Arumeru: Wanafunzi walazimika kujisaidia porini kwa kukosa huduma ya vyoo

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
wakosa.jpg

​
Zaidi ya wanafunzi elfu moja wa shule ya msingi Olimringaringa iliyopo kijiji cha Kimnyaki wilayani Arumeru wako hatarini kupata magonjwa ya milipuko kutokana na kulazimika kujisaidia porini kwa kukosa huduma ya vyoo.

Akizungumzia changamoto hiyo ya uhaba wa matundu ya vyoo mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi.Vick Laizer amesema tatizo hilo limedumu kwa muda mrefu.

Ili kutatua changamoto hiyo wadau wa elimu kutoka shirika la SOS Children’s Villages limetoa msaada wa mifuko hamsini ya saruji pamoja na mchanga tani kumi na nne kwa ajili ya ujenzi wa choo kipya.

Wakati wa makabidhiano hayo shirika la SOS Children’s village limesema litaendelea kumuenzi aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt. John Magufuli kwa kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwasaidia watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu ili dhamira yake ya kuhakikisha elimu kwa wote inafikiwa.

Chanzo: ITV
 
Mnataka msaada wa choo?

Yaani msaada wa Tsh laki 9 hadi mnarusha ITV hizi ndio zile NGO uchwara.

Hii NGO ndio ile ilijenga Shule kwa ajili ya yatima halafu shule ikageuzwa kuwa ya watoto wa vigogo?
 
Jamani hatari, viongozi wapo,mkuu qa afya yupoHii ndio hatari ya wakuu kukaa maofisini bila kwenda field na kuweka mipango ya kutembelea maeneo yao na kujua changamoto zilizopo!
 
Mnataka msaada wa choo?

Yaani msaada wa Tsh laki 9 hadi mnarusha ITV hizi ndio zile NGO uchwara.

Hii NGO ndio ile ilijenga Shule kwa ajili ya yatima halafu shule ikageuzwa kuwa ya watoto wa vigogo?
Ati nini?☹️☹️
 
Wa ar vipi tena!
Na matanzanite yote hayo?
Dah sio poa mambo mengine muwe munafichaga nyie ebo
Si mungeenda kwa yule laizer tu kimya kimya
Ingefaa zaidi mali ya sehemu husika ianze kufaidisha watu wake kuliko kwenda kuchanga interchange ambazo wananchi wa mali ilipotolewa haiwafaidishi☹️☹️☹️
 
wakosa.jpg

​
Zaidi ya wanafunzi elfu moja wa shule ya msingi Olimringaringa iliyopo kijiji cha Kimnyaki wilayani Arumeru wako hatarini kupata magonjwa ya milipuko kutokana na kulazimika kujisaidia porini kwa kukosa huduma ya vyoo.

Akizungumzia changamoto hiyo ya uhaba wa matundu ya vyoo mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi.Vick Laizer amesema tatizo hilo limedumu kwa muda mrefu.

Ili kutatua changamoto hiyo wadau wa elimu kutoka shirika la SOS Children’s Villages limetoa msaada wa mifuko hamsini ya saruji pamoja na mchanga tani kumi na nne kwa ajili ya ujenzi wa choo kipya.

Wakati wa makabidhiano hayo shirika la SOS Children’s village limesema litaendelea kumuenzi aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt. John Magufuli kwa kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwasaidia watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu ili dhamira yake ya kuhakikisha elimu kwa wote inafikiwa.

Chanzo: ITV
Halafu unanunua ndege kwa cash..then unapata hasara ya bilioni 60 ...
 
Fence tu ya anapokaa mtetezi wa wanyonge kijijini kwake unajenga vyoo 500 bila kusubiria msaada wa mabeberu kujengewa vyoo.
 
Halafu unanunua ndege kwa cash..then unapata hasara ya bilioni 60 ...
Sio ndege tu, kujenga ikulu mpya kwa bilioni 500 for nothing hali iliyopo ni toshelevu ndo mseme angetoka,Mungu ana makusudi yake kaona mbali kutuepusha mateso ya milele.
 
Ingekua shule ya binafsi ingefungiwa ila kwa sababu ni ya wanyonge poa tu hata wakipata magonjwa ya mlipuko
 
Back
Top Bottom