema wadudu wa malaria. Hii ipo kwa Metacalfin nazo za dozi moja (za Italia). Dawa kama Fancida, Amodiaquin na qunin zimepoteza ubora wa kupambana na malaria kwa ukanda wa kitropoki hasa Pwani. Wtaalamu wanadai zitaingizwa kwa tiba ya dozi ya kuanzia siku 3. Dawa za malaria imekuwa ni majaribio sasa...

Kwa Dar sifahamu zinapatikana wapi kwani sipo huko ila huku mikoani zipo tu kwenye baadhi ya famasi ila wanauza kwa kificho na hazijasajiliwa hata hivyo tunatumia tu kwani hata zilzosajiliwa ni majanga tu na hawa wanaosajili si wakweli hata kidogo maana wao hata kitu kizuri wanaita feki na mafeki yao wanayoyasajili ndiyo yanapigiwa debe.Nilikuwa Uganda nikatumia dawa nzuri kabisa nilipozitafuta hapa nikaambiwa eti ni feki hazijasajiliwa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Siku nyingine tumia ALU (mseto) ni dawa nzuri sana na ina few side effects, fuata ushauri wa dr namna ya kutumia, usijali kuhusiana na uwingi au urefu wa dozi
 
Back
Top Bottom