Arudisheje hisia kwa mumewe? ...Msaada tafadhali

Arudisheje hisia kwa mumewe? ...Msaada tafadhali

Babu ndio maana likatumika neno naomba ushauri, kama hujisikii kutoa ushauri kwa kuwa hakuna cha kushauri si ni bora ukakaa pembeni na kuvuta kiko chako?
Kwa nini usituache wenye muda wa kupoteza, tuendelee kuupoteza?
Ndo Ushauri huo aliotoa ODM au hujamuelewa?
 
Hapa sasa naamini umeamka hahahahahah the bottom ujumbe hapa ni kuwa aendelee tu kula ila asimshike kipofu mkono!! So asahau mambo ya kuwa mke mwema na blablah zake?! LOL Babu nidai zawadi yako leo
Na unajua nilivyo king'ang'anizi wa kudai?

Ka swali ka uzushi: What if ukampa ushauri afu asiufanyie kazi?
Kwa mfano ukachukua ushauri wa watu hapa kuwa mwache aendelee kubanjuka na mshefa nawe kwa kiherehere ukaenda kumpa.......... baada ya mwezi akarudisha mapenzi ya dhati kwa mumewe..........afu kwenye umbea wa kitandani akamsimulia mumewe ushauri wako..........Uko tayari kuzaa na mmewe?.....

MORAL: Bibi na Bwana Wakigombana, Shika jembe ukalime, wakipatana shika kapu ukavune.
 
Mbu bahati mbaya sana kaka zetu wengi tukishaolewa huwa wanakuwa kama wametufuta kwenye mioyo yao kama ndugu tunabakia kusubiri kukutana kwenye shughuli za kifamilia au kuzikana, Wachache sana wenye uwezo na moyo wa kuwatetea dada zao wanaonyanyasika kwenye ndoa sijui ndo wanaogopa kuambiwa wanaingilia?? Lakini cha ajabu sie kina dada na vimbelefront vyetu kuwasakama mawifi zetu ooh usitunyanyasie kaka yetu, unamtesa kaka yetu...na saa nyingine hata kama hanyanyaswi tunajifanya Knight Security kwao.

MJ1, for the first time i beg to differ, strongly!!!

the reverse is true.... jiulize kwanini kaka hawana issues sana na shemeji zao
 
Angetaka nilishike jembe nikalime asingekuja kuomba ushauri.

Umejuaje natafuta wa kuzaa naye?
 
MJ1, for the first time i beg to differ, strongly!!!

the reverse is true.... jiulize kwanini kaka hawana issues sana na shemeji zao
Allowed...

Ndo unijuze MTM am always a learning child you know me!
 
Aisee mwanajamiiOne, naomba umwambie Mbu aache kutubandikia picha za marehemu hapa jamvini kabla sijaripoti kwa mod aifunge hii sredi..........mpango wa kulizana mbele ya mkoloni nani anautaka?

Afu huyo dada mrembo namna hiyo ilikuwaje akaolewa na chizi?
 
Mbu bahati mbaya sana kaka zetu wengi tukishaolewa huwa wanakuwa kama wametufuta kwenye mioyo yao kama ndugu tunabakia kusubiri kukutana kwenye shughuli za kifamilia au kuzikana, Wachache sana wenye uwezo na moyo wa kuwatetea dada zao wanaonyanyasika kwenye ndoa sijui ndo wanaogopa kuambiwa wanaingilia?? Lakini cha ajabu sie kina dada na vimbelefront vyetu kuwasakama mawifi zetu ooh usitunyanyasie kaka yetu, unamtesa kaka yetu...na saa nyingine hata kama hanyanyaswi tunajifanya Knight Security kwao.

Nakubaliana nawe.

Iwapo kina kaka wangekuwa wanaingilia matatizo haya, hizi kesi za unyanyasaji zingepungua kwa kiwango kikubwa.
Ukweli ni kwamba wengi hutumia kigezo, "aah, mambo ya kina mama hayo, au kawaambie wazee...!"
 
Hakuna mwanaume mgumu duniani

Kama ni mgumu basi asingependa............. remember huyu mwanaume hajui kwamba mkewe anacheat, so if the lady decides to quit cheating, becomes a good woman at home and "massage their relationship at home" anaweza kuopen na kumsaidia mumewe na yeye mwenyewe how best to run their family

HAKUNA MWANAUME MGUMU DUNIANI, THAT IS IT.............. NI PRETENDENCE, TU, NA AKIWA MGUMU KWA WANAWAKE BADI WAWEZA KUTA MLAINI KWA WANAUME IT IS NATURAL;

kuna mahali MJ1 kasema huyu mume amejua...MJ1 saidia hapa.
 
Angetaka nilishike jembe nikalime asingekuja kuomba ushauri.

Umejuaje natafuta wa kuzaa naye?
Hahahahaha hili sredi limenifumbua macho jinsi ulivyo mbea.... Najaribu kuvuta picha wakati anakusimulia lazima ulikuwa umeshika tama huku ukimpiga na tuswali twa uzushi khaa......vijineno kama .... "acha masihara dada"........"kweli?"..........."Siamini".......... "Halafu"....... Havikukosekana wallah
 
Aisee mwanajamiiOne, naomba umwambie Mbu aache kutubandikia picha za marehemu hapa jamvini kabla sijaripoti kwa mod aifunge hii sredi..........mpango wa kulizana mbele ya mkoloni nani anautaka?

Afu huyo dada mrembo namna hiyo ilikuwaje akaolewa na chizi?

there you go,...lengo, nia na madhumuni ilikuwa kuamsha hisia hizo...."dada mrembo kaolewa na chizi!"...
utakubali dadako ale mkong'oto na kunyanyasika kiasi cha kupoteza maisha kwa kisingizio cha ndoa?

Hebu nijibu hilo kwanza kabla sijakuuliza iwapo utamsamehe huyu 'dada' wa MwanajamiiOne huko
alikokwenda tafuta faraja.
 
Nakubaliana nawe.
Iwapo kina kaka wangekuwa wanaingilia matatizo haya, hizi kesi za unyanyasaji zingepungua kwa kiwango kikubwa.
Ukweli ni kwamba wengi hutumia kigezo, "aah, mambo ya kina mama hayo, au kawaambie wazee...!"
Mkuu Mbu ebu niambie unaaanzaje kuingilia Ndoa ya Dadako? Mi nachojua kama dada yako amekuja kukuomba ushauri utamsaidia, sio kutoka na kwenda kwenye nyumba na kuanza kumpiga mkwala Mumewe? hivi akikujibu mchukue ukamuoe wewe utafanyaje?
 
Aisee mwanajamiiOne, naomba umwambie Mbu aache kutubandikia picha za marehemu hapa jamvini kabla sijaripoti kwa mod aifunge hii sredi..........mpango wa kulizana mbele ya mkoloni nani anautaka?

Afu huyo dada mrembo namna hiyo ilikuwaje akaolewa na chizi?
.........Amekusikia ODM nakutaka radhi kwa niaba.

Eti akaolewa na chizi!! una mambo wewe
Nakubaliana nawe.

Iwapo kina kaka wangekuwa wanaingilia matatizo haya, hizi kesi za unyanyasaji zingepungua kwa kiwango kikubwa.
Ukweli ni kwamba wengi hutumia kigezo, "aah, mambo ya kina mama hayo, au kawaambie wazee...!"

Mbu MTM amenibishia hapa hebu tusubirie. Mimi nilikuwa na feelings kuwa pengine kwa kuwa na wengi wao at some point wanakuwaga maabuser so ukipeleka kesi ya abuser mwenzao kwao ni kama wanakushangaa vile?? ni sawa na kesi ya ngedere uipeleke kwa nyani!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Allowed...

Ndo unijuze mwaya MTM am always a learning child you know me!
Hahahahaha......... haya maneno mazuri sana kwenye kusaka kaumbea...... ngoja nisepe naona nachakachua sredi isiyochakachuka..........ngoja nimjaribu klorokwini aje ajaribu bahati yake.
 
MJ1 kuna siku mwenyewe na kimbelembele changu nikapeleka kesi huwezi amini jibu nililopata mbona mambo ya kawaida hayo mdogo wangu hata sie twafanyaga hayo ushaur niliopokea ni jinsi gani ya kuendelea kuvumilia na kunyenyekea balaa tupu.

Mbu MTM amenibishia hapa hebu tusubirie. Mimi nilikuwa na feelings kuwa pengine kwa kuwa na wengi wao at some point wanakuwaga maabuser so ukipeleka kesi ya abuser mwenzao kwao ni kama wanakushangaa vile?? ni sawa na kesi ya ngedere uipeleke kwa nyani!![/QUOTE]
 
there you go,...lengo, nia na madhumuni ilikuwa kuamsha hisia hizo...."dada mrembo kaolewa na chizi!"...
utakubali dadako ale mkong'oto na kunyanyasika kiasi cha kupoteza maisha kwa kisingizio cha ndoa?

Hebu nijibu hilo kwanza kabla sijakuuliza iwapo utamsamehe huyu 'dada' wa MwanajamiiOne huko
alikokwenda tafuta faraja.
Mdogo wangu kipindi flani alinipigia simu kuwa mmewe kamcharaza makonde.... akafika mbali kuisema familia yetu vibaya........ Nilikamata Dar Express kesho yake nikatua Arusha wanakoishi. Shughuli iliyotokea, mpaka leo haipiti wiki lazima anipigie simu na kuniamkia "shkamoo shemeji". Kama ni member wa JF akaisoma hii thread basi tena ndo kashaijua ID yangu...........Nadhani nitakuwa nimekujibu indirect........ Nasubiria swali la pili.
 
Mkuu Mbu ebu niambieunaaanzaje kuingilia Ndoa ya Dadako? Mi nachojua kama dada yako amekuja kukuomba ushauri utamsaidia, sio kutoka na kwenda kwenye nyumba na kuanza kumpiga mkwala Mumewe? hivi akikujibu mchukue ukamuoe wewe utafanyaje?
beat1.jpg

...Hivi, kweli unaweza jifanya mpofu na kiziwi ukiona dada'ko anakula mkong'oto wa Mbwa mwizi?
khaaa, acheni nidhamu za woga bana. Kuniolea dada yangu haina maana hiyo mahari itumike kumdhalilisha.

Haikubaliki. Haina nitaanzaje anzajhe wala nini, ni mapambano juu. Nimezaliwa Mwanaume nimlinde na kumtetea dadangu bana. Damu nzito..
 
kuna mahali MJ1 kasema huyu mume amejua...MJ1 saidia hapa.

Ni kweli nyamayao mdada mumewe alijua kuwa mke aLIcheat na akamsamehe baada ya kuamini na mke kukiri kuachana na Mshefa. Sasa yeye mdada anajaribu kuzirejesha hisia zake kwa mumewe lakini kwa mshefa amekuwa kama Mbwa mbele ya chatu vile!
 
Back
Top Bottom