Arusha: Aliyejeruhi mke anyimwa dhamana

Arusha: Aliyejeruhi mke anyimwa dhamana

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limemfikisha mahakamani mtuhumiwa Isaack Mnyangi (45)Mkazi wa Sombetini Jijini Arusha na kusomewa shtaka moja la shambulio la Kudhulu Mwili.

Mbele ya Hakimu ,Jenifa Edward wa mahakama ya wilaya Arusha,katika kesi namba 80 ya mwaka 2023,mwendesha mashtaka wa serikali ,Charles Kagilwa akisaidiana na Godfrey Nungu na Callorine Kasubi,alidai mnamo Mei 23 mwaka huu majira ya saa tano usiku katika eneo la Osunyai kwa Diwani jijini Arusha

Mshtakiwa Mnyangi alimshambulia Jackline Mkonyi(38)ambaye ni mke wake na kumng'oa jino moja, kumpiga kwa Mkanda Usoni na mgongoni na maeneo mengine ya mwili wake na kumsababishia madhara.


Hata hivyo mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na upande wa jamhuri ulidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuiomba mahakama kumsomea mshatakiwa maelezo ya awali .

Akisoma maelezo kwa mshtakiwa, wakili wa jamhuri Godfrey Nungu alidai mnamo Mei 23 mwaka 2023,majira ya saa tano usiku, mhanga (Jackline)alisikia mlio wa honi ya gari nje ya geti na alipojaribu kwenda kufungua alibaini kuwa mtoto wake wa kiume tayari alikuwa ameshafika getini kufungua

Wakili Kagilwa alieleza mahakama kuwa Mhanga aliendelea kumsubiria Mhuhumiwa sebuleni lakini mtuhumiwa alipoingia ndani hakumsalimia badala yake alipitiliza chumbani.

Alidai kuwa Mhanga alimfuata chumbani lakini mhuhumiwa alimshika mkono na kumvuta na kusha kumtupa Sebuleni kwenye Kochi.

Alieleza kuwa Mtuhumiwa alianza kumpiga Mhanga kwa ngumi Usoni na kuendelea kumpiga mateke na kumkanyaga na baadaye alichomoa mkanda wake wa suruwali na kuendelea kumpiga katika meneo mbalimbali ya mwili wake ikiwemo mgongoni.

Alidai kwamba mtuhumiwa alichukua Plaizi na kumng'oa jino moja la mbele, ambapo mhanga alitokwa na damu nyingi akiwa hajitambui.

Wakili aliendelea kudai kuwa, mhuhumiwa alimwacha Mhanga akiwa na majeraha makubwa mwilini akiwa anavuja damu nyingi hapo sebuleni na kwenda kuwaamsha watoto na baadaye alimpigia simu mama yake na Mhanga(mama mkwe)na kumweleza kuwa anamleta mtoto wake nyumbani.

Alieleza kuwa mhanga huyo alipakia kwenye gari pamoja na watoto na kwenda hadi Sinoni Daraja mbili nyumbani kwa mama mkwe na kumtelekeza na kutoweka kusikojulikana .

Alidai kwamba siku iliyofuata Mhanga alipelekwa hospitali na kushondwa majeraja na daktari alithibitisha kuwa Mhanga alikuwa amng'oa jino moja na kutobolewa sehemu ya jicho lake.

Alidai uchunguzi wa polisi ulifanyika na mtuhumiwa alikamatwa mei 27 mwaka huu akiwa amejificha kwa mchungaji eneo la Himo Mkoani Kilimanjaro na baadaye kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo upande wa jamhuri ulidai kuwa utakuwa na mashahidi watano na kielelezo kimoja.

Hata hivyo upande wa jamhuri uliwasilisha maombi madogo ya kupinga dhamana kw mshtakiwa na kueleza mbalimbali ikiwemo, mshtakiwa kutoroka baada ya tukio,hali ya taharuki kwa wananchi pamoja na kujenga chuki kwa mkewe na watoto.

Mshtakiwa alipelekwa rumande katika gereza kuu la Kisongo,Arusha hadi juni 13 mwaka huu.
 
Hasira hasaraa!
Jogoo tu hukuti anapigana na kuku,beberu akupigana na jike,ng'ombe na wengineo.ila mwanaume anampiga mwanamke.


Halafu avue hiyo jezi anatudhalilisha
 
Yani hayo yote yanafanyika wote hawaongee wako kimya kimya tu, hamna watu waongo kama wanawake duniani......
 
Kuoa wanawake wajuaji, wanye vibuli, wasomi, ndo matokeo yake bora upate wa darasa la saba mwenye kutii mme wake, hao walikua na ugomvi wa siku nyingi sana na kuendelea kulazimisha ndoa ndo matokeo yake.
 
Kuna Daktari alitilia Shaka usahihi wa tukio hili Kuwa 100% Sasa na Mimi naungana naye. Daktari alihoji Mtu aliyetobolewa jicho na kung'olewa jino bila ganzi anawezaje kulazwa siku 1 tu hospitali na akatoka bila operation sehemu jicho lilipong'olewa?

Mashitaka yaliyosomwa dhidi ya mtuhumiwa yamenifumbuwa macho kutokana na elimu ya sheria niliyopata kabla sijajikita kwenye uandishi wa kiuchunguzi.

Huwezi kumshitaki mtuhumiwa aliyeng'oa Mtu jicho/jino Kwa kosa la dogo la shambulio la kudhuru mwili badala ya kosa sitahiki la Kujeruhi. Labda kama kuna mpango wa kumbeba mshtakiwa apigwe faini vinginevyo Tangu awali tukio hili ni exaggerated.
 
Daktari aliyelitolea ufafanuzi hili jambo nilimuelewa sana, kuna walakini wa huyo mwanamke kuchunguzwa vizuri, maelezo yake yana ukakasi sana.
 
Kuna Daktari alitilia Shaka usahihi wa tukio hili Kuwa 100% Sasa na Mimi naungana naye. Daktari alihoji Mtu aliyetobolewa jicho na kung'olewa jino bila...
Ile post ya daktari hata mimi niliiona.

Akasema kama huyo dada katobolewa jicho na kung'olewa jino kweli basi waziri mwenye dhamana amvue udaktari wake, maana mtu aliefanyiwa hivyo sio rahisi kutoka hospital kwa siku moja tu.

Akasisitiza sana jicho kwasababu nae ni daktari wa macho..

Wanawake ni waongo sana aisee.
 
Kwa jinsi Baba wa huyu mwanamke alivyoelezea nashindwa kuwa na huruma,sisemi kupigwa sawa lakini sometimes ni sawa kabisa.
 
Sometimes unatamani ungeamkia hosp au mortuary kuliko mambo yanayokukuta.

Aliimba na Fanuel Sedekiya miaka mingi iliyopita, kumbe shetani alikuwa anamfuatilia ili amwangamize.

Pole Izaki, pole zaidi Dada uliyeumizwa
Huyo Izaki pole ya nini?

Akaonyeshe umwamba jela.

Mwanamke kama anazingua unapiga chini unavuta chombo kipya kikali zaidi. Jamaa ana hasira za kishamba nahisi atakua mmeru huyu bwege.
 
Atamsamehe mmewe huyo dada nyie subirini tu
 
Kuoa wanawake wajuaji, wanye vibuli, wasomi, ndo matokeo yake bora upate wa darasa la saba mwenye kutii mme wake, hao walikua na ugomvi wa siku nyingi sana na kuendelea kulazimisha ndoa ndo matokeo yake.
Wanawake siku hizi wamejaa viburi na jeuri sababu wanatiana sana ujinga hawa kupitia hicho wanacho kiita eti haki sawa,haitakuja kutokea mwanamke na mwanaume wawe sawa katika dunia hii
 
Huyo Izaki pole ya nini?
Akaonyeshe umwamba jela.
Mwanamke kama anazingua unapiga chini unavuta chombo kipya kikali zaidi. Jamaa ana hasira za kishamba nahisi atakua mmeru huyu bwege.
Mambo sio rahisi hivyo mzee labda kama hujawahi kuoa na huna familia
 
Back
Top Bottom