#COVID19 Arusha: Aliyesimamishwa kwa mzaha wa chanjo ashangazwa na hatua dhidi yake

#COVID19 Arusha: Aliyesimamishwa kwa mzaha wa chanjo ashangazwa na hatua dhidi yake

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Waliochanjwa.jpg

Mkuu wa idara elimu msingi halmashauri ya Jiji la Arusha, Omary Kwesiga amesema ameshangazwa kusimamishwa kazi akidaiwa kufanya igizo la kuchomwa chanjo ya ugonjwa wa Covid-19.

Amesema picha za video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha kuwa hakuchomwa chanjo hiyo zimechezewa, na kubainisha kuwa alichanjwa.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Agosti 6, 2021 Kwesiga amesema anashangazwa na video hiyo, "nimezuiwa kuongea na vyombo vya habari kulingana na maadili ya kazi na kikubwa mimi nimechanjwa nina ushahidi na nipo Salama."

Ofisa huyo na ofisa muuguzi msaidizi wa hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Scolastica Kanje leo wamesimamishwa kazi na mamlaka zao kwa tuhuma za kufanya igizo la kuchanja.

Kwa takribani siku tatu video hiyo inayomuonyesha Kwesiga na Kanje wakifanya kile ambacho kimetafsiriwa ni maigizo imebua mjadala mitandaoni.

Chanzo: Mwananchi

Pia, soma:
 
Hoja yake ni yamsingi, kwamba hakufanya maigizo, alichanja kweli.
Kuna mmoja pembeni akasema ili kuhamasisha wengine wachome. Ina maana ilikuwa ni kuigiza tu ili na wengine waone wakachome
 
Naona kama kuna jambo haliko sawa hapa, asihukumiwe kabla hajasikilizwa, kwasababu nikiangalia umri wake haufanani na ule utoto unaoonekana kwenye ile video, nikiongezea na kauli yake kwamba ile video imechezewa, naanza kumuamini.
 
Huyu mzee anazeeka vibaya,nani alimtuma ajirekodi na kurusha mtandanoni?
Kama anajua picha zinachezewa,kwanini azirushe yeye mwenyewe bila kujiridhisha na maudhui yaliyomo ndani?
Aliyekuwa akirekodi alisema "Afisa Elimu akichoma korona" na si chanjo ya corona.
Huoni kama watu wanaweza kufikiri corona inasambazwa kwa makusudi?
Aende akalee wajukuu nyumbani apishe wenye uwezo wa kazi wafanye kazi kwa weledi.
 
Back
Top Bottom