Arusha: Afariki dunia akidaiwa kuchapwa viboko 280

Arusha: Afariki dunia akidaiwa kuchapwa viboko 280

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mkazi wa Sanawari, Wilaya ya Arumeru Mkoa Arusha, Nelson Mollel (32) amefariki dunia baada ya kudaiwa kupewa adhabu ya kuchapwa vikobo 280 kutokana na tuhuma ya kumtukana mama yake mzazi.

Wazee wa jamii ya Kimaasai na Kimeru wilayani Arumeru mkoani Arusha wamekuwa wakitoa adhabu ya kuwachapa viboko vijana ambao wamekuwa wakibainika kufanya matendo ambayo ni kinyume cha maadili.

Miongoni mwa matendo hayo ni pamoja na kutukana wazazi, kunywa pombe mchana na kufanya vurugu, kuvaa nguo ambazo sio za heshma na kufanya uhalifu ikiwepo kupigana.

Mama mzazi wa marehemu Nelson, Janeth Kimario amesema kijana wake alimtukana Matusi ya nguoni Januari 1, 2023.

Amesema baada ya kutukwanwa ndipo alimwambia baba yake mdogo, Abel Mboya (45) ambaye alifanikiwa kumpata Nelson na kumpeleka porini na kuanza kumchapa fimbo akiwa na watu wengine.

“Lakini adhabu ilikuwa kubwa sana na kweli alistaili kuchapwa ila wamezidisha hadi nimempoteza mwanangu," amesema.

Dada wa marehemu, Jackline Elias Mollel amesema mdogo wake amepigwa viboko 280 badala ya fimbo 70 vinavyopaswa kwa mujibu wa taratibu zao.

"Hii ni mila na desturi zetu, sisi Wamasai lakini wamezidisha na pia wamemchapa kwa sifa sana, wamemvunja mbavu miguu na mikono," amesema.

Polisi Wilaya ya Arumeru wamethibitisha kupokea taarifa hizo hata hivyo, afisa mmoja wa polisi katika wilaya hiyo jina linahifadhiwa amesema msemaji ni Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha.

"Wewe unajua utaratibu, msemaji ni kamanda na nadhani mkimfuata atawapa taarifa rasmi ni kweli tukio hilo limeripotiwa,"amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Justine Masejo alipotafutwa kwa simu kuelezea mauaji hayo hakupatikana kutokana na simu yake kutopokelewa.

MWANANCHI
 
Yani nimeona hyo video Azam Tv kwenye taarifa ya habari.. nimesikitika sana..wameshika fimbo 3 wanapokezana kwa nguvu mnoo zile fimbo za kimasai..mwingine kamkalia krb na shingo anambonyeza kichwa kisiamke...ni unyamaa ni unyamaa..mila zingine ni za kishamba..haya sasa wameua alietukanwa(mama) anamlilia mwanae..
 
Kumbe nimemic mengi ngoja nisubili saa 5:00 usiku marudio niione
 
Attachments

  • IMG_20230111_231306.jpg
    IMG_20230111_231306.jpg
    337.2 KB · Views: 11
Watoto wa Sasa walaini Sanaa...

Sabini moja tu Kwa mwaka ameondoka!?

Ilikuwa ni Sabini karibu kila mwezi na maisha yanaendelea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wa Sasa walaini Sanaa...

Sabini moja tu Kwa mwaka ameondoka!?

Ilikuwa ni Sabini karibu kila mwezi na maisha yanaendelea...

Sent using Jamii Forums mobile app
Mshaanza wazee wa kujifanya miamba

Mkuu hakuna fahari yoyote kutandikwa kama mnyama, wapo wanaotandikwa hivyo na wanaishia kuwa masugu na makatili, na wapo wanaopewa adhabu za kawaida na wanaelewa wananyooka

Hizo adhabu zingekuwa zinawasaidia, basi leo hii jamii isingekuwa imejaa mivibaka na mitapeli kila kona, sababu hata nao huwa wanajisifia kuwa walilelewa kigumu utadhani sifa
 
Hizo adhabu zingekuwa zinawasaidia, basi leo hii jamii isingekuwa imejaa mivibaka na mitapeli kila kona, sababu hata nao huwa wanajisifia kuwa walilelewa kigumu
I'm not in the mood..

Asante Kwa ku reply post yangu.

Kumbatia culture yako, wacha wengine nao wajivunie na ya kwao.. Ndio raha hiyo ya uhuru wenyewe.

Mbaya tu ni kutaka kuishi Kwa kukumbatia culture za wengine kutaka kuzileta kwenye maisha yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshaanza wazee wa kujifanya miamba

Mkuu hakuna fahari yoyote kutandikwa kama mnyama, wapo wanaotandikwa hivyo na wanaishia kuwa masugu na makatili, na wapo wanaopewa adhabu za kawaida na wanaelewa wananyooka

Hizo adhabu zingekuwa zinawasaidia, basi leo hii jamii isingekuwa imejaa mivibaka na mitapeli kila kona, sababu hata nao huwa wanajisifia kuwa walilelewa kigumu utadhani sifa
Boraaa usemee wee cc, tukisema wenginee tutaambiwa kuwa tunateea taasisi fulaani.
 
Back
Top Bottom