BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mkazi wa kijiji cha Geilailumbwa kilichopo wilayani Longido mkoani Arusha, Lemindia Lesiria amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka binti mwenye umri wa miaka 16.
Mbali na kosa hilo mtuhumiwa huyo na rafiki yake, Kulasa Mandeu wamekutwa na hatia katika makosa mengine mawili ambayo ni shambulio la mwili na kumfanyia ukatili mtoto ambapo wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kila kosa na faini ya Sh2 milioni kama fidia ya kumjeruhi.
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne Desemba 27,2022 na Hakimu Mkazi Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha, Regina Oyier ambapo amesema matukio hayo ya ukatili wa mtoto na kumjeruhi yalitokea Septemba 13 na 14, 2022 katika kijiji cha Gelailumbwa kilichopo wilayani humo baada ya binti huyo ambaye ni mke wa Lesiria kuvunja chupa ya dawa ya mifugo.
Akisoma hukumu hiyo, hakimu huyo alieleza kuwa mahakama imewatia hatiani katika makosa yote matatu baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri kuthibitisha makosa hayo pasipo na shaka ambapo katika kesi hiyo ya jinai namba 23/2022 katika kosa la kwanza lililokuwa linawakabili watuhumiwa wote ni kusababisha majeraha.
Kosa hilo kinyume na kifungu cha 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ambapo inadaiwa Septemba 14, 2022 washtakiwa hao kwa pamoja walisababisha majeraha kwa binti huyo aliyetajwa kama (MK) kwa kumchapa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia fimbo.
Kosa la pili lilikuwa ni ukatili kwa mtoto ambalo linawakabili wote wawili, inadaiwa wakiwa na jukumu la kumjali binti wa miaka 16 walimtendea matendo ya kikatili ambayo yalileta madhara katika afya yake kwa kumchapa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia fimbo.
Kosa la tatu lililokuwa linamkabili Lesindia ni ubakaji ambapo inadaiwa kati ya kipindi cha mwaka 2020 hadi Septemba 14, 2022 alifanya mapenzi na binti huyo mwenye umri wa miaka 16 kwa sasa ambapo mwaka 2020 alikuwa na miaka 14.
“Kulikuwa na majeraha yaliyopelekea majeraha ya mwisho, haibishaniwi kwamba binti huyo mhanga kwenye shauri hili alipata majeraha makubwa kwenye mwili wake na katika hili mahakama iliangalia uthibitisho wa kitabibu wa shahidi namba 5 ambaye ni daktari aliyempokea na kumtibu binti huyu huko Longido.
“Vitendo vya washitakiwa kumchapa huyu binti sehemu mbalimbali za mwili wake, kumfunga kwenye mti, kurarua shuka lake na kumuacha uchi, kumlazimisha alale nje usiku, kufunga kamba na kumpeleka msituni kumpiga na kumtelekeza akiwa amefungwa mikono na miguu, vingeweza kuhatarisha maisha yake. Kumuacha porini angeweza kushambuliwa na mnyama mkali,” amesema.
Kuhusu kosa la tatu, hakimu huyo amesema mshitakiwa wa kwanza alikuwa anamwingilia kimwili binti huyo na haina ubishani kwa sababu daktari amethibitisha binti alikuwa ameingiliwa na hata binti alikiri mahakamani na mumewe huyo alikiri na kuwa ni kinyume na Sheria ya Ndoa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Amesema mahakama imewatia hatiani katika makosa yote yaliyothibitika pasipo kuacha shaka yoyote ambapo kosa la kwanza wanahukumiwa kifungo cha miaka mitano, kosa la pili kifungo cha miaka mitano na kosa la tatu kwa mshitakiwa wa kwanza kifungo cha miaka 30 na adhabu zinaenda sambamba.
Wakili wa serikali katika shauri hilo, Jackline Linus aliomba mahakama itoe adhabu kali kwa washitakiwa hao kwa vitendo walivyofanya ili iwe fundisho kwa jamii huku katika utetezi washtakiwa hao waliomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwa kuwa wana matatizo ya kiafya.
MWANANCHI