Arusha: Anayedaiwa kubomoa nyumba ya ndugu yake, achomewa nyumba na wananchi

Arusha: Anayedaiwa kubomoa nyumba ya ndugu yake, achomewa nyumba na wananchi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Baadhi ya wananchi wa kata ya Sokoni 2 halmashauri ya Arusha leo Ijumaa Julai 9, 2021 wamechoma moto nyumba ya Ng'ida Loisulye anayedaiwa kubomoa nyumba ya ndugu yake, Benjamin Mollel kwa maelezo kuwa ameshinda kesi mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya nyumba hiyo iliyobomolewa, Mollel amesema leo mchana alishangaa kuona polisi na madalali wakifika katika nyumba hiyo na kuibomoa kwa maelezo kuwa ameshindwa kesi mahakamani.

“Mimi nina kesi na huyu ndugu yangu muda mrefu na tulishapelekana tulianzia ngazi za chini hadi tukafika mahakamani na tulishaweka kizuizi nyumba isibomolewe na kesi ilikuwa inatajwa tena Septemba 6, 2021 sasa huyu nashangaa leo amefika hapa kuja kubomoa wakati hatuna barua wala taarifa yoyote kuhusu tukio hili,” amesema Benjamini.

Diwani wa Sokoni 2, Obedi Melami amesema akiwa nyumbani kwake alipigiwa simu na kuelezwa kuhusu tukio hilo na alipofika eneo la tukio alikuta nyumba imebomolewa.

“Nimeshangaa tukio hili kufanyika bila taarifa yoyote kwa mtendaji wa kata, kijiji na hata mimi pia sikuwa na taarifa yoyote. Matukio ya namna hii lazima tupate barua ya kushirikishwa kisheria tukiwa kama viongozi wa kata ili tuweze kusimamia kwa umakini zaidi, lakini nashangaa sijui kilichofanyika," amesema diwani huyo.

Amesema muda mfupi baada ya nyumba hiyo kubomolewa, wananchi walivamia nyumba ya anayedaiwa kushinda kesi hiyo na kuichoma moto.

"Mimi nilimpigia simu OCD (mkuu wa polisi wa wilaya) wa Arumeru kumuuliza akasema yeye ndiye amewatuma polisi kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya mahakama kubomoa nyumba hiyo,” amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema polisi wanafuatilia mgogoro huo na taarifa rasmi itatolewa.
 
Arusha kwenye ardhi hawana undugu kabisaaa, ndo mana wanalogana sana
 
Back
Top Bottom