Arusha: Afisa Mtendaji ahukumiwa miaka 20 jela kwa ufujaji wa fedha

Arusha: Afisa Mtendaji ahukumiwa miaka 20 jela kwa ufujaji wa fedha

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Agosti 24, 2022 Jamhuri imeshinda katika Shauri Na. ECO. 90/2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha. Shauri hili lilimhusu, JULIUS K. MBISE, aliyeshtakiwa kwa makosa ya Ufujaji na Ubadhirifu, Matumizi Mabaya ya Madaraka pamoja na Kuisababishia Serikali Hasara, kinyume na vifungu vya 28 (1), 31 vyote vya PCCA, Cap 329 na aya ya 10 (1) ikisomwa pamoja na Jedwali la kwanza la Sheria ya EOCCA, Cap 200 [R.E 2019].

Mshtakiwa ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya KIKWE, alifuja kiasi cha sh Milioni Saba (7,000,000/=) fedha za Halmashauri ya (W) ya Meru.

Mshtakiwa amepatikana na hatia na amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 Jela na kutakiwa kurejesha kiasi cha sh. Milioni Saba (7,000,000/=) alizofuja.
 
Duh!! Hivi wale akina ESCROW, Profesa Anna Tibaijuka na zile pesa ya mboga si watafungwa karne?? Au mtego ni wa dagaa tuu, papa wanautoboa???
 
Wezi wakubwa hukumu ndogo, wezi wadogo hukumu kubwa
 
Back
Top Bottom